Global News

REDIO YAFUNGIWA SUDANI KUSINI
Global News

VIKOSI vya Usalama nchini Sudani Kusini vimefunga kituo cha redio iliyokuwa ikiunga mkono mpango wa kumaliza mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yanayoendelea nchini humo. Mamlaka ya nchi hiyo, imekilazimisha kituo cha radio cha Free Voice South Sudan kinachoungwa mkono na Marekani kutorusha matangazo yake siku ya jana, siku moja tu baada ya kulifungia gazeti la The Citizen. Wapatanishi wa kimataifa wamewapa rais Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar mpaka katikati ya mwezi Agosti kusaini makubaliano ya amani....

Like
235
0
Wednesday, 05 August 2015
TRENI MBILI ZAKOSEA NJIA NA KUTUMBUKIA MTONI INDIA
Global News

TRENI mbili zimekosea njia huko nchini India na kutumbukia katika mto uliokuwa umefurika kufuatia mvua kubwa katika Jimbo la Madhya Pradesh. Shirika la habari la Associated Press limemnunukuu mmoja wa waokoaji akisema kuwa wamehesabu maiti 20 na  kwamba zaidi ya abiria 250 wameokolewa, baada ya mabehewa sita kutumbukia katika mto huo. Wakuu wa shirika la Reli la India wanasema ajali hiyo ilitokea usiku wa manane kuamkia leo jumatano....

Like
201
0
Wednesday, 05 August 2015
MWANAHARAKATI APIGWA RISASI BURUNDI
Global News

MWANAHARAKATI maarufu wa haki za kibinaadamu nchini Burundi amepigwa risasi na kujeruhiwa vibaya na watu waliokuwa katika pikipiki. Pierre Claver Mbonimpa alishambuliwa katika mji mkuu wa Burundi Bujumbura ambapo pia kwa kipindi kirefu amekuwa mkosoaji mkubwa wa mchakato wa rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu. Siku ya jumapili mshauri wa rais huyo jenerali Adolphe Nshimirimana aliuawa katika shambulizi ndani ya gari lake Mjini Bujumbura wakati akisimamia usalama wa rais....

Like
195
0
Tuesday, 04 August 2015
YEMEN: KAMBI KUBWA YA WAASI WA HOUTHI YASAMBARATISHWA
Global News

IMEBAINIKA kwamba vikosi vinavyounga mkono serikali nchini Yemen vimechukua kambi kubwa ya wanaanga katika makabiliano na waasi wa Houthi. Uharibifu mkubwa pamoja na majeraha yameripotiwa katika kambi ya jeshi ya Al-Anad kaskazini mwa mji wa Aden baada ya mapigano makali yaliofanyika katika siku za hivi karibuni. Hatua hiyo imekuja baada ya vikosi vinavyoiunga mkono serikali vikisaidiwa na mshambulizi ya angani ya muungano unaoongozwa na Saudia kuchukua mji wa Aden mwezi...

Like
201
0
Tuesday, 04 August 2015
IKULU YA URUSI YAISHUTUMU MAREKANI KUVURUGA AMANI SYRIA
Global News

IKULU ya Urusi Kremlin, inasema hujuma za ndege za kivita za Marekani dhidi ya vikosi vya serikali ya Syria zinaweza kuvuruga zaidi utulivu nchini humo na kuwafaidisha wanamgambo wa itikadi kali wa Dola ya Kiislam – IS. Matamshi hayo ya Urusi yametolewa kufuatia ripoti iliyotolewa na gazeti mojawapo nchini humo inayosema serikali ya Marekani mjini Washington inapanga kutumia ndege za kivita kufanya hujuma nchini Syria ili kuwasaidia makuruti wanaopambana dhidi ya Dola la Kiislam. Hata hivyo amebainisha kuwa hujuma kama...

Like
332
0
Tuesday, 04 August 2015
OBAMA AZINDUA HATUA MUHIMU KUPAMBANA NA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI
Global News

RAIS wa Marekani Barack Obama amezindua kile alichokiita hatua muhimu zaidi ya kupambana na mabadiliko ya tabia nchi. Katika uzinduzi huo Rais Obama amesema kizazi hiki ni cha mwisho chenye kushughulikia suala hilo na kwamba imeilazimu Marekani kuchukua hatua madhubuti za kutokomeza visababishi vya mabadiliko ya tabia nchi. Obama amesisitiza hatua kali kuchukuliwa haraka kupunguza gesi ya ukaa inayotoka katika viwanda vilivyopo nchini humo kwa theluthi moja ifikiapo mwaka...

Like
204
0
Tuesday, 04 August 2015
JESHI LA NIGERIA LAWAOKOA WATU 180
Global News

JESHI la Nigeria linasema kuwa limewaokoa zaidi ya watu 180, wengi wao wanawake na watoto, kutoka kwa kundi hatari la wapiganaji wa kiislamu la Boko Haram, katika jimbo la Borno. Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, msemaji moja wa jeshi amesema kuwa kambi kadhaa za waasi hao zilizoko karibu na mji wa Maiduguri zimeharibiwa na kamanda mmoja wa Boko Haram kukamatwa, lakini duru hizo hazijasema ni lini tukio hilo lilifanyika. Wakati hio huo, Rais wa Niger, Mahmadou Issoufou, amesema kuwa...

Like
165
0
Monday, 03 August 2015
NKURUNZIZA AOMBA UTULIVU BURUNDI
Global News

RAIS wa Burundi Pierre Nkurunziza ameomba utulivu baada ya wapiganaji waliovalia magwanda ya kijeshi kumuua mmoja wa majenerali walio na ushawishi mkubwa serikalini, Adolphe Nshimirimana  .   Katika hotuba aliyoitoa leo mchana baada ya shambulio hilo, Nkurunziza ameomba utulivu akisema kuwa kitendo cha kulipiza kisasi kitamaliza kizazi chote.  ...

Like
179
0
Monday, 03 August 2015
MALAYSIA YATOA WITO KUTOLEWA KWA TAARIFA JUU YA MABAKI YA NDEGE
Global News

MAAFISA nchini Malaysia wametoa wito kwa nchi zilizo karibu na kisiwa cha Reunion katika Bahari ya Hindi kusaidia kutoa habari zozote kuhusu mabaki ambayo huenda yanahusiana na ndege iliyotoweka ya Malaysia. Wito huo umekuja baada ya kipande cha ubawa kupatikana katika kisiwa hicho magharibi mwa Bahari ya Hindi. Kipande kipya cha mabaki kilichopatikana jana Jumapili katika kisiwa hicho kiligunduliwa kuwa ni ngazi ya kawaida ya nyumbani na wala hakihusiani na ndege hiyo ya Malaysia iliyotoweka mwaka mmoja...

Like
199
0
Monday, 03 August 2015
HALI YA WASIWASI YAANZA KUTANDA BURUNDI
Global News

KUMERIPOTIWA kuwepo kwa hali ya wasiwasi nchini Burundi kufuatia mauaji ya Jenerali mmoja ambaye alikuwa mtu wa karibu ya Rais Pierre Nkurunzinza katika masuala ya kiusalama. Jenerali Adolphe Nshimirimana aliuawa jana kwa kupigwa risasi akiwa ndani ya gari katika mji mkuu Bujumbura. Nshimirimana ambaye alikuwa mshauri mwandamizi wa masuala ya usalama wa Rais Pierre Nkurunzinza aliuawa wakati watu waliokuwa ndani ya gari walipomfyatulia risasi yeye na mlinzi wake katika kitongoji cha mji mkuu cha...

Like
230
0
Monday, 03 August 2015
UGANDA: MBABAZI KUWANIA URAIS NJE YA CHAMA TAWALA CHA NRM
Global News

WAZIRI  mkuu wa zamani wa Uganda John Patrick Amama Mbabazi ametangaza kuwa hatawania urais kwa chama tawala NRM katika uchaguzi mkuu mwakani. Mbabazi ametangaza hilo leo mchana akiwa nyumbani kwake Kololo katika siku ya mwisho ya kurejesha fomu za uwaniaji wadhfa katika chama hicho tawala. Tangazo hilo la Mbabazi limetokea baada ya rais Yoweri Museveni kutangaza kuwa atarejesha fomu zake za kuwania uwenyekiti wa chama tawala NRM leo....

Like
242
0
Friday, 31 July 2015