Global News

SALVA KIRR AONYWA KUHESHIMU NA KUTEKELEZA MKATABA WA AMANI
Global News

MAREKANI imemuonya rais wa Sudan Kusini Salva Kirr, kuheshimu na kutekeleza mkataba wa amani aliousaini jana mjini Juba. Rais Kirr, alikuwa amekataa kusaini mkataba huo wiki iliyopita mjini Adis Ababa Ethiopia. Lakini, licha ya kusaini mkataba huo, ameelezea wasi wasi wake kuhusiana na masuala kadhaa ya mkataba huo, hasa kugawana madaraka na waasi....

Like
285
0
Thursday, 27 August 2015
LAMORDE AKANUSHA UFISADI NIGERIA
Global News

MKURUGENZI mkuu wa shirika la kupambana na ufisadi nchini Nigeria-EFCC– Ibrahim Lamorde amekanusha madai kuwa zaidi ya dola bilioni tano zimetoweka kutoka kwa hazina ya shirika hilo. Lamorde amesema kuwa hata fedha zilizokusanywa na –EFCC- zikijumuishwa na ufadhili wote unaotolewa na shirika hilo, haziwezi kufika dola bilioni tano kwa pamoja. Aidha ameliambia shirika la utangazaji la BBC kuwa madai hayo hayana msingi na yananuia kumharibia sifa, kwa sababu EFCC kwa sasa bado inamchunguza mtu aliyetoa madai...

Like
254
0
Thursday, 27 August 2015
NKURUNZIZA KUPAMBANA NA MAUAJI
Global News

KATIKA hotuba yake aliyoitoa kwa taifa zima rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza ameonyesha hisia zake kuhusu kujumuisha vikosi vya ulinzi na usalama nchini humo. Hayo yamekuja wiki moja baada ya Rais huyo kuapishwa kushika nafasi ya Urais wa nchi hiyo kwa muhula mwingine huku wakasoaji wakisema kuwa ni kinyume cha Katiba ya nchi hiyo. Rais Nkurunziza amezitaka kamati za ulinzi na usalama kufanya kazi usiku na mchana ili kupambana na kile alichokiita kundi la watu wachache wanaofanya mauaji na kusababisha...

Like
264
0
Thursday, 27 August 2015
MSCHANA WA MIAKA 16 AKIRI KUTEKELEZA UGAIDI UINGEREZA
Global News

MSICHANA mmoja mwenye umri wa miaka 16 amekiri kutekeleza ugaidi katika mahakama moja ya mjini Manchester Uingereza. Msichana huyo ambaye jina lake haliwezi kutajwa amekiri kumiliki vilipuzi na maelezo ya kutengeza bomu. Kukamatwa kwake mnamo mwezi Aprili kunafuatia uchunguzi na kitengo cha kukabiliana na ugaidi cha kaskazini magharibi. Alikamatwa pamoja na mvulana mmoja wa miaka 14 kutoka eneo la Blackburn ambaye amekiri kuhusika katika njama ya kuwashambulia polisi katika gwaride nchini Australia....

Like
237
0
Wednesday, 26 August 2015
SALVA KIIR KUSAINI MUAFAKA WA KUGAWANA MADARAKA
Global News

WAKATI leo rais wa Sudan  Salva Kiir akitarajia kusaini muafaka wa kugawana madaraka mjini Juba, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeongeza mbinyo kwa rais huyo, likionya kuwa liko tayari kuchukua hatua ya haraka ikiwa hatosaini muafaka wa kumaliza vita vilivyodumu miezi 20. Rais Kiir anatarajiwa kusaini muafaka wa kugawana madaraka mjini Juba , pamoja na viongozi wa Kenya, Uganda, Sudan na Ethiopia, lakini msemaji wake amesema bado hajaridhishwa. Kiongozi wa waasi Riek Machar alisaini makubaliano hayo wiki moja...

Like
170
0
Wednesday, 26 August 2015
UMOJA WA ULAYA KUISAIDIA HUNGARY JUU YA ONGEZEKO LA WAHAMIAJI
Global News

UMOJA wa Ulaya umesema uko tayari kuisaida Hungary kulishughulikia ongezeko la wahamiaji wanaovuka mipaka yake. Umoja huo umesema utaipa nchi hiyo kile kinachoitwa kuwa ni hadhi ya ‘eneo hatari la uhamiaji’, ikiwa na maana kuwa nchi hiyo ipewe raslimali za ziada kupambana na hali hiyo. Hayo yanajiri baada ya serikali ya Hungary kusema kuwa zaidi ya wakimbizi 2,000 waliingia nchini humo hapo jana wiki hii pekee nakuifanya nchi hiyo ikabiliwe na changamoto ya kuwasili nchini humo raia wa nchi jirani...

Like
177
0
Wednesday, 26 August 2015
WATOTO 10 WAUAWA KATIKA MLIPUKO AFGHANISTAN
Global News

IMEELEZWA kuwa Mlipuko mkubwa uliotokea nje ya kituo cha kusambazia gesi katika mji wa Herat nchini Afghanistan, umesababisha vifo vya watoto kumi na mtu na kumjeruhi mmoja. Msemaji wa hospitali mojawapo karibu na eneo hilo amesema kwamba watu wengine 18 wamejeruhiwa katika eneo palipotokea mlipuko ambalo hutumika kama kambi ya wakimbizi. Sanjari na hayo baadhi ya picha katika mitandao ya kijamii bado zinaonesha uwepo wa miale ya moto angani ingawa haijabainika iwapo mlipuko huo ulikuwa ajali au shambulizi....

Like
192
0
Tuesday, 25 August 2015
MABAKI YA WATU 40 YAZIKWA SOMALILAND
Global News

SHUGHULI ya kuzika mabaki ya zaidi ya watu arobaini imefanyika katika eneo lililojitangazia uhuru la Somaliland ambapo Mabaki hayo yalipatikana katika kaburi moja. Taarifa zinasema kuwa Mifupa hiyo ya watu ilipatikana wakati mitaro ya mabomba ya maji ilipokuwa ikichimbwa katika mji mkuu Hargeisa. Hata hivyo bado inaaminika kwamba watu hao waliuawa wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyotokea mwaka...

Like
205
0
Tuesday, 25 August 2015
KOREA KUPUNGUZA HALI YA WASIWASI MPAKANI
Global News

NCHI za Korea kaskazini na Kusini zimefikia makubaliano ya kupunguza hali ya wasiwasi iliyopo mpakani mwa nchi hizo mbili. Hatua hiyo imefikiwa baada ya mazungumzo ya muda mrefu ambapo nchi zote mbili ziliweka vikosi vyake vya ulinzi kama tahadhari baada ya mapigano ya muda mfupi yaliyotokea wiki iliyopita. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na pande hizo mbili, Korea kusini imekubali kuacha kueneza habari zenye propaganda zinazochochea pande hizo, huku Korea kaskazini ikielezea masikitiko yake juu ya tukio la hivi karibuni...

Like
202
0
Tuesday, 25 August 2015
MACEDONIA KUFUNGUA MIPAKA KWA WAHAMIAJI
Global News

MAELFU ya wahamiaji, wengi wao wakimbizi wa Syria, wamesafiri kupitia Macedonia na Serbia wakielekea Ulaya Magharibi. Shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia wakimbizi UNHCR limesema zaidi ya watu  elfu 7,000 wakiwemo wanaume, wanawake na watoto, walivuka mpaka na kuingia kusini mwa Serbia na Macedonia usiku wa kumkia jana Jumapili, huku wengi wakitarajiwa kuwasili. Shirika hilo limesema jana limehakikishiwa na serikali ya Macedonia kwamba mipaka itakuwa wazi kwa wakimbizi wanaokimbia mizozo katika nchi...

Like
228
0
Monday, 24 August 2015
BOKO HARAM YASHAMBULIA MSAFARA WA MNADHIMU MKUU WA JESHI NIGERIA
Global News

KATIBU MKUU wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon anaendelea na ziara yake ya siku mbili nchini Nigeria. Ki Moon aliwasili jana mjini Abuja saa chache baada ya jeshi kutangaza wapiganaji wa kundi la Boko Haram walikuwa wameushambulia msafara wa mnadhimu mkuu wa jeshi la nchi hiyo Luteni Kanali Tukur Buratai. Buratai ambaye hakudhurika, alikuwa akiwatembelea wanajeshi Jumamosi wakati wanamgambo walipokishambulia kijiji cha Falijari,  kilometa 40 mashariki ya mji mkuu wa jimbo la Borno,...

Like
238
0
Monday, 24 August 2015