Global News

Trump arudi nyuma katika sera yake ya kuzitenganisha familia
Global News

Rais Donald Trump wa Marekani amesitisha sera yake uhamiaji iliyokuwa inalazimu kuzitenganisha familia za wahamiaji wanaobainika kuvuka mipaka kinyume cha sheria na watoto wao. Pamoja na kulegeza msimamo huo kutokana na kulalamikiwa kwa sera hiyo ndani na nje ya taifa hilo, Trump amesisitiza kwamba bado ataendelea kuilinda mipaka yake. Rais Trump ambaye tangu kuingia kwake madarakani alionekana kuhitaji sheria kali zaidi ya kukomesha suala la uhamiaji haramu, amejikuta matatani, safari na hasa baada ya picha zenye mguso za watoto...

Like
415
0
Thursday, 21 June 2018
Marekani yajitoa katika baraza la Umoja wa Mataifa la haki za binaadamu
Global News

Marekani imejitoa katika baraza la haki za binaadamu la Umoja wa Mataifa na kulitaja kuwa na ‘unafiki wa kisiasa na lenye upendeleo’. “Taasisi hiyo ya “unafiki na upendeleo inakejeli haki za binaadamu”, amesema mjumbe wa Marekani katika Umoja huo Nikki Haley. Bi Haley mwaka jana alilishutumu baraza hilo kwa kuwa na “upendeleo mkali dhidi ya Israel” na kusema Marekani inatafakari uwanachama wake. Baraza hilo lililoundwa mnamo 2006, lililo na makao yake Geneva limeshutumiwa kwa kuruhusu mataifa yenye...

Like
393
0
Wednesday, 20 June 2018
Mwanamuziki XXXTentacion auawa kwa kupigwa risasi Florida, Marekani
Global News

Mwanamuziki wa nyimbo za rap Marekani XXXTentacion, ambaye alipata umaarufu kwa haraka kupitia albamu zake mbili ameuawa kwa kupigwa risasi akiwa na miaka 20. Alikuwa anaondoka kwenye duka la kuuza pikipiki kusini mwa Florida Jumatatu pale mtu mwenye bunduki alipomfyatulia risasi. Polisi katika tarafa ya Broward wanasema XXXTentacion, ambaye jina lake Jahseh Onfroy, alikimbizwa hospitalini lakini akathibitishwa kufariki. Alikuwa mara nyingi akielezwa kama mmoja wa wanamuziki wa rap wenye kuzua utata zaidi. Alikuwa pia amekabiliwa na mashtaka...

Like
917
0
Tuesday, 19 June 2018
‘Spiderman’ aliyemuokoa mtoto Ufaransa arejea kwao Mali
Global News

Mhamiaji raia wa Mali Mamoudou Gassama, ambaye alipata umaarufu kote duniani mwezi uliopita wakati alikwea jengo mjini Paris, Ufaransa kumukoa mtoto, amesema amefurahishwa sana kurudi kwao Mali kutembea. “Nina furaha sana. Nina furaha sana sana kwa sababu kila mtu alikuja uwanja wa ndege na kisha nikamuona baba yangu na watu wote wa familia yangu. Sikuwa nimemuona baba yangu kwa miaka tisa,” aliiambia BBC. Video ya Mamoudou Gassam akimuokoa mtoto ilisambaa sana kwenye mitandao ya kijamii. Alivuka kutoka kwenye ubaraza mmoja...

Like
419
0
Tuesday, 19 June 2018
Ivan Dukee aibuka mshindi Urais Colombia
Global News

Mshindi wa uchaguzi wa urais nchini Colombia, Ivan Dukee amewahutubia wafuasi wake mjini Bogota. Bwana Dukee, mwenye umri wa miaka 41,aliahidi kufanyia marekebisho mkataba wa amani uliyofikiwa kati ya serikali na wapiganaji wa FARC. Alijizolea asilimia 54 ya kura ikiwa ni asilimia kumi na mbili zaidi ya mpinzani wake,Gustavo Petro ambaye ni mpiganaji wa zamani. Bwana Duque anatajwa kuwa ni chaguo la wafanyabiashara kwa sababu anataka kupunguza na kuongeza uwekezaji na kuongeza thamani ya fedha. Hata hivyo matokeo hayo bado...

Like
541
0
Monday, 18 June 2018
Wahamiaji wakataliwa na nchi za Ulaya Hispania
Global News

Meli tatu zimeegesha nchini Hispania,zikiwa mamia ya wahamiaji waliokolewa majini wiki iliyopita wakitokea nchini Libya.Wameorodheshwa na kuendelea kupatiwa matibabu na misaada. Serikali ya Hispania imekubali kuwachukua,baada ya Italia na Malta kukataa meli hizo zilizowaokoa wahamiaji hao kuegesha katika bandari.Tukio hili limezua mjadala wa kisiasa Ulaya. Shrika la msalaba mwekundu,limezitaka nchi za jumuiya ya Ulaya,kuiga mfano wa Hispania kuonyesha mshikamano katika suala la wahamiaji. Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini...

Like
442
0
Monday, 18 June 2018
Marekani inaitaka Korea Kaskazini kuangamiza silaha ifikapo 2020
Global News

Marekani ina matumaini ya kuanza kuona shughuli ya kuangamizwa silaha nchini Korea Kaskazini ifikapo mwaka 2020, mwa mujibu wa waziri wa mashauri ya nchi za kigeni Mike Pompeo. Matamshi yake aliyoyatoa alipofanya ziara nchini Korea Kusini, yanafuataia mkutano kati ya Rais Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un. Walisaini makubaliano ya kufanya kazi katika kuangamiza kabisa silaha za nyuklia katika rasi ya Korea. Lakini nakala hiyo imekosolewa kwa kukosa taarifa za kina kuhusu ni lini na ni vipi...

Like
543
0
Thursday, 14 June 2018
Kim Jong-un na Trump waalika kwenye Nchi Zao
Global News

Shirika la habari la serikali nchini Korea Kaskazini limesema kuwa kiongozi wa taifa hilo Kim Jong Un amekubali mwaliko wa Rais wa Marekani Donald Trump wa kufika Washington. Kiongozi huyo alipewa mwaliko wakati wa mkutano wa historia baina ya wawili hao nchini Singapore Jumanne. Kim pia alimwalika pia Trump kutembelea Pyongyang. “Viongozi ao wawili wakuu walikubali mwaliko wa kila mmoja,” shirika la KCNA limeripoti. Kenye tamko lake la kwanza kabisa tangu kutokea kwa mkutano huo, Bw Kim amenukuliwa akisema kwamba...

Like
527
0
Wednesday, 13 June 2018
Trump na Kim Jong-un wawasili Singapore
Global News

Rais wa Marekani Donald Trump na Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un wamewasili Singapore kwa ajili ya mkutano wao unaoelezwa kuwa wa kihistoria. Trump aliwasili saa chache tu baada ya Kim kuwasili na ujumbe wake. Mkutano wao ambao ni wa kwanza utafanyika siku ya Jumanne katika kisiwa cha Sentosa. Uhusiano wa viongozi hawa wawili umepitia kwenye milima na mbonde kwa kipindi cha miezi 18 iliyopita, wakirushiana matusi na kutishiana vita kabla ya uhusiano wao kuchukua mkondo mwingine na kuamua wawili...

Like
635
0
Sunday, 10 June 2018
Mchungaji auawa akiwabatiza waumini Ziwani
Global News

Mchungaji wa Kiprotestanti Docho Eshete aliyekuwa akibatiza watu katika ziwa Ayaba kusini mwa Ethiopia ameuawa na mamba. Mashambulizi yaliyo karibu na mji wa Arba Minch yanahusishwa na kupunguza idadi ya samaki ambacho ni chakula cha Mamba na hivyo kuanza kuvamia watu na kuwaua. Mchungaji, Docho, ndo kwanza alikuwa ameanza kumbatiza mfuasi wa kwanza kati ya themanini waliokwenda kufanyiwa huduma hiyo katika ziwa Ayaba, huko Ethiopia wakati mamba aliporuka nje kutoka majini na kumchukua mchungaji huyo. Mchungaji alijitahidi kupambana na...

Like
497
0
Wednesday, 06 June 2018
Kenya Yapiga Marufuku Kuwatembelea Watoto Shuleni
Global News

Wizara ya Elimu nchini Kenya imeivunjilia mbali bodi ya usimamizi wa shule ya Moi Girls na kutangaza kwamba ni marufuku kuwatembelea watoto shuleni baada ya mapumziko ya katikati ya muhula kwa shule zote za upili za umma. Hii ni kufuatia uchunguzi unaoendelea kubaini kesi ya ubakaji wa mwanafunzi katika shule hiyo. Waziri wa Elimu nchini Amina Mohammed alitoa agizo kwa maafisa katika wizara yake wafanye upya ukaguzi wa usalama katika shule zote kuepuka uwezekano wa wanafunzi kuingiliwa. Mwalimu mkuu katika...

Like
637
0
Wednesday, 06 June 2018