Global News

AL SHABAAB ALIYEJIUNGA NA IS ANASWA SOMALIA
Global News

KAMANDA wa kundi la al-Shabaab aliyejiunga na kundi linalojiita Islamic State nchini Somalia amekamatwa na maafisa wa usalama nchini humo.   Hassan Mohamed Siad ambaye pia hujulikana kama Hassan Fanah alikamatwa jana Jumapili baada ya maafisa wa ujasusi wa Somalia kufanya operesheni katika nyumba moja mtaa wa Kahda.   Vyombo ya habari nchini Somalia vinasema alikuwa anajificha katika mtaa huo kutoka wa wapiganaji wa al-Shabab. Serikali ya Somalia ilikuwa imeahidi zawadi ya $2,000 kwa mtu ambaye angetoa habari za kusaidia kukamatwa...

Like
259
0
Monday, 25 April 2016
ICC YAANZISHA UCHUNGUZI WA AWALI KUHUSU MAUAJI YA BURUNDI
Global News

MWENDESHA mashtaka mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) amesema mahakama hiyo imeanzisha uchunguzi wa awali kuhusu mauaji ambayo yamekuwa yakitokea nchini Burundi.   Bi Fatou Bensouda amesema amekuwa akifuatilia kwa karibu matukio ya Burundi tangu Aprili 2015 na kwamba mara kwa mara amezitaka pande zote husika kutojihusisha na ghasia na mauaji.   Watu 430 wameuawa na wengine 3,400 kukamatwa tangu kuanza kwa machafuko Aprili mwaka...

Like
308
0
Monday, 25 April 2016
MAREKANI KUPELEKA MAJESHI SYRIA
Global News

MAAFISA wakuu nchini Marekani wanasema kuwa Rais Barack Obama atatuma wanajeshi wa ziada wapatao 250 nchini Syria, ili kuunga mkono jitihada zinazofanywa na vikosi vya ndani vya nchi hiyo, katika kupambana na wapiganaji wa Islamic State. Kwa mujibu wa maafisa hao, lengo hasa ni kuwasajili waarabu wa dhehebu la Sunni kuungana na wapiganaji wa kikurdi waliopo kaskazini mashariki mwa Syria. Hata hivyo vikosi hivyo vya Marekani havitawajibika moja kwa moja katika mapambano...

Like
342
0
Monday, 25 April 2016
SUDAN KUSINI: MATAIFA YENYE NGUVU YATAKA MACHAR AREJEE JUBA
Global News

MATAIFA makuu duniani yamewapa muda viongozi wa pande zinazohasimiana nchini Sudan Kusini kuhakikisha wanakubaliana na kuhakikisha kiongozi wa zamani wa waasi Riek Machar anarejea Juba ifikapo kesho. Mataifa hayo yamesema kuwa wakishindwa kukubaliana, makubalianao ya amani yaliyolengwa kumaliza miaka miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe yatavunjika. Siku ya Jumamosi April 23 imewekwa na wawakilishi wa  halmashauri ya JMEC iliyoundwa na Umoja wa Afrika, Umoja wa Ulaya, China, Uengereza, Norway na Marekani ambapo Sudan Kusini ni mwanachama wa...

Like
313
0
Friday, 22 April 2016
MAREKANI: IDADI YA WATU WANAOJIUA YAONGEZEKA
Global News

TAKWIMU rasmi za serikali zinaonesha idadi ya watu wanaojiua nchini Marekani imeongezeka kwa kiasi kikubwa. Takwimu hizo kutoka Kituo cha Taifa cha Takwimu za Afya zinaonyesha kuwa viwango vya watu kujiua vimeongezeka kwa karibu asilimia 25 katika kipindi cha miaka 15 iliyopita. Utafiti huo uliofanyika kwa jinsia zote umeonesha kwamba viwango vya wanawake kujiua ndivyo vilivyoongezeka zaidi, vikipanda kwa asilimia 36 vikiwahusisha zaidi wanawake wa umri wa makamo.                        ...

Like
346
0
Friday, 22 April 2016
VOLKSWAGEN YATANGAZA KUNUNUA MAGARI YAKE
Global News

KAMPUNI ya magari ya Volkswagen imetangaza kuyanunua magari ya kampuni yake kutoka kwa wateja nchini Marekani yapatayo laki tano kama sehemu ya kutimiza makubaliano yaliyoafikiwa na idara ya sheria ya Marekani dhidi ya kampuni hiyo kuhusika na kashfa ya uchafuzi wa hali ya hewa. Jaji kutoka San Francisco hajabainisha wazi kiasi ambacho wamiliki wa magari hayo watalipwa na kampuni ya Volkswagen pale watakapo iuzia kampuni hiyo magari yake wanayoyamiliki. Makubaliano mengine yaliyofikiwa ni kwamba Volkswagen itatakiwa kutoa fungu la fedha...

Like
256
0
Friday, 22 April 2016
OBAMA AISIHI UINGEREZA ISIJITOE EU
Global News

RAIS wa Marekani Barack Obama amesema anaunga mkono Uingereza kubaki katika jumuiya ya Umoja wa Ulaya ili kuweza kuchangia katika vita dhidi ya ugaidi na masuala ya wahamiaji na utatuzi wa migogoro ya kiuchumi. Rais Obama amenukuliwa na gazeti la Uingereza la Telegraph, akisema kwamba uanachama wa Uingereza katika umoja wa Ulaya una umuhimu mkubwa na endapo nchi hiyo itajiondoa katika umoja huo itapunguza nguvu katika vita dhidi ya ugaidi duniani. Hata hivyo Obama amesema anatetea hoja ya umoja wa...

Like
285
0
Friday, 22 April 2016
KENYA YAITAKA ICC KUIKABIDHI FAILI ZA WASHUKIWA 3
Global News

KENYA sasa inataka faili za kesi zinazowakabili wakenya watatu wanaotuhumiwa kuingilia ushahidi wa mashahidi wa ICC kushtakiwa nchini humo. Mwanasheria mkuu Profesa Githu Muigai amesema kuwa Kenya ina mahakama zilizo na uwezo za kushtaki kesi ndogo kufuatia kuanguka kwa kesi kuu iliowahusisha wakenya sita maarufu kama Ocampo 6. Mwanasheria huyo pia ameshtumu idara ya mashtaka katika mahakama ya ICC kwa kushindwa kushirikiana na Kenya kuhusu ombi la awali lililowasilishwa kwa aliyekuwa kiongozi wa mashtaka Moreno Ocampo kuikabidhi Kenya faili...

Like
233
0
Thursday, 21 April 2016
KANALI WA JESHI AUAWA BURUNDI
Global News

KANALI mmoja wa Jeshi amepigwa risasi na watu wasiojulikana katika mji mkuu wa Burundi ,Bujumbura,kulingana na vyombo vya habari vya kundi la SOS nchini humo. Kanali Emmanuel Buzubona aliuawa pamoja na mtu mmoja aliyekuwa akiendesha pikipiki siku ya Jumatano kaskazini mwa makaazi ya mji huo. Ni miongoni mwa maafisa wa jeshi wa hivi karibuni kuuawa tangu rais Pierre Nkurunziza kunusurika jaribio la mapinduzi na maandamano kufuatia hatua yake ya mwaka jana kujiongezea muda wa kuhudumu kama rais wa taifa...

Like
273
0
Thursday, 21 April 2016
WAKIMBIZI 500 WAHOFIWA KUFA KWENYE BAHARI YA MEDITERANIA
Global News

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa linaloshughulkia wakimbizi limehofu kuwa huenda wakimbizi 500 wamefariki kwenye bahari ya Mediterania walipokuwa njiani kuelekea Italia. Hata hivyo msemaji wa shirika hilo amewaambia waandishi wa habari kwamba haijulikani ni lini wakimbizi hao wamefariki lakini amesema wachunguzi wanawahoji wakimbizi 41 walionusurika. Umoja wa Mataifa umebaisha kwamba miongoni mwa watu waliookolewa walikuwa wakimbizi kutoka Somalia, Ethiopia, Misri na...

Like
380
0
Thursday, 21 April 2016
KURA YA KUMTIMUA ROUSSEF ITAFANYIKA
Global News

MAHAKAMA ya juu zaidi nchini Brazil imekataa ombi la serikali la kutaka kutupiliwa mbali kura ya bunge kuamua ikiwa rais Dilma Rousseff ataondolewa madarakani. Mahakama imekataa kufuta amri ya kupiga kura iliyoamuliwa na spika wa bunge la chini, ambayo itaamua siku ya Jumapili ikiwa Rousseff ataondolewa madarakani au la. Wafuasi wa rais huyo, walikuwa wamedai kuwa zoezi hilo litavurugwa kwa sababu wabunge kutoka majimbo yanayompinga Rousseff huenda wakapiga kura kwanza. Bi Rousseff amelaumiwa kwa kuvuruga bajeti kabla ya uchaguzi wa...

Like
289
0
Friday, 15 April 2016