MTOTO wa hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Makongoro Nyerere, amekanusha taarifa zilizotambaa Katika mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa Mjane, Mama Maria Nyerere amefariki dunia. Akizungumza na Efm kwa njia ya simu kutoka nchini Uganda, Mheshimiwa Makongoro amesema familia imesikitishwa na mtu aliyevumisha taarifa hizo, nakwamba mama yao ni mzima. Hata hivyo amewataka Watanzania, kuacha tabia ya kuvumisha taarifa ambazo siyo za kweli kwani zinachangia upotoshaji kwa watu na badala yake kuwa na ufuatiliaji wa mambo kabla hawajaanza...
NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mheshimiwa ANNE KILANGO MALECELA, amekemea Wazazi wilayani Bagamoyo ambao wanakatisha watoto wao masomo, kwa kisingizio cha kukosa Ada, na badala yake hutumia gharama kubwa kuwafanyia watoto Ngoma za Kimila. Aidha amekemea Familia zinazoombea watoto wao wafeli katika Mitihani yao, ili kuepuka gharama za kusomesha. Mheshimiwa KILANGO ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wazazi, walezi, walimu, wanafunzi, wananchi na Viongozi mbalimbali katika mafahali ya saba ya kidato cha sita katika shule ya...
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi SEIF ALI IDD, amesema Viongozi wa kisiasa wanaowakataza wananchi wasishiriki zoezi la kura ya maoni mwezi Aprili mwaka huu ili kuipitisha Katiba inayopendekezwa, wana alama za Udikteta na pia wanakwenda kinyume na matakwa ya Demokrasia. Balozi SEIF ameyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja na kusema jambo hilo ni fedheha katika dunia mpya inayooongozwa kwa kufuata misingi ya Demokrasia na utawala bora. Ameeleza kwamba...
JAMII nchini imetakiwa kushirikiana na Serikali katika kudhibiti tatizo la matumizi ya dawa za kulevya kwa vijana kuanzia ngazi ya Familia kwakuwa vijana ndiyo nguvu kazi ya Taifa. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Afisa Mtendaji wa kata ya Temeke Elias Wawa amesema kuwa tatizo la matumizi ya dawa za kulevya linaanzia katika ngazi ya familia hivyo wazazi na walezi wanapaswa kuzungumza na vijana wao ili kuondokana na tatizo hilo . Aidha amewataka wazazi kutowakatisha tama...
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mheshimiwa Ali Nasoro Rufunga kuomboleza vifo vya watu 38 huku wengine 82 wakijeruhiwa usiku wa kuamkia jana tarehe 4 Machi, mwaka huu. Tukio hilo la kusikitisha limetokea katika Kata ya Mwakata iliyoko katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga kufuatia mvua kubwa ya mawe iliyonyesha ikiambatana na upepo mkali, hivyo kuathiri watu 3,500. Katika Kata Mwakata iliyoathiriwa zaidi, kaya 350 zimeathiriwa...
BAADHI ya Wajawazito katika Kata ya Tinde,Halmashauri ya Wilaya Shinyanga wamewalalamikia wahudumu wa Kituo cha Afya Cha Tinde, kuwadai fidia na kuzuia kadi za Kliniki. Wahudumu hao baada ya kuwapima wajawazito ,hudai shilingi 2000 kwa kila Mjamzito.Wakizungumza na Efm kituoni hapo,baadhi ya wajawazito wamesema tabia hiyo ni ya siku nyingi na imekuwa ni kero...
SERIKALI ya China imetoa Zaidi ya Shilingi Milioni 265 kwa ajili ya Ujenzi wa Miradi ya Maji mkoani Tabora. Akiwasilisha taarifa yake katika kikao cha Kamati ya Bunge jijini Dar es salaam,Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji,Mhandisi MBOGO FUTAKAMA amesema pesa hizo zimetolewa kwa ajili Mkoa wa Tabora ambao una matatizo ya upatikanaji wa Maji. Ameeleza kuwa fedha hizo zitatumika katika miradi mbalimbali katika mkoa huo na Wilaya zake ili kuboresha Miundombinu na hatimaye kupatikana kwa...
TANZANIA kwa kushirikiana na Uturuki inatarajia kujenga kituo kikubwa cha watu wenye ulemavu wa Ngozi- albino, ambacho kitakuwa na huduma mbalimbali muhimu ikiwamo shule na afya. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amesema kituo hicho kitawasaidia albino kupata huduma muhimu wakiwa kwenye mikono salama. Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam baada ya kumalizika kwa kikao cha ndani cha mabalozi na wawakilishi wa nchi mbalimbali. Waziri Membe amesema kituo hicho kitakuwa na watalaam...
WATU 35 wamefariki dunia na wengine 55 kujeruhiwa baada ya nyumba zao kuwaangukia na kuwafunika usiku wa kuamkia leo kutokana na mvua kubwa iliyonyesha wilayani Kahama, mkoani Shinyanga. Taarifa zilizothibitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya amesema mvua hiyo kubwa iliambatana na upepo mkali, hivyo nyumba nyingi zilianguka na nyingine kuezuliwa na kuharibiwa kabisa. Mpesya amesema mpaka sasa wamefanikiwa kupata miili ya watu 35 waliopoteza maisha baada ya kufukua nyumba nyingi, na majeruhi wamekimbizwa hospitali ya wilaya kwa...
SHIRIKA lisilo la Kiserikali la Save Vulnerable foundation linatarajia kuanzisha mradi utakao wasaidia wananchi wa Mjini na Vijijini wanaoishi katika mazingira magumu,huku waliwalenga Zaidi watu wenye matatizo ya Ulemavu katika suala la Elimu Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam Katibu Mkuu wa Shirika hilo LEONTINE RWECHUNGURA amesema kuwa ripoti ya haki za Binadamu ya mwaka 2010 na Ripoti ya Tanzania ya mwaka 2008 imethibitisha kuwa kiwango cha ...
MENEJA Miradi ya Kinyerezi Mhandisi SIMON JILIMA amesema kuwa mtambo wa Kinyerezi 1 unaojengwa na kampuni ya Yakobsen Elektro ya Norway unatarajia kukamilika mapema Juni mwaka huu. Mhandisi JILIMA ameeleza hayo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini iliyofanya ziara katika Mtambo huo ili kujionea maendeleo ya ujenzi wake. Kamati hiyo imeanza ziara ya kutembelea Miradi ya umeme iliyopo katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Singida, Arusha na Kilimanjaro pamoja na kuzungumza na wadau wa...