Global News

WACHINA 15 MBARONI KWA KUGUSHI
Global News

RAIA 15 wa China wamefunguliwa mashitaka nchini Marekani kwa tuhuma za udanganyifu wa matokeo na nyaraka za kitaaluma walizozitumia kujiunga na elimu ya juu nchini Marekani. Kwa mjibu wa waendesha mashtaka nchini humo,wamebaini kuwa vijana hao wa China wamefanya udanganyifu wa kutumia simu wakati wa majaribio ya kujiunga na vyuo hivyo. Iwapo watakutwa na hatia kutokana na tuhuma hizo,raia hao wa China watafungwa hadi miaka 20 jela....

Like
155
0
Friday, 29 May 2015
IDADI YA WATU WANAOSUMBULIWA NA NJAA DUNIANI YAPUNGUA
Global News

IDADI ya watu wanaosumbuliwa na njaa ulimwenguni imepungua na kufikia chini ya watu milioni 800-kwa mara ya kwanza tangu Umoja wa mataifa ulipoanza kutoa takwimu hizo. Hii ni kwa mujibu wa shirika la Umoja wa mataifa la Chakula na Kilimo-FAO ambalo limesema katika ripoti yake ya mwaka iliyochapishwa jana. Shirika hilo lenye makao yake mjini Rome Italy limesema kuna watu milioni 795 ulimwenguni wanaosumbuliwa na njaa-idadi hiyo ikiwa na upungufu wa watu milioni 216 ikilinganishwa na jinsi  hali namna ilivyokuwa...

Like
208
0
Thursday, 28 May 2015
TONY BLAIR AJIUZULU NAFASI YA UJUMBE KATIKA KAMATI YA USULUHISHI WA MGOGORO WA MASHARIKI YA KATI
Global News

WAZIRI MKUU wa zamani wa Uingereza Tony Blair amejiuzulu nafasi ya ujumbe wa umoja wa kimataifa katika kamati inayoshughulikia usuluhishi wa mgogoro wa Mashariki ya kati, unaohusisha nchi ya Israel na Palestina nafasi ambayo ameitumikia kwa kipindi cha miaka nane. Vyanzo vya habari vilivyokaribu na Blair vinasema ataendelea kuwepo akijihusisha na baadhi ya shughuli katika eneo hilo. Afisa mmoja wa Palestina amemlaumu Blair kwa kufanya kazi ili kuwaridhisha waisrael na Marekani. Umoja huo unaundwa na UN, EU nchi ya Marekani...

Like
258
0
Thursday, 28 May 2015
UINGEREZA YATAKA KUBADILISHIWA MASHARTI YA KUWA MWANACHAMA WA UMOJA WA ULAYA
Global News

WAZIRI MKUU wa Uingereza David Cameron amependekeza mbele ya mwenyekiti wa Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Jean Claude Juncker, masharti ya nchi yake kuwa mwanachama wa Umoja huo, yabadilishwe. Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika katika makazi ya waziri mkuu huko Chequers, David Cameron ameweka wazi kabisa Waingereza hawakubaliani na hali namna ilivyo hivi sasa. Kwa mujibu wa msemaji wa waziri mkuu wa Uingereza, mkuu wa Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya ameahidi kusaidia kupatikana ufumbuzi wa haki kwa Uingereza....

Like
204
0
Wednesday, 27 May 2015
GAZA: MAJESHI YA HAMAS YALAUMIWA KWA UKATILI
Global News

SHIRIKA la kimataifa la kutetea haki za binaadamu la Amnesty International limelaumu majeshi ya Hamas huko Gaza kwa kuendesha vitendo vya kikatili na utekaji nyara, mateso na mauaji kwa raia wa kipalestina kufuatia mgogoro kati ya Israel na makundi ya wapiganaji wa Palestina katika maeneo ya mpakani. Mashambulizi hayo yaliwalenga raia wakiwatuhumu kwa kushirikiana na Israel. Amnesty imesema kwamba hali ni mbaya wakati vikosi vya askari wa Israel wakiwa katika harakati zao za mauaji ya kutisha na uharibifu kwa watu...

Like
232
0
Wednesday, 27 May 2015
POLISI WAPAMBANA NA AL SHABAAB KASKAZINI MASHARIKI MWA KENYA
Global News

ASKARI mmoja ameripotiwa kujeruhiwa baada ya kuwepo kwa mapambano makali kati ya Polisi na wanamgambo wa Al Shabaab Kaskazini Mashariki mwa nchi ya Kenya Wizara ya usalama wa Taifa nchini Kenya kupitia kwa msemaji wake MWENDA NJOKA imethibitisha kuwa askari mmoja amejeruhiwa wakati wa shambulizi la wanamgambo hao  katika kijiji cha Yumbis. Wakati huo huo AL SHABAAB wamekiri kuhusika katika shambulio hilo wakidai kuwa wamewaua Polisi 20 lakini vyombo vya usalama vimesema madai hayo sio ya...

Like
246
0
Tuesday, 26 May 2015
UTAFITI UNAONYESHA KUWA NA UZITO MKUBWA KATIKA UMRI MDOGO KUNAWEZA KUSABABISHA UGONJWA WA SARATANI YA UTUMBO
Global News

SHIRIKA la kimataifa la utafiti wa Saratani limebaini kuwa binadamu kuwa na uzito mkubwa katika umri mdogo kunaweza kusababisha ugonjwa wa saratani ya utumbo. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mtafiti wa masuala ya saratani kutoka shirika hilo la kimataifa RACHEL THOMSON zinasema kuwa uzito wa kupita kiasi unaweza kusababisha Kansa ya utumbo kwa kuwa kuna uhusiano wa karibu wa uzito mkubwa na ugonjwa huo. Uchambuzi uliochapishwa kwenye jarida moja unaonyesha kuwa vijana wadogo wapo hatarini mara mbili zaidi kupata...

Like
331
0
Tuesday, 26 May 2015
URUSI YAANZA MAZOEZI MAKALI YA KIJESHI
Global News

URUSI imeanza mazoezi makali ya kivita yanayojumuisha kikosi cha anga cha wanajeshi 150 pamoja na kikosi cha mashambulio ya mbali ya makombora. Wizara ya mambo ya ndani ya Urusi inasema kuwa wanajeshi elfu kumi na mbili wanatarajiwa kuhusishwa na mazoezi hayo makali ya siku nne yanayolenga kutaka kujua uimara wa jeshi hilo na utayari wake. Hata hivyo tukio hili la mazoezi ya majeshi hayo yanalenga nchi za magharibi kufuatia machafuko yanayoendelea Ukraine ambapo Urusi imekuwa ikinyooshewa kidole kutokana na machafuko...

Like
357
0
Tuesday, 26 May 2015
18 WAPOTEZA MAISHA KUTOKANA NA MAFURIKO TEXAS MAREKANI
Global News

JUMLA ya watu kumi na nane wamepoteza maisha kutokana na mafuriko makubwa yaliyotokea maeneo ya Magharibi mwa Marekani na Kaskazini mwa Mexco. Taarifa zaidi zinasema kuwa wengi wa waliothibitishwa kufariki dunia kutokana na mafuriko hayo ni kutoka mpakani mwa Mexco katika mji wa Acuna ambapo watu 3 wamefariki na wengine 12 hawajulikani walipo. Hata hivyo Gavana wa jimbo la Texas GREG ABBOTT amesema kuwa mafuriko hayo yameleta madhara makubwa katika jimbo lake hususani uharibifu wa makazi ya...

Like
224
0
Tuesday, 26 May 2015
BURKINA FASO: MWILI WA THOMAS SANKARA KUFUKULIWA
Global News

RIPOTI za mahakama nchini Burkina Faso zinasema kuwa mwili ambao unahisiwa kuwa wa raisi wa zamani aliyeuawa Thomas Sankara utafukuliwa hii leo katika jaribio la kutaka kubainisha ikiwa ni wake. Familia na marafiki wa rais Sankara wamekuwa na shauku iwapo mabaki hayo ni yake. Sankara ambaye aliuawa wakati wa mapinduzi mwaka 1987, alichukuwa uongozi baada ya mapinduzi ya mwaka wa 1983 na baadaye alipinduliwa na Blaise Compaore ambaye aliitawala Burkina Faso hadi mwaka uliopita alipolazimishwa kuondoka na maandamano makubwa katika...

Like
266
0
Monday, 25 May 2015
ETHIOPIA: CHAMA TAWALA KINATAZAMIWA KUSHINDA UCHAGUZI MKUU
Global News

UPIGAJI  kura umesogezwa hadi leo Jumatatu katika baadhi ya maeneo nchini Ethiopia, ili kuruhusu wanafunzi wa vyuo vikuu kushiriki katika uchaguzi mkuu ambao chama tawala kinatazamiwa kushinda kwa kishindo na kuendeleza utawala wake. Jana Jumapili, wapigakura wa upinzani walidai kuwepo na unyanyasaji na hata vurugu katika baadhi ya vituo vya kupigia kura. Karibu asilimia 80 ya wapigakura milioni 35 wa Ethiopia walijiandikisha kushiriki katika uchaguzi huo ambao wengi wanahisi matokoea yake tayari yanajulikana, katika taifa ambako chama tawala...

Like
257
0
Monday, 25 May 2015