KIONGOZI wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis yuko nchini Equador ambako alilakiwa na maelfu ya watu waliojitokeza barabarani jana jioni. Baba Mtakatifu Francis anatarajiwa kutoa hotuba 22 wakati wa ziara yake ya siku nane ambayo pia itamfikisha Bolivia na Paraguay. Mataifa hayo matatu ni miongoni mwa mataifa maskini kabisa katika bara la Amerika ya Kusini na Papa Francis mwenye umri wa miaka 78 mzaliwa wa Argentina, amesema ataangazia mahitaji ya watoto, wazee, wagonjwa na...
MRENGO wa vijana kutoka chama tawala cha Afrika Kusini-ANC– Youth League umesema unapanga kufanya sherehe ya tohara ya kitamaduni kwenye milima maalum iliyopo nchini humo. Shirika la Turathi la Umoja wa Mataifa-UNESCO– limetangaza eneo hilo la “Table Mountains” kuwa turathi kwa sababu kuna mimea ya kipekee zaidi ya aina elfu tano. Taarifa ya vijana hao wa –ANC– katika jimbo la Western Cape imesema hakuna ardhi ya kufanyiwa tohara ya utamaduni ingawa bado haijabainika ikiwa watapata idhini ya kuendesha...
WATU 29 wamefariki kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa kipundupindu nchini Sudan Kusini huku wengine elfu moja wakiwa katika hatari ya kuambukizwa ugonjwa huo. Takriban visa 484 vya ugonjwa huo ikiwemo vifo 29 ambavyo sita kati yake ni vya watoto wa chini ya umri wa miaka mitano idadi iliyoripotiwa mwishoni mwa mwezi Juni kutoka ofisi ya mratibu wa masuala ya kibinaadamu katika umoja wa kimataifa. Kwa mujibu wa ripoti hiyo watoto elfu tano walio chini ya umri wa miaka mitano...
JUMLA ya watu wanne wamefariki dunia wakiwa na dalili za ugonjwa wa Ebola huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Mbali na kutokea kwa taarifa za mgonjwa huyo wa Ebola Mamlaka za Afya nchini humo zimesema kuwa bado zinachunguza uwezekano wa kutokea zaidi kwa mlipuko wa ugonjwa huo. Waziri wa Afya Felix Kabange amesema wafanyakazi wa afya wamepelekwa katika kijiji cha Masambio kilichoko kilomita 270 kaskazini mwa mji mkuu wa nchi hiyo Kinshasa, kwa ajili ya uchunguzi zaidi ambapo wawindaji sita...
IMEELEZWA kwamba jumla ya Watu 150 wameuawa baada ya kundi la Boko Haram kuvamia na kufanya mashambulizi katika eneo la kaskazini mashariki mwa nchi ya Nigeria. Taarifa kutoka kwa mashuhuda wa mashambulizi hayo zinasema kuwa watu tisini na saba wameuawa katika kijiji cha Kukawa kilichopo karibu na Ziwa Chad kutokana na mashambulizi hayo. Hata hivyo baadhi ya Mashuhuda wanaokimbia eneo lililopo karibu na Ziwa Chad wamesema idadi kubwa ya wapiganaji wamevamia vijiji vitatu ambapo wamewaua wanaume, wanawake na...
RAIS wa Kenya Uhuru Kenyatta amechaguliwa na muungano wa wanafunzi wa Vyuo vikuu barani Afrika- AASU kama rais bora barani Afrika mwaka huu. Muungano huo unasema kuwa maelfu ya wanafunzi kutoka kote barani walishiriki katika kura hiyo. Kenyatta alichaguliwa kwa uwezo wake wa kujenga makubaliano kitaifa na kimataifa, juhudi zake za kubadilisha sera na kutoa ufumbuzi katika maswala yanayowaathiri wakenya. Rais wa Rwanda Paul Kagame alishinda tuzo kama hiyo mwaka...
WAZIRI MKUU wa Ugiriki Alexis Tsipras amesisitiza kura ya maoni aliyoitisha siku ya Jumapili wiki hii itaamua hatma ya mgogoro wa kiuchumi unaoikumba nchi yake. Mawaziri wa fedha wa kanda inayotumia sarafu ya euro waliokutana hapo jana wamesema hawatafanya mkutano mwingine wa kuzingatia maombi yoyote mapya ya kuipa nchi hiyo mkopo wa uokozi hadi kura hiyo ya maoni itakapofanyika. Tsipras amesema kura ya kupinga masharti magumu ya wakopeshaji wa Ugiriki haimaniishi nchi hiyo inajiondoa kutoka Umoja wa Ulaya bali ni...
BARAZA la usalama la Umoja wa Mataifa limeamua kuwawekea vikwazo majenerali sita wa kijeshi nchini Sudan Kusini wanaotuhumiwa kuchochea vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimedumu kwa miezi kumi na nane sasa. Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Samantha Power amesema uamuzi wa baraza hilo la usalama unadhihirisha kuwa wale wanaohusika na ukiukaji wa haki za binadamu na kuhujumu juhudi za kupatikana amani watakabiliwa na sheria. Majenerali hao sita waliowekewa vikwazo wamepigwa marufuku kusafiri na mali zao...
MAKUNDI ya wapiganaji yamefanya mashambulizi dhidi ya maafisa wa usalama nchini Misri katika Rasi ya Sinai. Jeshi limesema makabiliano yanaendelea huku wanajeshi kadhaa na wapiganaji wakiuawa.Taarifa ya jeshi imesema vizuizi vitano vya polisi vililengwa sawa na kituo kimoja cha polisi. Hili ndilo shambulio kubwa zaidi kufanywa na wapiganaji wa kiisilamu walioko eneo la Sinai, miaka miwili baada ya kuondolewa madarakani kwa Rais aliyeegemea mrengo wa kidini Mohamed Morsi....
INDONESIA imasema kuwa idadi ya watu waliofariki huko Medan katika ajali ya ndege ya kijeshi imepanda na kufikia watu 141. Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi la wana anga nchini humo hakuna yeyote aliyenusurika kifo miongoni mwa watu 122 waliokuwa ndani ya ndege hiyo ya mizigo. Jeshi limesema kuwa limeanzisha uchunguzi kubaini haswa ni akinani waliokuwa ndani ya ndege hiyo ya kijeshi baada ya uvumi kuenea kuwa ndege hiyo ilikuwa imewabeba abiria waliokuwa wamelipa nauli. ...
Zaid ya watu 140 wanahofiwa kufariki dunia kufuatia ajali ya ndege ya Kijeshi kuanguka katika makazi ya watu muda mfupi baada ya kupaa. Kaskazini mwa Indonesia . polisi na timu ya Taifa ya uokozi wanaendelea kuwatafuta waathirika wengine kwenye eneo hilo la tukio katika mji wa...