Global News

Mtoto mchanga wa siku 6 apona Ebola
Global News

Mtoto wa kike ambaye ilithibitishwa kuwa ana Ebola akiwa na siku sita pekee amepona, maafisa afya huko Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wamethibitisha. Mama yake na mtoto Benedicte alikuwa ameambukizwa ugonjwa wa Ebola na alifariki wakati anajifungua. Benedicte alianza kuonesha dalili siku chache baada ya kuzaliwa na madaktari walikuwa na wiki tano tu kumtibia na kuhakikisha anakuwa hai Baba na shangazi yake walimpeleka nyumbani siku ya Jumatano wiki iliyopita. “Baba yake, Thomas, alikuwa na hisia kali… ndio mtoto wangu...

Like
1168
0
Tuesday, 18 December 2018
Marekani yamzuia mama raia wa Yemen kumuona mtoto wake aliye karibu kufa
Global News

Mama wa mtoto aliye raia wa Yemeni amezuiwa kumuona kijana wake aliye karibu kuaga dunia kutokana na sheria ya kuwazuia wageni kutoka nchini mwake, familia imeeleza. Mtoto Abdullah Hassan alizaliwa na maradhi ya ubongo ambapo madaktari walisema hataweza kuishi. Ndugu wanasema mama yake anataka kumuona kwa mara ya mwisho kabla ya kuondoa mashine ya kumsaidia kupumua. Baba yake anasema mama wa Abdullah hawezi kwenda nchini Marekani kutokana na marufuku iliyowekwa na utawala wa Trump. Abdullah na Baba yake ni raia...

Like
544
0
Tuesday, 18 December 2018
Je wajua waweza kujifunza kitu chochote kwa saa 20 tu?
Global News

Iwe Kirusi, Kiarabu ama Kichina, au hata fizikia ya maumbo. Ubongo wa binaadamu unaweza kujifunza kitu chochote kile, hata kiwe kigumu namna gani, tena kwa haraka. Utafiti unaonesha kuwa muda bora kabisa wa kujifunza kitu ni saa 20 za awali unapokutana na somo ama ujuzi mpya. Wakati huo ndio kasi ya ubongo kupata uelewa ni kubwa zaidi. Kutokana na hamu ya kung’amua mapya, uwezo wa ubongo kufahamu nao huwa mkubwa. Mwanafalsafa wa karne ya 19 nchini Ujerumani Herman Ebbinghaus ambaye...

Like
657
0
Monday, 17 December 2018
Vladimir Putin ataka muziki wa rap udhibitiwe
Global News

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameitaka serikali yake “kuchukua uongozi” wa muziki wa kufoka foka ama rap. Japo matamasha kadhaa ya muziki huo yamezuiwa katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo katika siku za hivi karibuni, jitihada za serikali kuupiga marufuku kabisa zimegonga mwamba. Sababu marufuku ya serikali imeshindikana, Putin anataka mamlaka zifanye kazi ya ziada kuudhibiti. “Wizara ya Utamaduni itatafuta namna bora ya kusimamia matamasha ya vijana,” amesema Putin. Kauli ya Putin inakuja siku chache baada mwanamuziki...

Like
596
0
Monday, 17 December 2018
Moyo wasahaulika ndani ya ndege
Global News

Ndege ya abiria ya Marekani iliyokuwa ikisafiri kutoka mji wa Seattle kuenda Dallas ililazimika kukatiza safari baada ya moyo wa binadamu kusahaulika ndani yake. Shirika la ndege la Southwest linasema kuwa kiungo hicho kilisafirishwa Seattle kutoka California, ambako ilitarajiwa kutolewa mishipa ambayo ingetumiwa baadaye kwa utaratibu wa tiba ya upandikizaji. Lakini kisanduku ambacho kilikuwa kimehifadhi moyo huo kilisahaulika ndani ya ndege hiyo na hilo lilifahamika baada ya ndege kuanza safari kuelekea Dallas. Kisa hicho kilitokea siku ya...

Like
820
0
Friday, 14 December 2018
Kijana wa Kimaasai afunga ndoa na wanawake wawili wakati mmoja
Global News

Morani mmoja katika kaunti ya Kajiado nchini Kenya ameacha watu midomo wazi baada ya kufunga ndoa na wanawake wawili kwa mpigo. Tom Mako, maarufu kama Junior, 27, alifanya sherehe hiyo ya harusi Jumanne wiki hii. Mako anatokea kwenye familia ambayo ndo za wake wengi ama mitala ni jambo la kawaida. Hata hivyo kuoa wake wawili kwa mpigo ni jambo ambalo halikuwahi kusikika katika jamii ya Kimaasai ambayo wanandoa hao wametokea. Wapo wanaume wanaowaoa wake wengi lakini si kwa wakati mmoja....

1
1454
0
Friday, 14 December 2018
Binti wa miaka 7 amburuza baba yake mzazi polisi
Global News

Binti wa miaka saba nchini India amemshitaki baba yake polisi baada ya kushindwa kutekeleza ahadi aliyomuahidi. Hanifa Zaara amewaambia polisi kuwa baba yake “amemdanganya” na anatakiwa akamatwe na kushtakiwa. Ahadi yenyewe ni ya kujengewa choo, binti huyo amesema anaona aibu kwenda haja vichakani kwa kukosa choo. Wahindi wengi hawana vyoo na takribani watu milioni 500 huenda haja nje, kwa mujibu wa shirika la Unicef. Hata kwa baadhi ya wenye vyoo, hawavitumii na badala yake kujisaidia nje. Hanifa amabaye anaishi na...

Like
617
0
Thursday, 13 December 2018
Ndege za kuangusha mabomu za Urusi zaikera Marekani
Global News

Maafisa wakuu wa Urusi na Marekani wamejibizana baada ya ndege mbili kubwa za kuangusha mabomu za Urusi kutua nchini Venezuela, taifa linalopatikana Amerika Kusini. Ndege hizo mbili zina uwezo wa kubeba silaha za nyuklia. Ndege hizo za kivita aina ya Tu-160 zilitua Venezuela Jumatatu katika kile kinachoonekana kama jaribio la kuonyesha uungaji mkono wa Urusi kwa rais wa Kisoshialisti wa Venezuela Nicolás Maduro ambaye amekuwa akikabiliwa na shinikizo. Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo amesema kitendo hicho...

Like
1285
0
Wednesday, 12 December 2018
Je Museveni atafanikiwa kupambana na ‘pepo la rushwa’ Uganda?
Global News

Rais Yoweri Museveni wa Uganda amezindua kitengo kipya cha kupambana na rushwa na Ufisadi nchini Uganda na hasa katika idara zote za Serikali kuchunguza tatizo la rushwa. Rais Museveni ameeleza kuwa jukumu la kupambana na rushwa liko kwa wananchi, ambao amewataka kuwasiliana na kitengo hicho kipya kitakachohudumu moja kwa moja chini ya ofisi yake. Kiongozi huyo yupo katika shinikizo kuonyesha uwajibikaji wa serikali yake, wakati anakabiliwa na changamoto na upinzani kutoka kwa wanasiasa wanaowavutia wapiga kura vijana – kama mwanamuziki...

1
655
0
Tuesday, 11 December 2018
Afrika Kusini imeghadhabishwa na mtandao wa Rwanda uliomuita waziri wake “kahaba”
Global News

Afrika Kusini imemuita balozi wa Rwanda mjini Pretoria baada ya mtandao unaoipendelea serikali nchini Rwanda kumita “kahaba” waziri mmoja wa serikali ya Afrika Kusini. Lindiwe Sisulu, waziri wa masuala ya uhusiano wa kimataifa nchini Afrika Kusini amekosolewa kwenye Twitter na afisa wa cheo cha juu wa Rwanda. Msemaji wake aliiambia BBC kuwa matamshi hayo hayatakubaliwa na lazima yakome. Bi Sisulu hivi majuzi alikutana na mtoro na mkosoaji wa Rais wa Rwanda, na kuzua mzozo wa kidiplomasia kati ya nchi hizo...

Like
662
0
Tuesday, 11 December 2018
Kabila haondoi uwezekano wa kugombea tena urais baadaye
Global News

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo anayeondoka madarakani Joseph Kabila amesema haondoi uwezekano wa kugombea tena urais mwaka 2023 Katika mazungumzo ya nadra na vyombo vya habari, Rais Joseph Kabila ameliambia shirika la Associated Press (AP) kwamba anatarajia kuendelea kutoa mchango katika kushughulikia matatizo yanayoikumba Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hata baada ya uchaguzi wa Desemba 23 ambao utaamua mrithi wake. Kabila ameiambia AP kwamba amejitahidi ”kadri ya uwezo wetu” kwa maslahi mema ya Congo tangu alipoingia...

Like
533
0
Monday, 10 December 2018