Local News

WIZARA YA MAJI IMELIOMBA BUNGE KUHIDHINISHA SHILINGI BILIONI 455
Local News

WIZARA ya Maji imeliomba Bunge kuidhinisha kiasi cha shilingi bilioni 455, milioni 900 laki 9 na elfu 81 kwaajili ya kuboresha utekelezaji wa miradi ya maji katika kipindi cha mwaka 2015 hadi 2016.   Akiwasilisha makadilio ya matumizi ya wizara, waziri wa wizara hiyo Profesa JUMANNE MAGHEMBE amesema kuwa kiasi hicho cha fedha kitasaidia kurahisisha ukamilishaji wa miradi hiyo ambapo kati ya kiasi hicho shilingi bilioni 17 zitatumika kwaajili ya mishahara.   Kwa upande wake kamati ya kudumu ya bunge...

Like
276
0
Friday, 05 June 2015
SHERIA YA MTOTO YA MWAKA 1971 YACHANGIA UWEPO WA NDOA NA MIMBA ZA UTOTONI
Local News

SEREKALI  imetakiwa kuangalia upya sheria ya  mtoto ya mwaka 1971 kwani imebainika kuwa ni chanzo kimojawapo kinachoruhusu uwepo wa ndoa na mimba za utotoni.   Akizungumza katika kongamano lililoandaliwa na shirika la intiative for youth –INFOY– mwenyekiti wa baraza la watoto wilaya ya Arusha HASSANI OMARY amesema kuwa ni wajibu wa serekali kuangalia upya sherika hiyo kwani imekuwa ikiwaathiri watoto wengi hapa nchini.   Amesema kuwa sheria hii imekuwa ikiruhusu watoto hata wenye umri chini ya miaka 18 kuolewa  iwapo...

Like
296
0
Friday, 05 June 2015
RAIS AJAE ATAKIWA KULINDA NA KUDUMISHA MUUNGANO
Local News

IMEELEZWA kuwa rais mpya ajaye nchini Tanzania anakabiliwa na changamoto kubwa ya kuhakikisha Tanzania inaendelea kubakia kuwa moja kwa kudumisha Umoja na Amani kwani Tanzania inatokana na muungano wa nchi mbili. Kauli hiyo imetolewa na rais Jakaya Kikwete jijini Stockholm – Sweden ambapo alikuwa akiongea na watanzania waishio Sweden mara baada ya kuwasili na kuanza ziara ya kikazi ya siku 3, kuanzia tarehe 3 hadi 5 Juni, mwaka huu. Watanzania mbalimbali walioko nchini Sweden kwa ajili ya shughuli za kikazi,...

Like
233
0
Friday, 05 June 2015
TMA YAKUTANA NA WADAU KUJADILI USHIRIKISHAJI WA TAARIFA ZA HALI YA HEWA
Local News

KATIKA kudhibiti athari za majanga yatokanayo na mabadiliko ya hali ya hewa ikiwemo mafuriko, mamlaka ya hali ya hewa nchini-TMA-imekutana na wadau mbalimbali kujadili juu ya ushirikishaji wa taarifa za hali ya hewa ili kupunguza madhara hayo. Akizungumza katika warsha iliyowakutanisha wadau hao leo jijini Dar es salaam Kaimu mkurugenzi wa –TMA– dokta LADISLAUS CHANG’A amesema kuwa ili kudhibiti majanga hayo ni muhimu kwa kila mtu kuwa mfuatiliaji wa masuala ya hali ya hewa kila inapotolewa na mamlaka hiyo. CHANG’A...

Like
307
0
Thursday, 04 June 2015
RAIS AJAE ATAKIWA KUWA KIONGOZI MWENYE KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WALIMU
Local News

UMOJA wa mabadiliko ya walimu Tanzania –VUMAWATA umemwomba rais ajae awe kiongozi ambae ataweza kutatua  changamoto mbalimbali zinazo wakabili walimu hapa nchini. Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Mwenyekiti Taifa wa Umoja huo ALLY MAKWIRO amesema kuwa changamoto za walimu zimekuwa ni kitu cha kawaida na hazijapata suluhisho la kudumu mpaka sasa kitu ambacho kinasababisha walimu kuwa masikini na kutokuwa na hadhi katika nchi na jamii kwa ujumla. MAKWIRO amesema kuwa walimu wana changamoto nyingi katika maisha...

Like
301
0
Thursday, 04 June 2015
UKAME WAATHIRI SEHEMU KUBWA YA ARDHI YA NCHI
Local News

OFISI ya Makamu wa Rais- Mazingira imebainisha kuwa takribani asilimia 61 hadi 75 ya eneo la ardhi ya Tanzania limeathirika na janga la ukame ambao unaweza kusababisha uzorotaji wa shughuli za ukuaji wa uchumi. Hayo yalielezwa na Afisa Mazingira wa Ofisi ya Makamu wa Rais, ZAINAB SHABAN wakati akitoa mada katika semina ya kukuza uelewa wa masuala ya usimamizi wa mazingira kwa watendaji wa halmashauri ya jiji la Tanga mkoani humo. Aidha amesema kuwa uchumi wa Tanzania unategemea kwa kiasi...

Like
333
0
Thursday, 04 June 2015
RITA YAWATAKA WANANCHI KUWA NA TABIA YA KUANDIKA WOSIA KATIKA FAMILIA ZAO
Local News

KATIKA kuelekea wiki ya Utumishi wa Umma nchini Wakala wa usajili na  udhibiti  wa Vizazi na Vifo- RITA-imewataka wananchi kuwa na tabia ya kuandika wosia katika familia zao ili  kuepusha utata na migogoro ya mara kwa mara  inayoweza kujitokeza mara baada ya mtu kufariki. Akizungumza na efm Meneja Masoko, Mawasiliano na Elimu kwa Umma kutoka –Rita– JOSEPHAT  KIMARO amesema kuwa kumekuwa na  dhana kwa jamii kuwa mtu akiandika wosia  anajitabiria kifo jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo katika familia nyingi. Aidha...

Like
308
0
Wednesday, 03 June 2015
WAFUGAJI NCHINI WAMETAKIWA KUFUATA SHERIA NA KUACHA TABIA YA KUCHUKUA SHERIA MKONONI
Local News

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dokta Mohammed Gharib Bilal amewataka wafugaji nchini kuhakikisha wanafuata sheria na kuachana na tabia ya kuchukua sheria mkononi ili kufanikisha usalama wao na watu wengine.   Mheshimiwa BILAL ameyasema hayo Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kupokea ujumbe kutoka kwa Chama cha Wafugaji Tanzania ulioongozwa na Mwenyekiti wao ALLY HAMIS LUMIYE. Awali akizungumza kwa niaba ya Baraza la Wazee wa Chama hicho Tanzania, Mwenyekiti wa Chama amesema kuwa chama chao...

Like
241
0
Wednesday, 03 June 2015
SUMAYE ATANGAZA RASMI NIA YA KUWANIA NAFASI YA URAIS KWA TIKETI YA CCM
Local News

WAZIRI Mkuu mstaafu mheshimiwa FREDERICK SUMAYE leo ametangaza rasmi nia ya kuwania nafasi ya urais kwa tiketi ya chama cha mapinduzi na kuhidi kuwa endapo atapewa ridhaa hiyo atahakikisha anawakwamua watanzania katika umaskini na kupambana na maovu. Mheshimiwa SUMAYE ametoa ahadi hiyo jijini Dar es salaam wakati akiongea na wananchi juu ya malengo yake katika kulisaidia Taifa kukua kimaendeleo na kuingia katika ushindani wa kiuchumi. Aidha akiwahutubia wananchi Waziri huyo mstaafu amebainisha kwamba anazo sifa zote za kuwaongoza wananchi...

Like
213
0
Tuesday, 02 June 2015
BUNGE LAAHIRISHWA KUFUATIA KIFO CHA MBUNGE WA JIMBO LA UKONGA EUGENE MWAIPOPO
Local News

NAIBU spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa JOB NDUGAI amelazimika kuahirisha shughuli za bunge hadi june 4 mwaka huu kufuatia kifo cha mbunge wa jimbo la Ukonga Eugene Mwaiposa kilichotokea nyumbani kwake Chaduru mjini Dodoma kwa shinikizo la damu. Naibu spika Ndugai amesema kuwa mwili wa marehemu umepelekwa katika hospitali ya mkoa wa Dodoma kwa uchunguzi zaidi ambapo shughuli za kuaga mwili huo itafanyika kesho mjini humo. Awali kabla ya bunge kupokea taarifa hiyo wizara ya...

Like
390
0
Tuesday, 02 June 2015
BAN KI-MOON ALAANI KUFUKUZWA KWA MRATIBU WA MISAADA YA KIBINAADAMU WA UMOJA WA MATAIFA
Local News

KATIBU Mkuu wa umoja wa mataifa BAN KI-MOON amelaani kufukuzwa kwa mratibu wa misaada ya kibinaadamu wa Umoja wa Mataifa TOBY LANZER huko nchini Sudan Kusini . Katibu mkuu huyo ameitaka serikali hiyo kubadili uamuzi huo mara moja kwa kuwa  Lanzer alikuwa mstari wa mbele katika kutafuta ufumbuzi wa mahitaji kwa jamii ya nchi hiyo iliyoathiriwa na mzozo kwa kuhakikisha kwamba misaada inawafikia. Aidha amesema kuwa suala hilo ni muhimu sana hasa kwa wakati huu wa vurugu zinazoendelea kwa pande...

Like
270
0
Tuesday, 02 June 2015