Local News

RAIS KIKWETE AANZA ZIARA NCHINI KENYA
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, ameanza ziara rasmi ya Kiserikali ya siku tatu katika Jamhuri ya Kenya kwa mwaliko wa Rais wa nchi hiyo, Mheshimiwa Uhuru Muigai Kenyatta ambako miongoni mwa shughuli atakazozifanya ni pamoja na kulihutubia Bunge la Kenya.   Rais Kikwete ameanza ziara yake jana kwa kuungana na Rais Kenyatta kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Barabara ya Taveta-Mwatate ambayo ni sehemu ya barabara inayounganisha Tanzania na Kenya ikianzia Arusha-Holili-Taveta-Mwatate.  ...

Like
689
0
Monday, 05 October 2015
121 MBARONI KWA MAKOSA YA KIHALIFU
Local News

JESHI la polisi nchini kwa kushirikiana na ofisi za interpol kanda ya kusini mwa afrika limefanikiwa kukamata jumla ya watuhumiwa 121 kwa makosa mbalimbali ya kihalifu baada ya kufanya operesheni ya pamoja kutokana na maamuzi yaliyoafikiwa kwenye mikutano ya wakuu wa majeshi wa nchi za kusini mwa Africa-SARPCCO. Akizungumza leo jijini dar es salaam, Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai CP Diwani Athumani amesema kuwa watuhumiwa wamekutwa na vielelezo vya uhalifu zikiwemo nyara za serikali, dawa za kulevya ,...

Like
213
0
Thursday, 01 October 2015
WAZEE WAIOMBA SERIKALI IJAYO KUZINGATIA MAHITAJI MUHIMU
Local News

KATIKA kuadhimisha siku ya wazee dunia leo, baadhi ya wazee waishio jijini dar es Salaam wameiomba serikali ijayo kuhakikisha inazingatia mahitaji muhimu ya wazee nchini ikiwa ni pamoja na kutekeleza ahadi ya huduma bure za matibabu. Wakizungumza na kituo hiki wazee hao wameeleza kuwa ahadi ya huduma bure za afya haijaweza kutekelezeka kwani wazee wengi wakienda kupata matibabu katika hospitali za serikali wanatibiwa magonjwa madogomadogo na yale yanayohitaji vipimo vikubwa na dawa wanatakiwa kujihudumia...

Like
196
0
Thursday, 01 October 2015
MAMA ALIYETELEKEZWA AANZA KUPATIWA MISAADA
Local News

September 30 kwenye kipindi cha Ubaoni ilitoka ripoti ya mama mwenye watoto wanne akieleza jinsi alivyotelekezwa na mume wake na kupelekea yeye na watoto wake kukosa huduma muhimu za kimaisha. Mama huyo aliyejitambulisha kwa jina la Frola Frank alitoa rai yake kwa watanzania wenye nia ya kumsaidia wajitokeze ili waweze kutoa misaada tofauti . Moja ya watanzania ambae Hakutaka jina lake litwaje ni miongoni mwa watu walioguswa na mapito ya maisha ya mama huyu amejitolea kiasi cha shilingi laki nne...

Like
327
0
Thursday, 01 October 2015
BEI YA MAZAO YA NAFAKA YAPANDA DAR
Local News

IMEELEZWA kuwa bei ya mazao ya nafaka kwasasa imepanda katika masoko mbalimbali Jijini Dar es salaam kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa yanayopelekea mavuno yasiyo tarajiwa kwa wakulima shambani. Wakizungumza na efm wafanyabiashara wanao uza mazao hayo katika soko la Tandika wamesema kuwa upandaji huo unasababishwa na aina ya kilimo kilichopo cha kutegemea nvua na siyo...

Like
418
0
Thursday, 01 October 2015
KITUO CHA MICHEZO CHA JMK KUZINDULIWA RASMI OKTOBA 17 NA RAIS KIKWETE
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Oktoba 17, mwaka huu atazindua rasmi Kituo cha Michezo cha Kisasa cha Jakaya M. Kikwete Youth Park (JMK Park), Kidongo Chekundu, Dar es Salaam, kikiwa ni kituo cha kwanza cha aina yake nchini chenye kulenga miongoni mwa mambo mengi kuanza kulea wanamichezo tokea wakiwa wadogo.   Rais Kikwete alikubali kuzindua Kituo hicho wakati wa mazungumzo kati yake na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Umeme ya Symbion Power, Bwana Paul...

Like
206
0
Thursday, 01 October 2015
WANASIASA WAMETAKIWA KUACHA KUPIGANA VIJEMBE NA MATUSI
Local News

ZIKIWA zimebaki siku 24 kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani, baadhi ya Wananchi wamewataka wanasiasa kuacha kampeni za kupigana vijembe na matusi bali wafanye kampeni za kistaarabu. Wakizungumza na EFM kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema wanahitaji kusikia sera za vyama kupitia ilani za vyama hivyo na sio kufanya kampeni za kutupiana maneno na matusi jukwaani kwa kuwa wanasiasa wote lengo lao ni kujenga nyumba moja ambayo ni Tanzania ya awamu ya...

Like
251
0
Wednesday, 30 September 2015
RAIS KIKWETE AKUBALI KUJIUNGA NA KUNDI LA WATU MASHUHURI DUNIANI KWENYE MAPAMBANO DHIDI YA MALARIA
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta Jakaya Mrisho Kikwete ameombwa na amekubali kujiunga na kundi la watu mashuhuri duniani wakiwemo viongozi wa Afrika, matajiri wa Marekani na watu wengine mashuhuri katika kutafuta majawabu ya kumaliza ugonjwa wa malaria duniani kwa kuanzia na Bara la Afrika.   Ombi hilo kwa Rais Kikwete kujiunga na kundi hilo ambalo litaongozwa na tajiri mkubwa zaidi duniani, Bwana Bill Gates, liliwasilishwa kwa mara ya kwanza kwake wiki iliyopita na Mjumbe Maalum wa Umoja...

Like
247
0
Wednesday, 30 September 2015
ELIMU ZAIDI YAHITAJIKA JUU YA YUGONJWA WA KIPINDUPINDU
Local News

IMEELEZWA kuwa inahitajika elimu ya kutosha kwa wananchi juu ya suala zima la ugonjwa wa kipindu pindu na umuhimu uliopo kwa watanzania wote kudumisha hali ya usafi na kujiepusha na mambo yoyote ambayo yatapelekea kwa namna moja ama nyingine ongezeko la maambukizi ya ugonjwa huo.   Akizungumza na Waandishi wa habari Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni MUSSA NATTY Amesema kuwa suala zima la kudhibiti ugonjwa wa kipindu pindu jijini linashindikana kutokana na watanzania wengi kutozingatia mambo muhimu ambayo  yameelekezwa na...

Like
267
0
Wednesday, 30 September 2015
RAIS KIKWETE ATOA CHANGAMOTO KWA BUNGE LA MAREKANI KUFUNGA MASOKO YA PEMBE ZA NDOVU NA FARU DUNIANI
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametoa changamoto kwa Wabunge wa Bunge la Marekani kufunga masoko ya pembe za ndovu na faru duniani, kama njia yenye uhakika ya kukomesha ujangili dhidi ya wanyamapori katika nchi za Afrika na kwa haraka zaidi.   Aidha, Rais Kikwete amewataka Wabunge hao kuzisaidia nchi za Afrika kifedha, ili kukomesha ujangili huo kwa sababu Wabunge hao tayari wameitangazia dunia kuwa wanazo fedha za kutosha kwa ajili ya kukabiliana na majanga...

Like
225
0
Wednesday, 30 September 2015
ZANZIBAR: BODI YA CHAKULA, DAWA NA VIPODOZI YAANDAAMIONGOZO YA UTOAJI HUDUMA BORA
Local News

BODI ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDB) imesema kuwa imeandaa miongozo ya utoaji huduma bora katika kufanikisha  Mpango wa uwiano wa Itifaki ya pamoja kwa Nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki.   Mkurugenzi wa ZFDB  Dokta Burhani Othman Simai ameeleza hayo katika Mkutano wa wadau wa dawa Zanzibar ulioandaliwa na Mpango wa Udhibiti wa bidhaa za Chakula na Dawa wa Jumuia ya Afrika Mashariki.   Katika mkutano huo dokta Simai amesema kuwa kuanzia sasa bidhaa zote za chakula...

Like
238
0
Tuesday, 29 September 2015