Local News

Afrika yaongoza kwa rasilimali ya maji baridi
Local News

Zaidi ya asilimia 30 ya maji baridi Duniani yapo katika ukanda wa Afrika, hayo yamebainishwa na Meneja wa mamlaka ya udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) kanda ya kati, Mhandisi Norbet kayonza katika semina ya siku moja ya wakandarasi wa umeme wa manispaa ya singida. Mhandisi Kayonza ametahadharisha kuwa licha ya mahitaji ya maji kuongezeka lakini vyanzo vya maji vinapungua kwani idadi ya watumiaji inaongezeka siku hadi siku, nakusisitiza “rasilimali ya maji duniani inapungua huo ni ukweli ambao haupingiki, lakini...

Like
684
0
Thursday, 13 December 2018
Umoja wa wabangua Korosho wampongeza JPM
Local News

Uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, kununua korosho za wakulima na kuzibangua nchini umepongezwa na Umoja wa Wabanguaji Wadogo wa Korosho Tanzania (UWWKT). Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa umoja huo, Tumpale Magehema ambapo amesema kuwa uamuzi wa Rais Magufuli una nia ya kuwapa ajira wanachama wake wapatao 2881, jambo ambalo ni la kupongezwa. Amesema kuwa uamuzi huo wa kijasiri uliofanywa na Rais Magufuli utaongeza ari ya kufanya kazi na kuchochea ukuaji wa...

Like
766
0
Thursday, 13 December 2018
Vigogo watano wa WETCU watupwa jela
Local News

Vigogo watano wa Chama Kikuu cha Wakulima wa Tumbaku Kanda ya Magharibi (WETCU), wamehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka minne kila mmoja, baada ya kutiwa hatiani kwa makosa mawili likiwemo la kukisababishia chama hicho hasara ya zaidi sh. milioni 109. Vigogo hao ambao walitiwa hatiani na Mahakama ya Wilaya ya Tabora, mbele ya Hakimu Mkazi, Tengwa Chiganga na kupewa adhabu hiyo, watatumikia kifungo cha miaka miwili gerezani kutokana na adhabu za kifungo. Waliotiwa hatiani na kupewa adhabu hiyo ni  pamoja na aliyekuwa...

Like
608
0
Wednesday, 12 December 2018
BANDARI TANGA KUHUDUMIA SHEHENA YA NCHI SABA KWA KUTUMIA MPAKA MMOJA
Local News

Bandari ya Tanga inaelezwa kuwa bandari ya kipekee na ya aina yake barani Afrika inayoweza kuhudumia nchi saba kwa kutumia mpaka mmoja. Hayo yameelezwa na Meneja wa bandari hiyo, Percival Salama, ofisini kwake jijini Tanga wakati akizungunza na waandishi wa habari kuhusu maboresho mbalimbali yaliyofanyika katika kuhakikisha wanaongeza ufanisi wa bandari hiyo. Amesema mbali na kuwa na uwezo wa kuhudumia nchi saba bandari ya Tanga kijografia ina sifa ya kuwa bandari pekee ya asili kutokana na kuwa na kina cha...

Like
1178
0
Wednesday, 12 December 2018
Uwekezaji katika sekta ya madini waongezeka
Local News

Waziri wa Madini, Angela Kairuki amesema kuwa uwekezaji katika sekta ya madini umeongezeka, hasa kwa wawekezaji wa nje kutoka katika kipindi cha miaka miwili iliyopita tangu sheria ya madini ya mwaka 2010 ifanyiwe marekebisho na kuanza kutumika mwaka 2017. Akizungumza mara baada ya kongamano la uwekezaji katika sekta ya madini kati ya Tanzania na China lililofanyika Beijing nchini China Jumatatu wiki hii, Kairuki alisema kasi ya uwekezaji katika sekta ya madini imeendelea kuongezeka baada ya kufanya marekebisho hayo ya sheria...

Like
585
0
Tuesday, 11 December 2018
Mafuriko ya wasafiri, Wamiliki wa Mabasi waililia Serikali
Local News

Kutokana na idadi kubwa ya abiria waliofurika katika vituo vya mabasi yaendayo mikoani kwa lengo la kusafiri katika msimu huu wa sikukuu za Christmas na Mwaka Mpya, wamiliki wa mabasi wameiomba Serikali kuzingatia ushauri wao ili kumudu hali iliyopo. Katibu Mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi (TABOA), Enea Mrutu ameiomba Serikali kuruhusu mabasi ya abiria kusafiri usiku na mchana. Ameiomba Serikali kuongeza ulinzi kwa mabasi yanayotoka Dar es Salaam ili yasilale Shinyanga na badala yake yaruhusiwe kuingia Mwanza. Kadhalika,...

Like
1167
0
Tuesday, 11 December 2018
William Ole toa neno Simanjiro, asisitiza ushirikiano
Local News

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha ameitaka Serikali ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara kuhakikisha inahusisha Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA katika ujenzi wa Chuo cha VETA Simanjiro ili miundombinu ya chuo hicho iweze kujengwa kwa utaratibu na viwango vinavyohitajika. Ametoa agizo hilo Mkoani Manyara wakati akikagua eneo ambalo Serikali ya Wilaya hiyo inategemea kujenga Chuo cha Veta kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Hiari ECLAT. Amesema kuwa ni vizuri Mamlaka...

Like
881
0
Tuesday, 11 December 2018
Biashara ya kubadili fedha za kigeni kudhibitiwa
Local News

Mamlaka nchini zimeazimia kuendeleza kampeni ya kudhibiti biashara ya maduka ya kubadilisha fedha za kigeni nchini ili “kuzuia kuyumba kwa sekta ya fedha”. Mwezi uliopita, Benki kuu (BoT) iliyafunga zaidi ya maduka 100 ya kubadili fedha jijini Arusha kwa kutokukidhi masharti ikiwemo kutokuwa na leseni halali za biashara. Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Gavana wa BoT Profesa Florens Luoga amesema operesheni hiyo haitakoma, na huenda mji mkuu wa kibiashara Dar es Salaam ukafuata baada ya Arusha. “Hatuhitaji maduka 100...

Like
1670
0
Monday, 10 December 2018
Serikali yalipa zaidi ya shil. bilioni 83 kwa wakulima wa Korosho
Local News

Serikali imesema kuwa mpaka sasa imelipa zaidi ya shilingi bilioni 83 kwa wakulima wa Korosho katika mikoa ya Lindi, Mtwara, pamoja na Ruvuma huku zaidi ya wakulima 82,835 kutoka mikoa hiyo wakiwa wamepatiwa fedha zao. Hayo yamesemwa na Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga ambapo amesema kuwa Jumla ya fedha iliyolipwa kwa wakulima hao ambao tayari wamefanyiwa uhakiki katika Mkoa wa Mtwara pekee ni 50,835, Lindi wakulima 22,131 na Mkoa wa Ruvuma ambao takribani wakulima 9,445 wamelipwa. Ameyasema hayo wakati akizungumza...

Like
912
0
Monday, 10 December 2018
MKURUGENZI WA BOT TAWI LA DODOMA AFUNGUA SEMINA YA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU MASUALA YA UCHUMI NA FEDHA JIJINI DODOMA
Local News

Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania tawi la Dodoma Bw. Richard Wambali aliyemwakilisha Dkt. Yamungu Kayandabila  Naibu Gavana anayeshughulikia Uchumi na Fedha akifungua  semina ya siku tano ya  waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali kuhusu masuala ya uchumi na fedha inayofanyika kwenye ukumbi wa (BOT) jijini Dodoma. Katika semina hiyo wanahabari watapata ufafanuzi wa masuala  yanayoshughulikiwa  na benki hiyo pamoja na  mabenki ya biashara ya kifedha nchini Tanzania kwa kufuata sheria kanuni na taratibu zinazosimamiwa na Benki Kuu...

Like
1190
0
Monday, 10 December 2018
Benki ya Dunia kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya miradi ya Tanzania
Local News

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akutana na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kanda ya Afrika Dkt. Hafez Ghanem ambaye ametangaza kuwa Benki ya Dunia imeridhia kutoa Dola za Marekani milioni 300 kwa ajili ya mradi wa kuongeza ubora wa elimu ya Sekondari. Katika Mazungumzo hayo: Benki ya Dunia imeridhia kutoa Dola za Marekani Milioni 300 sawa na shilingi Bilioni 680.5 kwa Tanzania kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa kuongeza ubora wa elimu ya sekondari unaokusudiwa kujenga vyumba...

Like
695
0
Friday, 16 November 2018