WAZIRI wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu amesema kuwa matumizi mabaya ya ardhi yasiyozingatia mpango bora yamekuwa tishio kwa maeneo yanayozunguka hifadhi za jamii. Nyalandu ameyasema hayo wakati akihutubia mkutano kati ya Wizara na Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori –WMAs– uliofanyika jijini Arusha ambapo amesema kuwa ili kuwa na uhifadhi endelevu utakaorithiwa na vizazi vijavyo mpango wa matumizi bora ya ardhi hauna budi kuzingatiwa. Aidha amesema kuwa ujenzi wa miji katika maeneo ya hifadhi ikiwemo Hoteli na kumbi za...
SERIKALI imeahidi kuendelea na shughuli za uboreshaji wa miundombinu katika maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kuwaletea manufaa zaidi wananchi. Hayo yamesemwa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Ujenzi dokta JOHN MAGUFULI wakati akijibu swali la mbunge wa ubungo mheshimiwa John Mnyika aliyetaka kufahamu mikakati ya serikali juu ya suala hilo. Mheshimiwa Magufuli amesema kuwa kwa kiasi kikubwa serikali imekamilisha uboreshaji wa miundombinu katika maeneo mbalimbali na kwamba ipo tayari kuendelea na utekelezaji wa mikakati hiyo...
SERIKALI kupitia vyombo vya ulinzi na Usalama vimeombwa kuchunguza Asasi, Taasisi, Mashirika na watu binafsi wanaotumia mwamvuli wa matatizo ya watu wenye ulemavu wa ngozi kujinufaisha kwa kufanya harambee mbalimbali. Katibu wa Chama cha Maalbino Wilaya ya Temeke Gaston Mcheka ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam baada ya kile alichodai kuchoshwa na tabia ya baadhi ya watu kukusanya pesa kwa ajili ya kuwasaidia albino na badala yake kutokomea pasipo walengwa...
JAMII imeombwa kuwa na mazoea ya kupima afya zao mara kwa mara hususani kwa Watoto ilikuweza kutambua matatizo au magonjwa ya moyo mapema kwakuwa idadi inonesha katika watoto milioni moja na laki saba waliozaliwa mwaka 2014 asilimia 1 mpaka 2 ya watoto hao sawa na watotoelf 13 na mia 6 wanamagonjwa ya moyo mbalimbali. Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam wakati wakutiliana saini mkataba wa makubaliano maalum kati ya Hospitali ya Taifa Muhimbili na Taasisi binafsi ya misaada ya...
SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa ANNE MAKINDA amelazimika kuahirisha kikao cha bunge kabla ya wakati kufuatia Muongozo ulioombwa na mbunge wa Ubungo mheshimiwa JOHN MNYIKA juu ya kubadili mfumo wa uwasilishwaji na upitishwaji wa miswada ambayo bado haijawasilishwa hali iliyosababisha kutoelewana kwa wabunge wa chama tawala na wabunge wa vyama vya upinzani. Hali hiyo imekuja baada ya wabunge wa vyama vya upinzani kuonesha hali ya kuonewa kwa madai kuwa hawapewi nafasi ya kutosha katika kujadili...
WAZIRI MKUU wa Ethiopia Heilemariam Disalegn Boshe leo anatembelea Kiwanda cha kutengeneza Dawa za Kuulia Wadudu-TAMCO- kilichopo Kibaha Mkoani Pwani akiongozana na Mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Ziara hiyo ya siku mbili ni sehemu ya Mapambano ya Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Nchi ya Ethiopia dhidi ya Mazalia ya Mbu ili kudhibiti kuenea kwa Ugonjwa wa Malaria ambapo Waziri Mkuu Boshe ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Viongozi wa Afrika katika Mapambano dhidi ya Malaria. Mheshimiwa Boshe amewasili jana...
IMEELEZWA kuwa, Magonjwa yasiyoambukiza kama vile kansa, kisukari na shinikizo la damu, yameonesha kushika kasi katika nchi zinazoendelea hususani nchi ambazo zinauchumi mdogo zaidi ikiwemoTanzania. Hayo yamesemwa leo na Kaimu Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya Dokta CHARLES MASSAMBU alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya ufunguzi wa semina iliyoandaliwa na Wizara hiyo ambayo imehusisha Sekta mbalimbali yenye lengo la kujadili namna ya kuthibiti na kuzuia magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza nchini....
SERIKALI imewasilisha mswada wa sheria ya kuwalinda watoa taarifa za uhalifu na mashahidi wa mwaka 2015 unaolenga kuweka utaratibu wa kisheria wa kulinda watoa taarifa za uharifu na mashahidi. Akiusoma kwa mara ya pili leo Bungeni mjini Dodoma, Waziri wa Katiba na Sheria, Dokta Asha Rose Migiro, amesema lengo hilo litatekelezwa kwa kuimarisha mifumo iliyopo ya upatikanaji wa taarifa za...
KUPITIA mradi wa gesi wa kuongeza sifa za kuajiriwa kupitia mafunzo ya ufundi stadi, Chuo cha mafunzo na ufundi stadi –VETA, kimetoa nafasi ya mafunzo ya gesi kwa wanafunzi wa vyuo hivyo ili kuweza kuongeza wataalamu zaidi katika sekta hiyo. Akizungumza na efm, mwalimu wa taaluma ya umeme chuo cha ufundi veta Lindi, MAJOLE MWIGOLE amesema kuwa wameamua kuweka mafunzo hayo ili vijana wengi waweze kuingizwa katika sekta hiyo na kuepuka kuchukua wataalamu kutoka...
SERIKALI imelitaka Shirikala la Umeme nchini-Tanesco kuhakikisha linafuatilia mita zenye matatizo hususani za luku, ili kuondoa usumbufu kwa wateja wao na kuwafungia mita zinazofanya kazi. Kauli hiyo ya Serikali imetolewa leo Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage wakati akijibu swali la mheshimiwa Diana Chilolo, Mbunge wa Viti Maalum, katika kipindi cha maswali na majibu. Katika swali lake Mheshimiwa Chilolo alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kutoa elimu kwa wananchi juu ya mita mpya ambazo...
IMEELEZWA kuwa migogoro ya Ardhi hapa Nchini inasababishwa na baadhi ya Viongozi wa Serikali za Mitaa na Vijiji wasiokuwa na uelewa mpana kuhusu maswala ya sheria na utaratibu wa ugawaji ardhi. Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Mwemwekiti wa Jukwaa la Ardhi Tanzania Docta STEPHEN MUNGA amesema kuwa suala la migogoro ya ardhi limekuwa ni changamoto kubwa katika jamii hususani ya wakulima na wafugaji ambao wamekuwa na madai ya mara kwa mara katika maeneo yao. MUNGA ameongeza kuwa...