WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Frank – Walter Steinmeier amewaalika Mawaziri wenzake kutoka Urusi, Ukraine na Ufaransa mjini Berlin siku ya Jumatatu kujadili utekelezaji wa makubaliano ya amani yaliyofikiwa mjini Minsk kuhusu mashariki mwa Ukraine, nchini Belarus Februari mwaka huu. Mzozo kati ya waasi wanaoungwa mkono na Urusi na Majeshi ya Serikali ya Ukraine mashariki mwa nchi hiyo umesababisha watu elfu sita kupoteza maisha. Viongozi wa ...
WAZIRI Mkuu wa Ugiriki, Alexis Tsipras, amewasili mjini Moscow kukutana rais wa Urusi Vladimir Putin kwa mazungumzo maalum. Ugiriki inasema kuwa mazungumzo yao yatajadili uhusiano kati ya muungano wa bara la Ulaya na Urusi. Uhusiano huo ulidorora kwa kiasi kikubwa katika siku za hivi karibuni kufuatia mzozo wa Ukraine. Wachanganuzi wanasema kuwa Ugiriki inapania kuboresha uhusiano na Moscow hasa ikiwa uhusiano wao na wadeni wao bara Ulaya wa kuikopesha pesa ukishindikana ambapo kesho nchi hiyo inatakiwa kulipa deni la dola...
UGANDA inasema imekamata watu kadhaa kuhusiana na mauaji ya mwendesha mashtaka Joan Kagezi yaliyotokea wiki iliyopita. Mwendesha mashtaka huyo aliuawa na watu waliokuwa na bunduki wakitumia pikipiki na polisi kuanza uchunguzi kuhusiana na mauaji hayo. Kutokana na matukio ya kigaidi katika nchi jirani ya Kenya, polisi Nchini Uganda wamekuwa wakichukua tahadhari dhidi ya matukio yoyote...
WAKUU katika jimbo la South Carolina nchini Marekani wamemhukumu Afisa mmoja wa polisi mweupe, kwa kosa la mauaji. Mtuhumiwa huyo anadaiwa kumpiga risasi raia mmoja mweusi na kumuuwa. Mkanda wa video unaonesha mtu mmoja, WALTER SCOTT, akipigwa risasi alipokuwa akimkimbia Afisa huyo. ...
WAKENYA wameandamana kudai usalama zaidi wa taifa hilo kufuatia mauaji ya wiki iliyopita yaliyofanywa na wapiganaji kutoka Somalia wa kundi la Al-Shabaab , kabla ya kuwasha mishumaa usiku katika siku ya mwisho ya Maombolezi kutokana na kuuwawa kwa watu 148 mjini Garissa. Ndege za kivita za Kenya zimeshambulia maeneo yanayodhibitiwa na kundi hilo lenye mafungamano na Al-Qaeda Kusini mwa Somalia , lakini hasira imekuwa ikiongezeka kuhusiana na ...
WAZIRI Mkuu wa zamani wa Uingereza,TONY BLAIR ameingia katika kampeni za uchaguzi kwa kumshambulia Waziri Mkuu DAVID CAMERON, kwa ahadi yake ya kufanyika kwa kura ya maoni kuhusu uanachama wa Uingereza katika Umoja wa Ulaya, EU. Bwana BLAIR amesema Bwana CAMERON ametoka nje ya agenda kwa kuahidi kufanyika kura ya maoni na kwamba kujiondoa katika Umoja wa Ulaya kunatishia nafasi ya Uingereza kama taifa kubwa duniani Bwana BLAIR anatarajiwa kusema kuwa kiongozi wa Chama chake cha LABOUR ED MILIBAND ameonyesha...
SHIRIKA la Afya Duniani limetoa takwimu zinazosaidia kuelewa wa mgogoro uliopo nchini Yemen. Shirika la WHO limesema Zaidi 500 wameuawa katika mapigano ya wiki za hivi karibuni, na kwamba watu wapatao elfu moja na mia saba wamejeruhiwa katika mapigano hayo. Waasi kama “Houthi” na washirika wao wanapambana na majeshi ya Rais ABD RABBU MANSOUR HADI ambaye anaungwa mkono na jeshi la linaloongozwa na Saudi...
RAIA wa Uholanzi ambaye aliyetekwa nyara miezi Minne iliyopita na mtandao wa kigaidi wa AQIM, huko Timbuktu Kaskazini mwa Mali amekombolewa leo katika operesheni za kijeshi za Ufaransa. Wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa imesema mateka SJAAK RIJKE, ambaye ametekwa Novemba 25,2011 amekombolewa baada ya kufanyika Operesheni ya Kikosi Maalum cha jeshi la taifa hilo. Taarifa hiyo imesema kuwa operesheni hiyo vilevile imefanikisha kutiwa mbaroni kwa watu wengine...
WATAALAMU wa kuchunguza Maiti, wameanza kufukua zaidi ya Makaburi 12 ya halaiki, katika mji wa Tikrit, nchini Iraq. Hatua hiyo imekuja siku kadhaa baada ya Wapiganaji wa Islamic State, kutimuliwa nje ya mji huo. Makaburi hayo yaanaminika kuwa na zaidi ya Maiti Elfu Moja Mia Saba ya Wanajeshi Waislamu wa Kishia, waliouwawa mwezi Juni mwaka jana na Wanamgambo wa...
MAKUBALIANO kuhusu muundo wa baadaye wa mpango wa nyuklia wa Iran, yamefikiwa baada ya mazungumzo na mataifa Sita makubwa yaliyokuwa yakifanyika nchini Uswisi. Kwa mujibu wa mkataba huo, Iran itapunguza uwezo wake wa kurutubisha madini ya Urani huku ikiahidiwa kuondolewa vikwazo kwa awamu. Mataifa makubwa ya Dunia na Iran sasa yanalenga kuandika mkataba kabambe ifikapo Juni 30....
BOTI ya uvuvi ya Urusi imezama katika visiwa vya Kamchatka , ikiwa na mabaharia wapatao hamsini na wanne ambao inadhaniwa kuwa wamekufa maji wote. Watu wapatao sitini na watatu wameopolewa ambao nao walikuwa ndani ya boti hiyo ya uvuvi,wengine wamekumbwa na homa ya mapafu na wengine kumi na watano wameripotiwa kuwa hawaonekani. Taarifa za awali zinasema kwamba kabla meli hiyo ya uvuvi haijazama ilikuwa na watu wapatao miamoja na thelathini na mbili ,Wengi wao walikuwa wanatokea maeneo ya Vanuatu, Latvia...