Local News

UTURUKI KUWAALIKA WAWEKEZAJI KATIKA HIFADHI ZA TAIFA NCHINI
Local News

SERIKALI ya Uturuki imesema itawaalika wawekezaji kutoka nchini humo ili waweze kutumia nafasi za uwekezaji zilizopo katika Hifadhi za Taifa nchini. Kauli hiyo imetolewa na balozi wa Uturuki nchini, Yasemine Eralp alipotembelea Makao Makuu ya TANAPA jijini Arusha na kukutana na viongozi wa shirika. Balozi Eralp amesema kuwa sekta ya utalii ni miongoni mwa vipaumbele vyake na kwamba atatumia muda wake mwingi kuhakikisha kuwa sekta hiyo inastawi na kuvutia watalii wengi nchini kutoka Uturuki huku  akitoa nafasi kwa TANAPA kujitangaza...

Like
252
0
Thursday, 17 September 2015
MANYARA: MKUU WA KITENGO CHA MANUNUZI TANROADS AHUKUMIWA MIAKA 3 JELA KWA KUOMBA RUSHWA
Local News

MKUU wa kitengo cha manunuzi kutoka  wakala wa barabara nchini (Tanroads) Mkoani Manyara, Raphael Chasama amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu au kulipa faini ya shilingi milioni1 kwa kosa la kuomba rushwa ya shilingi 7.4. Hakimu mfawidhi wa mahakama ya Wilaya ya Babati, Bernadeta Maziku akisoma hukumu Mahakamani hapo amesema  Disemba 22 mwaka 2009, bwana Chasama alishawishi kupewa rushwa kinyume na sheria ya kuzuia na kupambana na...

Like
425
0
Thursday, 17 September 2015
WANANCHI WANUFAIKA NA MRADI WA MASHINE YA KUKAMULIA ALIZETI BABATI
Local News

WANANCHI wa Kijiji cha Endanoga Wilayani Babati Mkoani Manyara, imeelezwa kuwa wamenufaika na mradi wa mashine ya kukamulia alizeti wenye thamani ya shilingi  milioni 205  uliodhaminiwa  kwa ushirikiano wa  Serikali na wananchi. Mkuu wa wilaya ya Babati Crispin Meela ameitaka jamii ya eneo hilo kuutunza mradi huo uliofadhiliwa na Wizara ya kilimo, chakula na ushirika iliyotoa shilingi milioni 197.9, Halmashauri ya mji shilingi milioni 3.2  na jamii shilingi milioni 7.9. Meela amesema mashine hiyo itatumika kuongeza uchumi wa jamii...

Like
365
0
Wednesday, 16 September 2015
DK SHEIN: NIMETEKELEZA ILANI YA UCHAGUZI YA CCM KWA VITENDO
Local News

MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein  amesema kuwa katika uongozi wake ametekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM kwa vitendo huku pia, akitekeleza vizuri uongozi wake katika Serikali yenye muundo wa Umoja wa Kitaifa kwa amani na utulivu.   Dk. Shein ambaye ni Mgombea nafasi ya Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM aliyasema hayo katika hotuba yake aliyoitoa kwenye mkutano wa Kampeni wa chama hicho...

Like
229
0
Wednesday, 16 September 2015
JK AWAAPISHA WENGINE IKULU LEO
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo amewaapisha bwana Casmir Kyuki kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria, na Bibi Sarah Barahomoka kuwa Mwandishi Mkuu wa Sheria. Kabla ya uteuzi huu, bwana Kyuki alikuwa Mwandishi Mkuu wa Sheria na Barahomoka alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya uandishi wa Sheria. Uteuzi huo umefanyika jana na umeanza mara...

Like
309
0
Wednesday, 16 September 2015
WANAFUNZI NCHINI WAMETAKIWA KUWEKEZA KATIKA ELIMU
Local News

WANAFUNZI kote nchini wametakiwa kuwekeza katika elimu, pamoja na kufanya kazi kwa juhudi ili wanufaike katika maisha yao ya sasa na baadae sanjari na kuliletea Taifa maendeleo.   Hayo yamesemwa na Mkuu wa utawala na uongozi wa chuo cha Habari maalum Ernest Karata wakati wa mahafali ya kwanza ya chuo cha Full Bright college kilichopo Ngaramtoni wilaya ya Arumeru mkoani Arusha. Akizungumza katika mahafali hayo mkurugenzi mtendaji  wa chuo hicho Julius Matiko amewaasa wahitimu kutumia elimu waliyoipata katika kuhakikisha wanatimiza...

Like
193
0
Tuesday, 15 September 2015
SAMIA SULUHU AAHIDI KUSIMAMIA RASILIMALI ZA TAIFA IWAPO CCM ITAPEWA RIDHAA
Local News

MGOMBEA mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi-CCM-Samia Suluhu Hassan amesema kuwa endapo wananchi watakipa ridhaa chama hicho kuwaongoza kwa awamu nyingine atahakikisha anasimamia vyema rasilimali za Taifa. Samia ameyasema hayo wilayani Mkuranga, Kimanzichana wakati akizungumza na wananchi ikiwa ni moja ya ziara zake za kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Aidha Samia amewahakikishia watanzania kuwa serikali ya awamu ya tano ya –CCM- itaweka mikakati madhubuti ya kupambana na tatizo la rushwa...

Like
163
0
Tuesday, 15 September 2015
VIJANA WAMETAKIWA KUTOTEGEMEA KUAJIRIWA
Local News

VIJANA nchini wametakiwa kutumia vizuri mazingira yanayowazunguka katika kuibua mbinu mbalimbali za ujasiriamali ili kuweza kuondoka na Taifa tegemezi kwa kusubiri kuajiriwa mara baada ya kuhitimu masomo yao. Rai hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Susan Ndunguru alipokuwa akifunga mafunzo ya Wawezeshaji wa Kitaifa wa Stadi za Maisha yaliyofanyika Jijini Mwanza. Ndunguru amesema kuwa vijana waliopata mafunzo ya uwezeshaji wa stadi za maisha ni mabalozi ambao wana uwezo mkubwa wa kuweza kujenga Taifa lenye Afya nzuri, weledi...

Like
196
0
Tuesday, 15 September 2015
RAIS KIKWETE AMTEUA VICTORIA RICHARD MWAKASEGE KUWA BALOZI WA TANZANIA NCHINI MALAWI
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Victoria Richard Mwakasege kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi ambaye kabla ya uteuzi wake alikuwa Naibu Balozi wa Tanzania nchini Burundi. Aidha, Rais Kikwete amemteua Msaidizi wa Rais wa Diplomasia, Balozi Samwel Shelukindo kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue imeeleza kuwa Rais Kikwete amemteua Zuhura Bundala kuwa Balozi na...

Like
478
0
Tuesday, 15 September 2015
TFDA YAKAMATA  DAWA NA VIPODOZI HARAMU VYENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 135
Local News

MAMLAKA ya Chakula na Dawa Tanzania TFDA imefanikiwa kukamata dawa na vipodozi haramu vyenye thamani zaidi ya shilingi milioni 135, katika maeneo 243 kwenye Mikoa nane ya Tanzania Bara wakati wa Operesheni ya pili ya Giboia (Operesheni chatu) iliyofanyika kuanzia tarehe 19 hadi 21 Agosti Mwaka huu. Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Bwana Hiiti Sillo amesema baada ya uchambuzi na uchunguzi wa makosa kukamilika hatua mbalimbali zitachukuliwa pamoja na kuwapeleka Watuhumiwa mahakamani na kutoa adhabu kulingana na sheria ya chakula, Dawa...

Like
231
0
Monday, 14 September 2015
JUKWAA LA WAHARIRI LAWATAKA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA NA MASHABIKI KUACHA KUSHAMBULIA WAANDISHI
Local News

IKIWA Zimepita siku tatu tangu kupigwa kwa Mwandishi wa habari wa magazeti ya Uhuru publications Limited UPL, CHRISTOPHER LISSA Katika ofisi za chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Jukwaa la Wahariri Tanzania limewataka viongozi wa vyama vya siasa pamoja na mashabiki wa vyama hivyo kuacha vitendo vya kuwashambuliwa waandishi wa habari na kwamba vitendo hivi vikiendelea jukwaa litachukua hatua za kisheria dhidi ya vyama husika. Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Jukwaa hilo ABSALOM KIBANDA  amesema kuwa Jukwaa wamesikitishwa...

Like
313
0
Monday, 14 September 2015