SERIKALI imeombwa kuhakikisha inakomesha ubabe unaotumika kukeketa mabinti wa koo za Kikuria nchini. Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Kituo cha kupambana na Ukeketaji cha Masanga, Tarime Sista GERMAINE BAIBIKA wakati akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kukamilika kwa Sherehe ya Mahafali ya Sita ya Mabinti waliokwepeshwa Msimu wa Ukeketaji....
NAIBU WAZIRI wa Fedha Mheshimiwa MWIGULU NCHEMBA amefanya ziara kwenye Hospitali ya Mwananyamala kujionea hali halisi ya huduma zinazopatikana katika Hospitali hiyo pamoja na kuchangia damu salama ili kuhamasisha Kampeni ya kuchangia Damu Salama kwa Wagonjwa wanaohitaji Damu. Ziara hiyo ameifanya katika kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa,ambayo imelenga kutoa huduma za Kijamii kwa kuwasaidia watu Wasiojiweza, Wagonjwa pamoja na watu wenye Shida...
KATIBU MKUU wa AMINA CHIFUPA Foundation, HAMIS CHIFUPA amempongeza Rais JAKAYA KIKWETE kwa kurejesha kwa Wananchi kiwanda cha Chai Cha Mponde kilichopo Lushoto mkoani Tanga. Mzee CHIFUPA amechukua hatua hiyo kutokana na dalili njema aliyoionyesha Rais KIKWETE ya kurejesha rasilimali za Wananchi mikononi mwao ili kuwakomboa...
SERIKALI mkoani Mwanza imesema hakuna kulala hadi mtoto mwenye Ulemavu wa Ngozi PENDO EMMANUEL apatikane baada ya kutekwa na watu wasiojulikana. Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza MAGESA MULONGO alipokuwa akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Ndami Wilayani Kwimba katika Mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini...
KAMATI YA BUNGE ya Hesababu za Serikali za Mitaa-LAAC imeitaka Manispaa ya Temeke kuongeza makusanyo hadi kufikia Shilingi Bilioni 35. Akizungumza katika ziara ya Kamati hiyo jijini Dar es salaam,Mwenyekiti wa LAAC Mheshimiwa RAJAB MOHAMED amesema Manispaa hiyo ina uwezo wa kuiongezea Serikali mapato endapo itatumia vizuri rasilimali...
KAMANDA wa Kikosi cha Usalama Barabarani MOHAMED MPINGA ametoa onyo kwa baadhi ya Wamiliki wa Mitandao ya Kijamii kuacha tabia ya kusambaza taarifa ambazo hazijafanyiwa uchunguzi na kuthibitika kama zina ukweli ndani yake. Kamanda MPINGA ameeleza hayo wakati akiongea na Waandishi wa Habari kuhusu tukio la baadhi ya Mitandao kusambaza taarifa kuwa Basi la Dar Express limepata ajali hivyo kuleta taharuki kwa ndugu na...
ifikapo mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu Mradi wa Usambazaji wa Umeme Vijijini unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini -REA Awamu ya Pili kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Nchini -Tanesco unatarajiwa kukamilika, ikiwa ni pamoja na kuvipatia umeme Vijiji 1,500. Hayo yameelezwa na Waziri wa Nishati na Madini Profesa SOSPETER MUHONGO kwa nyakati tofauti alipofanya ziara katika vijiji vya Ihale, Bukombe, Nyamikoma, Bushigwamala, Mwamagigisi, Mkula vilivyopo katika Wilaya ya Busega mkoani Simiyu. Profesa MUHONGO amefanya ziara katika...
WANANCHI wenye hasira wamechoma moto nyumba tano za mtu anayedaiwa kuwa jambazi sugu katika eneo la Ugurubi wilayani igunga. Hatua hiyo imesababisha jeshi la Polisi Wilani humo kutumia risasi na mabomu ya machozi kudhiti tukio hilo. Kutokana na tukio hilo baadhi ya wananchi wamekimbia makazi yao wakiwakwepa polisi kuwakamata baada ya kutuhumiwa kuchoma nyumba za mtu huyo MAHONA...
MKUU WA KITENGO wa Cha kupambana na dawa za Kulevya nchini Kamanda GODFREY NZOWA amesema kuwa mtu yoyote atakayekamatwa na Dawa za Kulevya mali zake zitabinafsishwa. Akizungumza na EFM kuhusiana na mapambano dhidi ya Dawa za kulevya, Kamanda NZOWA ameeleza kuwa vita hiyo inaendelea hadi kuhakikisha kuwa matumizi ya Dawa hizo hapa nchini...
JAMII IMESHAURIWA kuwa na utaratibu wa kwenda kuwatembelea watoto Yatima na waishio katika Mazingira hatarishi ili kusaidia matatizo mbalimbali wanayakabiliana nayo Wito huo umetolewa na Mjasiriamali wa kujitegemea AGUSTA MASAKI alipokuwa akitoa msaada wa vitu mbalimbali katika kituo cha kulelea watoto waishio katika mazingira magumu Cha Diana Centre kilichopo Gongo la...
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema kwamba itaendelea kuruhusu kuanzishwa kwa Radio za Jamii kutokana na umuhimu wake katika kuhimiza maendeleo na kutumika kama daraja kati ya wananchi na serikali yao. Hayo yamesemwa na Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa jamii, Vijana, Wanawake na Watoto, ZAINAB OMAR MOHAMMED wakati akizundua kituo cha Radio ya Jamii Jimbo la Mkanyageni, Mkoani...