kupitia joto la asubuhi waweza kuwa mshindi pia, njia ni rahisi zaidi unachotakiwa kufanya ni kusikiliza kipindi cha Joto la asubuhi jumatatu hadi ijumaa Picha kulia n bwana Lwantwalr James Lutakoibwa kutokaMwananyamala Picha kulia ni Kijungu C Mwanji mkazi wa wazo...
WAZIRI wa mambo ya nje wa Uingereza Phillip Hammond amekutana na rais wa Iran Hassan Rouhani mjini Tehran kwaajili ya mazungumzo ya kiserikali baina ya nchi hizo mbili. Waziri Hammond amesema Iran ina ushawishi mkubwa katika eneo la Mashariki ya Kati na inaweza kuwa mshirika mojawapo muhimu katika mapambano dhidi ya ugaidi. Amesema mataifa hayo mawili yana msimamo wa pamoja licha ya historia ya kutoaminiana na yamekubaliana juu ya hoja ya kulishinda kundi la Dola la Kiislamu na kuzuia mihadarati...
IMEELEZWA kuwa kukosekana kwa huduma ya umeme katika baadhi ya vituo vya afya Jijini Mwanza kumesababisha kuzorota kwa upatikanaji wa huduma katika vituo hivyo. Zainabu Chambo ni Muuguzi kutoka zahanati ya Buhongwa iliyopo wilaya ya Nyamagana Jijini humo amesema hali hiyo husababisha mama wajamzito kwenda kutafuta zahanati nyingine kwa umbali mrefu kwaajili ya kupatiwa huduma hali inayowalazimu kutoa kiasi kikubwa cha fedha. Zainabu amesema kitendo cha kukosekana kwa umeme kimewawia vigumu wao kufanya ufuatiliaji na kujua nani ana...
CHUO kikuu cha Dodoma-UDOM-kinatarajia kufanya hafla ya kumuenzi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dokta Jakaya Mrisho Kikwete kama sehemu ya kutambua mchango wake wa kuwezesha kujengwa kwa chuo hicho. Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa chuo hicho profesa Idris Kikula wakati akizungumza na baadhi ya mabalozi na maafisa wa uwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania katika umoja wa mataifa inasema kuwa Rais Kikwete amefanya kazi kubwa katika kuhimiza na kufanikisha ujenzi wa chuo hicho. Profesa Kikula...
KATIKA kufanya Tathmini ya matatizo ya usafiri kwenye jiji la Dar es salaam, Mgombea Urais kupitia vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi-UKAWA– Edward Lowasa akiambatana na Mgombea mwenza Juma Duni Haji ametembelea maeneo mbalimbali ya jiji kwa kutumia usafiri wa daladala. Lowasa ametumia usafiri huo majira ya asubuhi akitokea Gongo la Mboto wilayani Ilala jijini Dar es salaam hadi eneo la Pugu na kutoka Pugu hadi Mbagala ambapo amejionea namna ambavyo wananchi wa Dar es salaam wanavyopata shida...
JUKWAA la Tiba asili Tanzania limewaasa wananchi kuithamini na kuendeleza Amani iliyopo kwa kuepuka kujihusisha na vishawishi vitakavyosababisha kuvunjika kwa Amani. Wito huo umetolewa Jijini Dar es salaam na mwenyekiti wa Jukwaa hilo Bonaventure Mwalongo wakati akizungumza na kituo hiki juu ya umuhimu kwa watanzania kushiriki katika kuilinda na kuitetea Amani. Mwalongo amebainisha kuwa ni muda muafaka sasa kwa kila mtu bila kujali itikadi ya chama, dini au kabila kushirikiana kwa pamoja katika kila suala muhimu na lenye...
IMEELEZWA kuwa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, yanatarajia kusaidia kuboresha matundu ya vyoo katika shule 10 zilizopo manispaa ya Moshi na wilaya ya Moshi vijijini. Hayo yamesemwa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo –MASHIRIKA YA UN KUSAIDIA UJENZI WA MASHIMO YA VYOO KWENYE SHULE 10 MOSHIUNDP– nchini Alvaro Rodriguez katika hafla ya kuweka msingi kwa ajili ya ujenzi wa matundu 18 ya vyoo katika shule ya msingi Kiboriloni wilayani...
WAGOMBEA mbalimbali wa nafasi za urais leo wamerejesha fomu zao katika Tume ya Uchaguzi- NEC, tayari kwa uzinduzi wa Kampeni kuelekea uchaguzi Mkuu oktoba 25 mwaka huu. Akizungumza mara baada ya kurejesha fomu yake, mgombea kupitia chama cha mapinduzi- CCM Dokta John Magufuli amesema ametimiza matakwa yote ya kisheria na sasa kilichobaki ni uzinduzi wa kampeni. Kwa upande wake mgombea wa nafasi ya urais kupitia vyama vinavyounda umoja wa katiba UKAWA Edward Lowasa, amewataka viongozi na wanachama kumuunga...
MTU mmoja ambaye hajafahamika jina lake mara moja mkazi wa wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani amemuua mke wake kwa kumchoma kisu sehemu tofauti za mwili kufuatia kuwepo kwa ugomvi wa muda mrefu baina yao. Hali hiyo imetokana na kuwepo kwa sintofahamu baina ya wanafamilia hao suala ambalo awali lilifikishwa kituo cha polisi kilichopo wilayani hapo kwaajili ya kulitolea ufafanuzi. Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Pwani ULRICH MATEI amesema kuwa tukio hilo limetokea katika...
TUME ya Taifa ya uchaguzi Makao makuu, leo imeanza kupokea fomu za uteuzi za vyama 13 kwa ajili ya uteuzi wa nafasi ya kugombea urais kwa ajili ya uchaguzi mkuu ambao utafanyika hapa nchini mwezi oktoba mwaka huu. Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na NEC, Zoezi hilo limeanza leo saa tatu asubuhi na chama cha UPDP na saa tano hiii ni zamu ya Mgombea wa Chama cha Mapinduzi –ccm baada ya mgombea wa Chadema kufanya hivyo saa nne asubuhi. Mwenyekiti...
IMEELEZWA kuwa Tanzania imefanikiwa kufikia miongoni mwa malengo ya millennia yakupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano pamoja na vifo vya akina mama wakati wa kujifungua. Hayo yamebainisha leo na mratibu wa maswala ya uzazi kutoka Wizara ya Afya Dokta Kokeleth Winani alipomwakilisha katibu mkuu wa wizara hiyo katika uzinduzi wa mtandao wa waandishi wa habari wa afya ya uzazi na jinsia. Amesema kwa sasa katika kila vizazi elfu moja, watoto wanaopoteza maisha ni...