KAMATI ndogo iliyoundwa na Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro ipo shakani kutekeleza jukumu iliyopewa. Kamati hiyo imeundwa kuchunguza uhalali wa umiliki wa kiwanda kilichoibua mgogoro kati ya madiwani na ofisi ya mkurugenzi wa Halmashauri hiyo. Hatua hiyo inatokana na kuwepo kwa wajumbe ambao ni wakuu wa Idara za Halmashauri hiyo ambao wanaelezwa kuwa hawana uhalali wa kisheria wa kumchunguza mkurugenzi ambaye ni mkuu wao wa kazi....
JESHI la Polisi nchini limeiomba Serikali kuwaongezea vifaa ili kuongeza ufanisi katika kupambana na makundi yanayovuruga amani kwenye uchaguzi mkuu ujao wa Rais, Wabunge na Madiwani. Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini ERNEST MANGU kwenye mkutano wa mwaka wa jeshi hilo uliofanyika mjini Dodoma, kwa kujumuisha maofisa wakuu wa Polisi ili kutathimini utendaji kazi kwa mwaka uliopita na kuangalia mahali walipokosea kwa ajili ya kurekebisha. Amebainisha kuwa hivi sasa wahalifu wamekuwa wakitumia mbinu mpya...
WENYEVITI wa Chama cha Mapinduzi Mikoa, wamekutana Jijini Dar es salaam kwa lengo la kuunga mkono na kupongeza maelekezo ya Kamati Kuu ya Halmashari Kuu ya chama hichoTaifa iliyoyatoa January 13 huko Zanzibar, kwa Serikali katika kutekeleza maazimio ya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu suala la Tegeta Escrow. Akizungumza kwenye Mkutano huo, Mwenyekiti wa Wenyeviti hao wa Mikoa CCM, Bwana Mgana Msindai amesema kuwa wanaipongeza Serikali kwa kutekeleza maelekezo hayo ndani ya wakati na wanashauri kwamba na...
POLISI Mkoa wa Dar es salaam wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi na wafuasi wa chama cha Wananchi-CUF, waliokuwa wamekusanyika kwa maandamano kwa lengo la kukumbuka mauaji yaliyofanyika Januari 26 na 27 mwaka 2001 Zanzibar na Bara kupinga matokeo ya Uchaguzi wa mwaka 2010. Polisi wamemuweka pia chini ya ulinzi mwenyekiti wa Chama cha Wananchi- CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na viongozi wengine wa chama hicho katika kituo cha Polisi Chang’ombe, jijini Dar es salaam. Kwa mujibu wa Taarifa za...
WAZIRI wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa LAZARO NYALANDU amezitaka nchi zinazopakana na Tanzania na zinazoshirikiana katika suala la Utalii kutumia zaidi njia ya Majadiliano kuepuka misuguano isiyo ya lazima Mheshimiwa NYALANDU ametoa rai hiyo katika mkutano wake na Waandishi wa Habari uliofanyika ofisini kwake wakati akizungumzia msuguano uliojitokeza na nchi za Kenya baada ya magari ya Tanzania ya kubeba Watalii kuingia katika Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta. Magari hayo yanayotokea katika jiji la Arusha na Moshi yalizuiwa kuingia nchini...
RAIS wa Zanzibar Dokta ALI MOHAMED SHEIN amesema anafarijika kuona utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa CCM katika kipindi cha miaka Minne ya uongozi wa Serikali yake umekuwa wa mafanikio licha ya kukabiliwa na changamoto kadhaa. Amebainisha kuwa historia ya utekelezaji mzuri wa Ilani ya uchaguzi wa CCM ambayo imezingatia malengo ya Mapinduzi ya mwaka 1964 umeendelea kujenga Imani ya Wananchi kwa Chama. Dokta SHEIN amesema hayo wakati akifungua Kongamano Maalum la Wana-Ccm wa Mikoa ya Pemba na Vijana Wasomi...
WATANZANIA wametakiwa kujiwekeza katika nyumba ili kuondokana na suala la kupanga na kuondokana na msongo wa mawazo juu ya kodi za nyumba kutokana na vipato vya mtu mmojammoja. Rai hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Meneja Mauzo wa kampuni ya Hifadhi Builders inayojishughulisha na ujenzi na uuzaji wa nyumba ambapo sasa wana mradi wa nyumba wa Dege Eco Vilage uliopo Kigamboni, Catherine Mhina alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika sherehe za miaka 57 ya uhuru wa India....
CHAMA cha NCCR-Mageuzi kimemtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano, Jakaya Mrisho Kikwete, kumuwajibisha kwa kumuondoa madarakani Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwakuwa yeye ndiye kiongozi Mkuu wa shughuli za bunge na ndiyo kiongozi wa Mawaziri wanaotuhumiwa kwa uchotaji wa mabilioni ya fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow. Akizungumza na wandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Katibu Mkuu wa chama hicho Mosema Nyambabe, amesema kitendo cha Waziri Mkuu kutojua kwamba kuna bilioni za fedha ya Umma zinachotwa na Mawaziri wake...
Kama ulikosa nafasi ya kusikiliza kipindi cha Mezani kuinachoruka kila siku ya juma mosi kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa nne unaweza kuitazama interview nzima hapa mwendelezo...
MTOTO mwenye umri wa mwezi mmoja amelazwa katika hospital ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma kutokana na kupigwa na Mchi kichwani na Baba yake Mzazi na kusababisha kupasuka fuvu. Kwa mujibu wa Mganga Mkuu wa Hospital ya Wilaya ya Mpwapwa ya Benjamin Mkapa Dokta SAID MAWJI amesema kuwa mtoto huyo amepokelewa na amelazwa Wodi namba saba huku hali yake ikiwa mbaya. Amebainisha kuwa wanaendelea kumfanyia uchunguzi hasa katika fuvu la kichwa ambapo uchunguzi wa awali umeonyesha limepasuka kutokana na kupigwa...
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete leo atawasili Mjini Berlin, Ujerumani ambako akitokea Riyadh, Saudi Arabia, ambako anatarajiwa kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa wa –Gavi Alliance, ambako viongozi mbali mbali duniani watajadili jinsi ya kuboresha mipango ya utoaji chanjo kwa watoto wadogo hasa katika nchi zinazoendelea. Baada ya kumaliza ziara yake Ujerumani, Rais Kikwete atakwenda Ufaransa ambako miongoni mwa mambo mengine atakutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Ufaransa. Aidha, Rais Kikwete atafungua...