Local News

MKURUGENZI MAMLAKA YA BANDARI ASIMAMISHWA KAZI
Local News

KUFUATIA malalamiko ya utendaji mbovu katika kufuata taratibu za uzabuni kutoka kwa wadau mbalimbali wa Maendeleo, Bodi ya dharura ya Mamlaka ya Bandari nchini-TPA imesimamisha kazi Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo MADENI KIPANDE na kumteuwa AWADHI MASSAWE kushika nafasi hiyo hadi uchunguzi rasmi utakapokamilika. Akizungumza na Waandishi wa Habari muda mfupi baada ya kikao cha bodi hiyo Waziri wa Uchukuzi Mheshimiwa SAMWEL SITTA amesema uamuzi huo ni muhimu katika kusaidia kuleta maendelea ya kukua kwa uchumi wa Taifa kupitia...

Like
323
0
Monday, 16 February 2015
NYUMBA MILIONI MOJA KUPATIWA UMEME WA SOLA IFIKAPO MWAKA 2017
Local News

SERIKALI ya Tanzania imesema hadi ifikapo mwaka 2017, itakuwa imetimiza mpango mahususi wa kutumia umeme wa sola uitwao ‘One Solar Homes’ katika nyumba milioni moja. Akizungumza Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini, LUTENGANO MWAKAHESYA, amesema mradi huo unatarajia kutoa huduma ya umeme kwa Asilimia 10 ya watu nchini na ajira 15000 zitakazohusu sola. Amebainisha kuwa mpango huo ni mfano mzuri kwa Mataifa mengine ambayo yana malengo sambamba na mradi wa Power Afrika Initiative uliotangazwa na Rais...

Like
288
0
Monday, 16 February 2015
TANZANIA YAIPONGEZA CHINA KWA KUTOA MISAADA YA KIMAENDELEO
Local News

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatafa BERNARD MEMBE, ameipongeza Serikali Jamhuri ya China kwa msaada wake wa kuhakikisha Tanzania imefungua Idara ya Maalum ya Upasuaji wa moyo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili -MNH. Hayo yamesemwa na Waziri MEMBE katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam kwa niaba ya Rais JAKAYA KIKWETE ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika sherehe ya mwaka mpya wa Kichina. Katika sherehe hizo,Jumuiya ya Wachina waishio nchini Tanzania wameungana pamoja na wageni...

Like
296
0
Monday, 16 February 2015
EWURA KUPUNGUZA GHARAMA ZA UMEME IFIKAPO MACHI MOSI MWAKA HUU
Local News

KUFUATIA agizo lililotolewa na Waziri wa Nishati na Madini hivi karibuni, Mheshimiwa George Simbachawene la kuitaka Mamlaka ya udhibi wa Nishati na Mafuta- EWURA kuangalia uwezekano wa kupunguza gharama za Umeme wa Tanesco, Mamlaka hiyo imetoa tamko la kupunguza gharama za umeme ifikapo Machi mosi mwaka huu. Tamko hilo limetolewa leo jijini Dar es salaam, na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngamlagosi wakati akiongeza na wandishi wa habari ambapo amesema kwa wateja wenye matumizi ya kawaida, bei ya Umeme itashuka...

Like
253
0
Friday, 13 February 2015
JK AZINDUA RASMI SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI 2014
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta, Jakaya Mrisho Kikwete, amezindua rasmi sera ya elimu na Mafunzo ya Ufundi ya mwaka 2014 uliokwenda sambamba uzinduzi wa maabara 3 za Sayansi katika shule ya Sekondari Majani ya Chai iliyopo Kipawa jijini Dar es salaam. Akizungumza katika uzinduzi huo Rais Kikwete amesema Elimu bora ni nyenzo muhimu katika maisha ya kila siku pamoja na kuliletea Taifa maendeleo kwakuwa inamgusa kila mtu bila kujali jinsia. Uzinduzi huo uliofanywa na Rais Kikwete, ni...

Like
410
0
Friday, 13 February 2015
TAMWA: NDOA ZA UMRI MDOGO NI UBAGUZI WA KIJINSIA
Local News

CHAMA cha wanawake wanahabari Tanzania -TAMWA kimesema ndoa za umri mdogo ni aina ya ubaguzi wa kijinsia ambao unawagusa wasichana wadogo na hivyo kupelekea kukatisha masomo yao. Akizungumza na EFM kaimu Mkurugenzi wa TAMWA GLADNESS MUNUO amesema kuwa ubaguzi huo unawafanya wawe waathirika kwa kuambukizwa virusi vya ukimwi kwa urahisi wakilinganishwa na wenzao ambao hawajaolewa. Amesema kuwa ndoa za umri mdogo ni swala la afya pamoja na ukiukwaji wa haki za binadamu lakini wasichana wengi walioolewa kwa umri mdogo wana...

Like
280
0
Friday, 13 February 2015
CHAMA CHA WANANCHI CUF CHASITISHA MAANDAMANO
Local News

CHAMA cha Wananchi CUF, kimetangaza kusitisha Maandamano yaliyokuwa yafanyike leo ambayo yaliandaliwa na Umoja wa Vijana wa chama cha wananchi- Cuf- JUVICUF. JUVICUF iliandaa maandamano hayo kwa lengo la kufikisha ujumbe wao kwa waziri wa mambo ya ndani juu ya vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na jeshi la Polisi pamoja na kuitaka tume ya taifa ya uchaguzi kuongeza siku za uandikishaji wa daftari la kudumu la wapika kura kutoka siku saba za sasa na hadi siku 14....

Like
274
0
Friday, 13 February 2015
WANANCHI WA JIMBO LA MTAMA MKOANI LINDI WAMTIKISA MEMBE
Local News

WANANCHI wa jimbo la Mtama mkoani Lindi wamemtaka mbunge wa jimbo hilo Bernald Membe anayemaliza muda wake kutokujishughulisha kwa namna yoyote kuwatafutia mrithi wa nafasi ya ubunge kwani kwa kufanya hivyo hawata mchagua. Wakizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam wamesema kitendo chochote cha kupingana na chaguo la wananchi kitasababisha Jimbo la Mtama kuwa na wakati mgumu na kwamba wanahitaji mbunge mwenye uchungu na jimbo kwa kuwa jimbo hilo lipo nyuma kwa Nyanja zote za Kielimu, Afya...

Like
382
0
Thursday, 12 February 2015
RAIS KIKWETE AMEWAAPISHA BALOZI MPYA WA TANZANIA NCHINI KENYA NA NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA FEDHA
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano Dokta Jakaya Mrisho Kikwete, amewaapisha Balozi mpya wa Tanzania nchini Kenya na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha. Katika hafla hiyo iliyofanyika leo Ikulu Jijini Dar es salaam, Rais Kikwete amemwapisha Bwana John Haule kuwa balozi mpya wa Tanzania Nchini Kenya na Dokta Hamisi Mwinyimvua ambaye ameapishwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha....

Like
368
0
Thursday, 12 February 2015
WANANCHI WAMETAKIWA KUVITUNZA NA KUVILINDA VYANZO VYA MAJI
Local News

NAIBU Waziri wa Maji, Mheshimiwa AMOS MAKALLA amesema wananchi hawatafaidika na Miradi ya Maji inayotekelezwa na Serikali hivi sasa, kama hawatakuwa makini kuvitunza na kuvilinda vyanzo vya maji. Mheshimiwa MAKALLA amezungumza hayo katika ziara yake Wilaya ya Babati, mkoa wa Manyara wakati akikagua Utekelezaji wa Miradi na kuzindua miradi iliyokamilika katika mkoa huo. Amebainisha kuwa miradi hiyo inagharimu fedha nyingi na Serikali imedhamiria kuwapa wananchi Maji na siyo vinginevyo, lakini bila ushirikiano wao lengo...

Like
235
0
Thursday, 12 February 2015
WASIRA AAGIZA SUKARI IINGIZWE SOKONI
Local News

WAZIRI wa Kilimo, Chakula na Ushirika Mheshimiwa Stephen Wasira, amewaagiza wazalishaji na wafanyabiashara wa sukari nchini, kuingiza Sukari nchini badala ya kuiweka kwenye maghala ili kushusha bei ya bidhaa hiyo muhimu. Agizo hilo la Serikali limekuja ikiwa ni siku chache baada ya kupanda ghafla kwa bei ya sukari kutoka shilingi 1,700 bei ya awali hadi shilingi elfu 3 kwa kilo. Waziri Wasira ametoa kauli hiyo ya Serikali alipokutana na wadau wa Sukari na kutoa tamko la Serikali kuhusu kupanda kwa...

Like
420
0
Thursday, 12 February 2015