Sports

SAMATTA AIONGOZA KRC GENK KUCHEZA EUROPA
Slider

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta ameingoza KRC Genk kufuzu kucheza Ligi ya Europa baada ya kuichapa Sporting Charleroi kwa mabao 5­-1 na kushinda kwa jumla ya mabao 5-­3. Kulingana na gazeti la Mwananchi, Samatta, ambaye katika mchezo wa kwanza walionyukwa 2­0 alianzia benchi, jana aliaminiwa kuanza mchezo huo na kocha wake Peter Maes, akicheza pamoja na Nikos Karelis katika safu ya bora ya ushambuliaji. Katika mchezo huo, Samatta alifunga bao moja na kutegeneza mengine mawili yaliyofungwa na Karelis...

Like
370
0
Tuesday, 31 May 2016
ALEXANDER GAULAND ADAIWA KUTOA MATAMSHI YA KIBAGUZI
Slider

Naibu kiongozi wa Chama cha kupambana na uhamiaji nchini Ujerumani amezungumza maneno ya kibaguzi dhidi ya mchezaji nyota wa Ujerumani Jerome Boateng ambaye baba yake ni raia kutoka Ghana. Alexander Gauland,aliliambia Gazeti la Ujerumani la (the Frankfurter Allgemeine) kuwa watu wanafikiri Boateng ni mchezaji mzuri lakini kamwe hatomuhitaji kama rafiki yake. Gauland alilaaniwa vikali na wachezaji mbalimbali,Waziri wa mambo ya ndani pamoja na Rais wa shirikisho la soka nchini Ujerumani ,Reinhard Grindel amesema maneno yake kuwa hayana maana....

Like
317
0
Monday, 30 May 2016
ZLATAN IBRAHIMOVIC AITWA NA KLABU YA UINGEREZA
Slider

Aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya PSG nchini Ufaransa Zlatan Ibrahimovic amesema kuwa alipokea ombi la kujiunga na kilabu moja ya ligi ya Uingereza lakini akakataa kuthibitisha iwapo klabu hiyo ni Manchester United au la. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 yuko huru baada ya kuondoka PSG na amehusishwa na uhamisho wa United. Alipoulizwa iwapo ombi hilo linatoka Old Trafford ,alisema :Wacha tuone kitakachofanyika. Aliyekuwa kocha wa Chelsea Jose Mourinho anatarajiwa kutangazwa mkufunzi wa Manchester United na alifanya kazi na...

Like
329
0
Thursday, 26 May 2016
FIFA YAMTIMUA NAIBU KATIBU
Slider

Shirikisho la soka duniani Fifa limemtimua naibu katibu wake Markus Kattner kwa kujihusisha na ukiukwaji wa matumizi ya siri ya mamilioni ya dola. Kattnet raia wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 45 alikua akiitumikia nafasi hiyo baada ya aliyekua katibu Jerome Valcke kutimuliwa kazi kutokana na kashfa za rushwa. Kufutwa kazi kwa kiongozi huyu kulikuja mara moja baada ya bodi ya uchuguzi ya ndani ya Fifa kugundua kulikua na ukiukwaji na uvunjaji wa majukumu yake. Kulikuwa na ushahidi wa kutosha...

Like
306
0
Tuesday, 24 May 2016
MANCHESTER UNITED YAMFUTA KAZI VAN GAAL
Slider

Mkufunzi wa kilabu ya Manchester United Louis van Gaal amefutwa kazi kama mkufunzi wa klabu ya Manchester United ,huku aliyekuwa mkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho akitarajiwa kuchukua mahala pake. Raia huyo wa Uholanzi anaondoka baada ya kukamilisha miaka miwili ya kandarasi yake kati ya mitatu.Kitengo cha habari za michezo cha BBC Sport kiliripoti siku ya Jumamosi kwamba ushindi wa United wa kombe la FA dhidi ya Crystal palace utakuwa mechi yake ya mwisho akiwa mkufunzi. Uteuzi wa Mourinho unatarajiwa kuthibitishwa baada...

Like
290
0
Monday, 23 May 2016
BOMU FEKI LAAHIRISHA MECHI YA MAN UNTD
Slider

Polisi nchini Uingereza imethibitisha kuwa kitu kilichokuwa kinadhaniwa kuwa ni bomu kilichoonekana kwenye uwanja wa timu ya Manchester United wa Old Trafford hakikuwa bomu kama ilivyodhaniwa bali kilikuwa ni kifaa cha wanausalama cha mazoezi kwa ajili milipuko. Kifaa hicho kiliachwa na walinzi wa kampuni moja ya binafsi baada ya kufanya mazoezi yaliyowahusisha mbwa wenye kunusa vifaa na vitu vya kihalifu. Kutokana na kuonekana kwa kifaa hicho mechi kati ya Manchester United na Bournemouth iliahirishwa. Tayari kifaa hicho kimeshaharibiwa chini...

Like
269
0
Monday, 16 May 2016
EUROPA LEAGUE: LIVERPOOL YATINGA FAINALI
Slider

Jurgen Klopp amefanikiwa kuifikisha Liverpool katika hatua ya fainali ya ligi ya Uropa baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Villarreal. Wakiwa nyuma kwa bao moja katika mchezo wa awali, Liverpool walisawazisha matokeo baada ya Bruno Soriano kujifunga. Daniel Sturridge aliongeza bao la pili baadaye na kuanza kuidididmiza timu hiyo kutoka Uhispania baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Roberto Firmino. Baada ya mchezaji wa Villareal Victor Ruiz kutolewa kwa kadi nyekundu, Adam Lallana alipigilia msumari wa...

Like
282
0
Friday, 06 May 2016
CHELSEA NA TOTTENHAM WAMEPIGWA FAINI
Slider

Chelsea na Tottenham wamepigwa faini kwa pamoja na shirikisho la soka nchini Uingereza FA kwa kukabiliwa na makosa matatu ya kushindwa kuwazuia wachezaji pamoja na maofisa wake wakati na baada ya mchezo wa jumatatu. Kiungo wa Spurs Mousa Dembele amekumbana na adhabu pia ya kusababisha vurugu katika mchezo huo ulioisha kwa suluhu ya 2-2.FA inasema kuwa kitendo cha Dembele kumuingizia vidole machoni mchezaji wa Chelsea Diego Costa ni utovu mkubwa wa nidhamu. Hiyo ina maana ”akikutwa na hatia” kufungiwa michezo...

Like
376
0
Thursday, 05 May 2016
ANDY MURRAY AANZA VYEMA MICHUANO YA MADRID OPEN
Slider

Mwingereza Andy Murray ameanza vyema kutetea taji lake katika michuano ya Madrid Open kwa ushindi wa seti 7-6 7-3 3-6 na 6-1 dhidi ya Radek Stepanek. Ilichukua muda wa saa mbili na dakika 16 kwa Murry kumshinda Stepanek raia wa Czech mwenye miaka 37. ”Sikucheza michezo mingi kipindi cha nyuma.Ilikua ngumu sana,”alisema Murray mwenye miaka 28 ambaye atakutana na Gilles Simon ama Pablo Busta katika mzunguko wa tatu siku ya Alhamisi. Mapema kwenye mchezo wa awali Muhispaniola Rafael Nadal alimshinda...

Like
297
0
Wednesday, 04 May 2016
LEICESTER CITY MABINGWA EPL, HUU NDIO MKWANJA WALIOVUTA
Slider

Leicester City watajizolea $200m (£150m) baada yao kufanikiwa kushinda Ligi Kuu ya Uingereza Jumatatu, watathmini wa michezo na utangazaji wa Repucom wanasema. Pesa hizo zinatokana na tuzo ya kushinda Ligi ya Premia, pesa za kushiriki Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, na ongezeko la mapato ya kila siku kutokana na mauzo ya tiketi. Klabu hiyo pia itajivunia kupanda kwa thamani ya udhamini na pia ongezeko la mashabiki duniani. Klabu hiyo inayotoka East Midlands itashiriki katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu...

Like
343
0
Tuesday, 03 May 2016
EPL: LEICESTER CITY YANYEMELEA UBINGWA!!!
Slider

Leicester City wamebakiwa na alama mbili pekee kuupata ushindi wa ligi kuu ya England baada ya kupata sare ya 1-1 dhidi ya klabu ya Manchester United katika dimba la Old Trafford huku wakitegemea matokeo ya mchezo kati ya Chelsea dhidi ya Tottenham utakaopigwa leo hii majira ya saa nne usiku kwa saa za afrika mashariki katika dimba la Stamford Bridge. Mbweha walipata afueni baada ya kuwa nyuma kwa goli moja lililofungwa na Antony Martial dakika ya nane ya mchezo kabla...

Like
270
0
Monday, 02 May 2016