KATIBU mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon amewasili jana nchini Nigeria tayari kwa kuanza ziara ya siku mbili nchini humo. Katika ziara hiyo Ban ki-moon anaitembelea Nigeria kwa lengo la kuwatembelea waathirika wa mashambulizi yaliyofanywa katika ofisi za umoja huo mjini Abuja yanayodaiwa kufanywa na wanamgambo wa Boko Haram miaka minne iliyopita. Ban Ki Moon pia atakutana na Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ili kujadili namna ya kupambana na vikundi vyenye msimamo mkali ambapo pia anatarajiwa kuwa na mazungumzo...
WAOKOAJI Kaskazini mwa Ufilipino wameendelea na kazi ya kuchimbua ardhini kwa lengo la kutafuta mamia ya wachimba madini waliofukiwa baada ya kukumbwa na kimbunga. Hali hiyo imekuja kufuatia zaidi ya watu kumi na tano kuripotiwa kufariki dunia na wengine kadhaa hawajulikani walipo kutokana na kimbunga hicho kikubwa. Hata hivyo mmomonyoko wa udongo ulisababishwa na kimbunga ambacho kilifukia migodi mitatu kaskazini mwa kisiwa cha Luzon ambapo kwa sasa kimepungua kasi na kinaelekea Japan katika kisiwa cha...
KIONGOZI wa Korea kaskazini Kim Jong-Un ameamuru majeshi yaliyoko mstari wa mbele kuwa tayari kwa vita leo, wakati hali ya wasi wasi ya kijeshi na Korea kusini ikiongezeka. Hali hiyo inafuatia mashambulizi ya makombora toka kila upande katika eneo lenye silaha nzito la mpakani. Shirika rasmi la habari la Korea kaskazini KCNA limesema hatua hiyo imekuja wakati wa mkutano wa dharura uliofanyika jana usiku wa kamisheni kuu yenye madaraka makubwa ya kijeshi...
WAZIRI MKUU wa Ugiriki Alexis Tsipras amejiuzulu na kuitisha uchaguzi ufanyike mapema. Hatua hiyo inaonekana kuwa juhudi za kuzima uasi ndani ya chama chake cha Syriza na kuimarisha uungwaji wake mkono wa mpango wa tatu wa uokozi wa uchumi wa nchi hiyo inayokabiliwa na madeni, ikiwa ni hatua ya kwanza ambayo imeidhinishwa na mawaziri wa fedha wa mataifa ya kanda ya euro wiki hii....
MAAFISA kutoka Ufaransa na Uingereza wamesaini makubaliano ya kuimarisha ushirikiano wa usalama katika kivuko kimoja muhimu cha mpakani, huku wakitangaza hatua zikiwemo teknolojia ya kisasa ili kuwadhibiti wahamiaji na waomba hifadhi wanaojaribu kuingia Uingereza. Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Bernard Cazeneuve na mwenzake wa Uingereza Theresa May, wamesaini makubaliano ya muafaka jana katika mji wa bandari wa Calais, ambako mamia ya watu wamejaribu kuvuka mpaka na kuingia Uingereza kutokea Ulaya katika kipindi cha mwaka huu...
WAENDESHA mashtaka nchini Brazil wamefungua mashtaka ya rushwa na usafishaji wa fedha chafu dhidi ya spika wa congress, Eduardo Cunha. Cunha anatuhumiwa kupokea dola milioni tano kama rushwa ili kuingia katika mikabata na shirika la mafuta la serikali, Petrobras. Bwana Cunha amekana tuhuma hizo na kusema zina ushawishi wa...
BOMU kubwa limelipuka karibu na makao makuu ya usalama kaskazini mwa mji mkuu wa Misri, Cairo ambako watu 29 walijeruhiwa akiwemo maafisa sita wa polisi. Eneo hilo kwa sasa limefungwa na kuna maafisa wengi wa polisi katika barabara za mji huo. Kundi la wapiganaji wa Islamic State limekiri kutekeleza shambulizi...
RAIS wa Burundi Pierre Nkurunziza anaapishwa kwa muhula wa tatu uliozua utata katika sherehe ambayo inadaiwa kuwa imefanyika kwa mshangao mkubwa kwa kuwa rais huyo alitarajiwa kuapishwa wiki ijayo. Hata hivyo hakuna kiongozi wa taifa lolote aliyehudhuria sherehe za kuapishwa kwake huku Afrika kusini ikishirikishwa na waziri mmoja kwa mujibu wa shirika AFP. Mataifa kadhaa yakiwemo yale ya China na Urusi yalituma mabalozi wao....
WAHAMIAJI wengi zaidi wanaendelea kuwasili nchini Bulgaria licha ya kuongeza ulinzi katika mipaka yake, kuweka kamera na vifaa vitakavyotambua nyendo za watu na kurefusha uzio wa usalama wenye urefu wa kilometa 160 ambao umejengwa kwenye mpaka wake na Uturuki. Data rasmi zinaonyesha kuwa kiasi cha watu elfu 25,000 wamejiandikisha kama wakimbizi nchini Bulgaria katika miaka miwili iliyopita, hiyo ikiwa ni idadi na ile iliyoandikishwa katika muda wa miongo miwili iliyopita....
UTAFITI umeeleza kuwa Watu wanaofanya kazi kwa saa nyingi wako hatarini kupata kiharusi,utafiti huo ulifanywa kwa zaidi ya watu laki tano. Takwimu zilizochapishwa kwenye jarida la kitabibu, Lancet, linaonyesha upo uwezekano wa ongezeko la hatari ya ugonjwa huo kwa watu wanaofanya kazi zaidi ya muda wa kawaida. Wataalam wanasema watu wanaofanya kazi kwa saa nyingi zaidi wawe na utaratibu wa kupima kiwango cha msukumo wa damu na kwamba kufanya kazi kwa muda mrefu zaidi kuliko kawaida na kukaa kwa...
BUNGE la Ujerumani limeanza kujadili kuhusu maamuzi ya mwisho ya kulipwa kwa deni la Ugiriki wakati ambapo kansela Angela Merkel anakabiliana na changamoto ya upande wa upinzani na wale wa chama chake kujadili juu ya deni la dola bilioni tisini na nne. Mambo ambayo yalipewa kipaumbele na wabunge wa upinzani ni kuhusiana na deni la ugiriki kulipwa na Ujerumani huku kukiwa na wasiwasi juu ya maamuzi ya shirika la fedha duniani IFM, kutoshiriki katika kulilipa deni hilo. Waziri wa fedha...