IKULU imesema Rais JAKAYA KIKWETE, hajapiga marufuku, wala kupinga au kusema vifaa vya kupigia kura kwa kutumia mfumo wa kisasa wa –BVR-, havifai kwa matumizi. Ikulu imetoa taarifa hiyo, na kufafanua kuwa katika hafla ambayo Rais aliwaandalia Mabalozi wanaowakilisha nchi na Mashirika ya Kimataifa juzi, kuna baadhi ya vyombo vya habari vilipotosha kuhusu suala...
LEO Wazanzibar wanaadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu yaliyofanyika January 12 mwaka 1964. Pamoja na hali hiyo bado Tanzania kama Taifa linaloundwa na Visiwa vya Zanzibar na Tanganyika wana kila sababu ya kujadili hali na mwenendo wa Taifa hili. Katika siku za hivi karibuni wameshuhudia matukio mabaya yanayoashiria uvunjifu wa Amani Visiwani humo na wakati mwingine hata raia wasiokuwa na hatia kupoteza maisha. ...
RAIS WA SHIRIKISHO la Jamhuri ya Ujerumani JOACHIM GAUCK amelaani shambulio la kigaidi la Paris na kulitaja kuwa ni shambulio dhidi ya uhuru. Rais GAUCK amesema Demokrasia imezidi kupata nguvu kuushinda ugaidi kabla ya mapokezi ya mwaka mpya ya mabalozi wa nchi za nje katika kasri lake mjini Berlin. Rais JOACHIM GAUCK ameendelea kusema kuwa hawataachia chuki...
Wajumbe wa kamati ya ufundi ya bodi ya maji Safi na Maji Taka Dar es salaam-DAWASA wamefanya ziara ya siku moja katika mikoa ya Dar es salaam na Pwani kukagua na kujionea hatua iliyofikiwa katika mradi wa ujenzi wa Miundombinu ya maji kutoka Ruvu Chini na Ruvu Juu ili kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji kwa wananchi katika mikoa hiyo. Ziara ya wajumbe hao wa kamati ya Ufundi imeanza kwa kukagua kazi ya ukarabati wa kituo yalipo matangi ya maji...
KAMATI KUU ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi -CCM inataraji kukutana Zanzibar Januari 13,mwaka huukatika kikao cha kawaida cha siku moja chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais JAKAYA KIKWETE. Kikao cha Kamati Kuu kitatanguliwa na Kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu kitakachofanyika Januari 10, jijini Dar es...
POLISI WA UWANJA wa Ndege wa Kimataifa wa Julias Nyerere-JNIA wamefanikiwa kumkamata Raia wa Kuwait,HASSAIN AHMED ALLY kwa tuhuma za kukutwa na Viumbe aina ya Kenge 149 wenye thamani ya Shilingi Milioni 6 nukta kinyume cha sheria . Kamanda wa Polisi wa Uwanjani hapo HAMISI SELEMAN amesema kuwan raia huyo amekamatwa na Kenge hao ambao amewaweka katika mifuko midogo midogo iliyokuwa kwenye begi lake kubwa. Amesema kuwa tukio hilo limetokea wakati HASSAN akijiandaa na safari ya kuelekea nchini Kuwait kupitia Dubai...
WATANZANIA wametakiwa kuwa na moyo wa kushirikiana ili wananchi wenye kipato cha chini waweze kupata mahitaji muhimu ya Binadamu ikiwa ni pamoja na Makazi salama. Wito huo umetolewa jijini Dar es salaam na Meneja Mtendaji Mkuu wa Chama Cha ushirika cha ujenzi wa Nyumba chenye makao makuu yake Mwenge jijini Dar es salaam THOMAS MOSHA alipozungumza na Waandishi wa Habari katika hafla ya kuwaapisha viongozi wapya wa Bodi ya chama hicho. Ameeleza kuwa kitendo cha kusaidia wananchi wa kipato cha...
MENEJA utaalamu Elekezi kutoka Wakala wa Nishati Vijijini -REA GISSIMA NYAMOHANGA amesema serikali imetumia Shilingi Bilioni 881 katika mradi wa kusambaza umeme vijijini unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini –REA Awamu ya Pili. NYAMOHANGA ameeleza hayo kwenye sherehe za Uzinduzi wa Mradi wa Umeme Vijijini unaofadhiliwa na REA uliofanyika katika Kata ya Shishiyu wilayani Maswa mkoani...
WANAFUNZI 10 kutoka vyuo Vikuu vya Bufalo na Empire vya Marekani wamewasili nchini kwa ziara ya mafunzo kwa mwaliko wa Mbunge wa Jimbo la Temeke, Mheshimiwa ABBAS MTEMVU. Akizungumza na Waandishi wa habari Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam mara baada ya kuwapokea Wanafunzi hao ambao wanaongozwa na Profesa DAN NYARONGA, Mbunge wa Temeke ABBAS MTEMVU amesema wageni hao watapata fursa ya kutembelea miradi mbalimbali iliyopo katika Jimbo lake pamoja na Kampuni yake ya Bravo...
WATU kadhaa wamenusulika kifo kutokana na ajali ya daladala lenye lenye namba za usajili T 702 AJG inayofanya safari kutoka Temeke kwenda Kawe iliyotokea mapema Asubuhi hii karibu na eneo la mzunguko wa barabara ya zamani ya Bagamoyo jijini Dar es salaam. Akizungumza muda mfupi mara baada ya kutokea kwa ajali hiyo SAJENT ERNEST kutoka kikosi cha usalama Barabarani Kawe amesema kuwa ajali hiyo kwa kiasi kikubwa imesababishwa na uzembe wa dereva kwa kuwa hakuwa makini wakati akipishana na gari...
WAZIRI WA NCHI ofisi ya Rais Kazi Maalum,Profesa MARK MWANDYOSA amesema kuna umuhimu wa kuwa na Maktaba za marais wastaafu ili kuwa na hazina kwa taifa. Profesa MWANDYOSA ameeleza kuwa kinachowatenganisha Waafrika na nchi zilizoendelea ni lugha ya Maandishi ambayo ni urithi kwa vizazi vijavyo kwa kutunza kumbukumbu za hekima,busara na harakati za ukombozi na mchango wa viongozi...