Local News

JUMUIYA YA VIJANA CUF IMEMTAKA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI AJIUZULU
Local News

JUMUIYA ya Vijana CUF –JUVICUF imemtaka waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mathias Chikawe kujiuzulu kufuatia tukio la kupigwa na kudhalilishwa kwa mwenyekiti wa chama hicho Profesa Ibrahim Lipumba,viongozi waandamizi na wanachama wake,pamoja na kutoa kauli ya uongo bungeni jana. Akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa JUVICUF Hamidu Bobali amesema kuwa wanasikitishwa na vitendo vilivyofanywa na jeshi la polisi na kulaani ukimya wa viongozi wa juu pamoja na upotoshaji unaofanywa na viongozi hao...

Like
288
0
Friday, 30 January 2015
SERIKALI YAANZA KUPITIA RIPOTI YA WADAU WA ELIMU KUHUSU WANAFUNZI WANAOPATA MIMBA SHULENI
Local News

SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, imeanza kupitia ripoti ya wadau wa Elimu kuhusu tafiti za watoto wanaopata ujauzito wakiwa shuleni ili kuwawezesha watoto hao kupata elimu. Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es salaam na Mratibu wa Elimu Kitengo cha Jinsia kutoka Wizara ya Elimu, Chimpaye Marandu wakati wakijadili ripoti iliyowasilishwa na Taasisi ya Policy Forum kuhusu tatizo la mimba kwa wanafunzi. Marandu amesema kuna idadi kubwa ya watoto wa kike wanaokosa Elimu kwa sababu ya kupata...

Like
340
0
Friday, 30 January 2015
VIJANA ZAIDI YA 70 WANUFAIKA NA MRADI WA KUIJIONGEZEA KIPATO
Local News

VIKUNDI saba vya vijana na wanawake vyenye wanachama 73 wamenufaika kwa kupata mikopo yenye thamani ya shilingi milioni 7 kwa ajili ya kuanzisha biashara na kujikwamua kiuchumi. Hayo yameelezwa na Mkuu wa wilaya ya Iringa, DoktaLeticia Warioba wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema vijana zaidi ya 70 wamepatiwa vifaa na mbegu na wamelima zaidi ya ekari 70 katika kijiji cha Isimani ikiwa ni mradi wa kujiongezea kipato. Amesema vijana hao wamepatiwa mikopo hiyo kwa ajili ya kuanzisha shughuli...

Like
295
0
Friday, 30 January 2015
SERIKALI YAANDAA MPANGO WA KUSHIRIKISHA SHUGHURI ZA KILIMO NA VIWANDA ILI KUONGEZA THAMANI YA MAZAO
Local News

KATIKA kupambana na umasikini nchini Serikali imeaandaa mpango wa kushirikisha shughuli za kilimo na viwanda ili kuongeza thamani ya mazao kwa wakulima yanayouzwa nje ya nchi badala ya kuendelea kuuza mazao ghafi kwa thamani ndogo. Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Waziri wa Kilimo na Chakula STEVEN WASIRA alipozungumza katika Mkutano wa maswala ya Kilimo ulioandaliwa na Shirika la Kilimo la Umoja wa Mataifa-IFAD- ambapo amesema mpango huo utawawezesha wakulima wadogo kuinuka kiuchumi na kuepukana na umasikini unaowasumbua wakulima...

Like
312
0
Friday, 30 January 2015
ESCROW: KUJIUZULU KWA PROF. MUHONGO HAITOSHI
Local News

IMEELEZWA kuwa pamoja na kijiuzulu kwa Profesa Sospeter Muhongo, bado hatua hiyo haitoshi kutatua tatizo la wizi mzito wa fedha za umma kwakuwa wahusika wakuu wa uchotaji wa fedha hizo, bado hawajakamatwa na hata kuhojiwa na hivyo mjadala wa Escrow bado ungali mbichi. Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini wa CHADEMA Arcado Ntagazwa kwenye mkutano na waandishi wa habari uliojadili namna sakata la Tegeta Escrow linavyoendeshwa. Akifafanua hayo Ntagazwa amesema kuwa hatua madhubuti...

Like
245
0
Thursday, 29 January 2015
KITUKO CHA HAKI ZA BINADAMU KIMELAANI KITENDO CHA KUPIGWA KWA MWENYEKITI WA CUF
Local News

KITUO cha sheria na haki za binadamu kimelaani vikali kitendo cha kupigwa kwa Mwenyekiti wa chama cha Wananchi –CUF, Profesa IBRAHIM LIPUMBA na kusema kuwa kitendo hicho ni cha kinyama. Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar e s salaam Mkurugenzi wa Kituo hicho, HELLEN KIJO BISIMBA amesema kuwa kumekuwa na ubaguzi mkubwa hasa katika vyama vya siasa jambo linalopelekea kuvigawa vyama hivyo na kuvikosesha haki yao ya msingi. Aidha amesema kuwa kitendo cha jeshi la polisi kujichukulia sheria mkononi...

Like
221
0
Thursday, 29 January 2015
ACT KIMELITAKA JESHI LA POLISI LITENDE HAKI KWA VYAMA VYOTE VYA SIASA
Local News

CHAMA cha Mabadiliko na Uwazi – ACT kimelitaka jeshi la Polisi litende haki kwa vyama vyote nchini kwa kuacha uwanja huru wa kufanya siasa pamoja na kujenga amani ya kudumu kwa watanzania.   Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho MOHAMMED MASSAGA amesema kitendo kinachofanywa na Jeshi la Polisi kuwanyima Uhuru Wanasiasa kufanya maandamano ni kinyume cha haki ya Mtanzania ambaye anapaza sauti katika kufikisha ujumbe...

Like
269
0
Thursday, 29 January 2015
NAIBU WAZIRI WA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO AMESEMA SERIKALI HAINA NIA YA KUFUNGIA CHOMBO CHOCHOTE CHA HABARI
Local News

SERIKALI kupitia Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe.Juma Nkamia imesema haina nia ya kufungia chombo chochote cha habari, lakini pia imesisitiza kuwa hakuna Uhuru usio na mipaka.   Alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA, katika kipindi cha Maswali na majibu, aliyetaka kujua kwanini Serikali haioni haja ya kulifungulia gazeti la Mwanahalisi ili kutoa uhuru kwa wananchi kupata habari kwa wakati.   Mheshimiwa Nkamia amesema ili kujiepusha na...

Like
233
0
Thursday, 29 January 2015
WANAFUNZI VYUONI WATAKIWA KUJIHESHIMU NA KUJITHAMINI
Local News

WITO umetolewa kwa wananfunzi wa vyuo mbalimbali nchini kujenga tabia ya kujiheshimu na kujitathimini ikiwa ni pamoja na kufuata kile kilichowapeleka chuoni ili kuweza kulinda heshima na utu wa mwanamke Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na aliyekuwa mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es salaam UDSM na mwanaharakati wa kutetea haki za kijinsia HILDA KIWASILI ambapo amesema kuwa wanafunzi wengi hasa wa vyuo vikuu wamekuwa na tabia ya kujiingiza katika makundi ya tamaa na kusahau kinachowapeleka vyuoni jambo...

Like
293
0
Wednesday, 28 January 2015
BUNGE LAAHIRISHWA BAADA BAADA YA JAMES MBATIA KUWASILISHA HOJA YA DHARURA
Local News

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda leo amelazimika kuahirisha kikao cha pili cha Mkutano wa bunge leo asubuhi, baada ya Mbunge wa kuteuliwa kupitia chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia kuwasilisha hoja ya kujadiliwa kwa dharula tukio lililotokea jana Wilayani Temeke Mkoa wa Dar es salaa, lililopelekea kupigwa na kukamatwa kwa Mwenyekiti wa chama cha Wananchi-CUF, Profesa Ibrahim Lipumba pamoja na wafuasi wake.   Katika hoja yake ya msingi, Mheshimiwa Mbatia amesema jambo hilo linaondoa amani,...

Like
252
0
Wednesday, 28 January 2015
PROF: LIPUMBA KUSIMAMA KIZIMBANI
Local News

POLISI Kanda Maalumu ya Dar es salaam, imelazimika kumpeleka Kituo cha afya cha UN, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi –CUF , Profesa Ibrahim Lipumba, baada ya kupatwa na mshituko wa Moyo akiwa katika mahojiano na polisi kuhusiana na maandamano yaliyokuwa yafanywe na chama hicho jana. Kwa mujibu wa Mwandishi wetu anayefuatilia tukio hilo, Hali ya Profesa Lipumba inaendelea vizuri na tayari amefikishwa katika Mahakama ya Kisutu ambako anatarajiwa kusomewa mashitaka yake. Hapo jana Profesa Lipumba pamoja na baadhi ya viongozi...

Like
249
0
Wednesday, 28 January 2015