Slider

WATANZANIA WAMETAKIWA KUENDELEZA MILA NA DESTURI ZA MWALIM NYERERE
Local News

MMOJA wa Viongozi Wakuu wa kiroho wa waislam Dhehebu la shia Ithnasheriya Tanzania SHEIKH HEMED JALALA amewataka watanzania  kuendeleza mila na desturi za kistaarabu alizoziacha mwasisi wa Taifa hili Mwalimu Julius Kambarage Nyerere  hasa katika kipindi hiki cha chaguzi. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dare s  salaam katika kumbukumbu ya mwaka mpya wa 1,437 H wa kiislamu amesema mwaka uliopita ulimwengu wa kiisalamu ulikumbana na changamoto nyingi  hivyo kwa mwaka huu mpya ipo haja ya kujifunza na kujirekebisha kutokana...

Like
253
0
Thursday, 15 October 2015
VYAMA VYA SIASA VIMESHAURIWA KUZUNGUMZA NA WAFUASI WAO KUTII SHERIA
Local News

BARAZA la Vyama vya Siasa nchini limevishauri vyama vya siasa kuzungumza na kuwasihi wafuasi wao kutii sheria bila shuruti ili kuendeleza amani iliyopo nchini.   Aidha Baraza hilo limeviomba Vyama kuwaeleza wafuasi na wapenzi wao kurudi majumbani na kuendelea na shughuli zao mara baada ya kupiga kura siku ya uchaguzi mkuu kama ilivyokuwa kwa hatua za uandikishwaji.   Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Peter Kuga Mziray wakati alipokuwa akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu...

Like
318
0
Thursday, 15 October 2015
GHASIA KENYA: CHUO CHAFUNGWA
Global News

CHUO kikuu kimoja nchini Kenya kimefungwa baada ya mwanafunzi mmoja kufariki wakati wa makabiliano kati ya wanafunzi na polisi usiku wa jana. Kaimu Naibu Chansela wa chuo kikuu hicho cha Maseno Bi Catherine Muhoma, ameagiza chuo hicho kufungwa haraka kutokana na vurugu kuzidi. Ghasia zilianza baada ya polisi kudaiwa kulifyatulia risasi gari lililokuwa likitumiwa na wanafunzi kupigia debe mmoja wa wagombea katika kampeni za uchaguzi wa viongozi wa wanafunzi...

Like
207
0
Tuesday, 13 October 2015
HUMAN RIGHT WATCH LAWALAUMU WAPIGANAJI WA KIKURDI
Global News

SHIRIKA la kibinadamu la Human Rights Watch limewalaumu wapiganaji wa kikurdi kutoka kaskazini mashariki Mashariki mwa Syria kwa kufanya kampeni ya makusudi kuwatimua katika makazi yao watu wenye asili ya Kiarabu kutoka maeneo ambayo wameyakomboa. Taarifa zinaeleza kuwa tatizo hilo linalingana na lililotokea awali katika eneo la Kaskazini mwa Iraq, ambapo Wakurdi wa Syria waliojitokeza kama wafuasi waaminifu zaidi kwa muungano wa wanajeshi wanaoongozwa na Marekani na kushambulia eneo hilo. Hata hivyo imebainika kuwa Wamarekani waliwasaidia...

Like
218
0
Tuesday, 13 October 2015
MKAPA ATAKA MABADILIKO UN
Local News

RAIS Mstaafu wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Benjamin Mkapa ametoa wito wa kufanyika kwa mabadiliko katika mfumo wa uendeshaji wa Umoja wa Mataifa ili kukidhi mahitaji ya sasa ya dunia. Mkapa ameyasema hayo jana katika mdahalo wa juma la Umoja wa Mataifa ambalo unakamilika leo sambamba na maadhimisho ya miaka 70 tangu kuundwa kwa umoja huo.   Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mh. Benjamin William Mkapa akimshukuru Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa...

Like
548
0
Tuesday, 13 October 2015
RAIS KIKWETE AZINDUA MTAMBO WA KUFUA UMEME KINYEREZI ONE
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo amezindua mtambo wa kufua Umeme uliopo Kinyerezi one Jijini Dar es salaam wenye uwezo wa Megawati 150. Katika uzinduzi huo Rais Kikwete amesema kuwa uzinduzi huo ni mojawapo ya mikakati ya kufikia lengo la mpango wa maendeleo wa miaka mitano unaoishia mwakani wa kufikisha megawati 2780 ambapo hadi sasa zipo megawati 1490 na kubakia megawati 1390. Mbali na hayo amesema kuwa Tanzania inaanza mpango mpya mwakani wa kuifanya...

Like
385
0
Tuesday, 13 October 2015
IS YASHUKIWA KUHUSIKA NA MAUAJI ANKARA
Global News

WAZIRI mkuu wa Uturuki Ahmet Davotuglo amesema kuwa wachunguzi wa nchi hiyo wanakaribia kumtambua mmoja kati ya washambuliaji wa kujitoa muhanga wa mashambulizi ya mabomu dhidi ya maandamano ya amani katika kituo cha treni yaliyowaua watu wasiopungua 97 mjini Ankara. Davutoglu amesema kwamba kundi la dola la Kiislamu limepewa kipaumbele katika uchunguzi huo kwa kushukiwa kuhusika kwa kiasi kikubwa. Wakati hayo yakijiri katibu mkuu wa Jumuiya ya kujihami ya NATO Jens Stoltenberg ameihimiza Uturuki iwe makini katika njia inazozitumia...

Like
218
0
Tuesday, 13 October 2015
ZIMBABWE: MUUAJI WA SIMBA CECIL KUTOSHITAKIWA
Global News

WAZIRI wa Mazingira wa Zimbabwe Oppah Muchinguri amesema kuwa daktari wa meno ambaye alisababisha hali ya taharuki baada ya kumuua Simba mmoja mashuhuri nchini Zimbabwe hatashtakiwa kwa kuwa alikuwa na kibali cha kuwinda. Daktari huyo anayefahamika kwa jina la Walter Palmer alikubali kumuua Simba aitwaye Cecil lakini alikana kutekeleza shughuli za uwindaji kinyume cha sheria. Awali Waziri huyo alitaka Palmer afunguliwe mashtaka ya kumuua mnyama huyo lakini baadaye ilibainika kuwa hakuna sheria iliyovujwa katika mauaji ya Simba...

Like
255
0
Tuesday, 13 October 2015
VIONGOZI WA SIASA WAMETAKIWA KUHAMASISHA WAFUASI WAO KUTOVUNJA AMANI
Local News

OFISI ya Msajili wa Vyama  Vya Siasa imewaasa na kuwataka viongozi wote wa  vyama  vya siasa kutoa kauli na maelekezo kwa wafuasi wao na wanachama wa vyama vyao kutoshiriki katika aina yoyote ile ya uvunjifu wa amani.   Hayo yamesemwa  na Msajili wa Vyama Vya Siasa, Jaji Francis Mutungi wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dares Salaam.   Jaji Mutungi amesema kuwa Dhamana ya nchi ipo mikononi mwa wananchi hivyo ushawishi wowote ule wa uvunjifu wa Amani...

Like
246
0
Tuesday, 13 October 2015
RAIA WA PALESTINA ASHAMBULIWA ISRAEL
Global News

POLISI wa Israel wamesema wamempiga risasi na kumuua mwanamume mmoja wa Kiarabu mapema leo aliyejaribu kumchoma kisu afisa mwenzao huko Jerusalem Mashariki.   Polisi wamemueleza mshambuliaji huyo wa Kipalestina kuwa ni gaidi lakini hawakutoa maelezo zaidi kuhusu utambulisho wake.   Msemaji wa polisi amesema Mpalestina huyo ambaye ni wa 24 kuuawa tangu mwanzoni mwa mwezi huu, alimshambulia afisa wa Israel aliyejaribu...

Like
211
0
Monday, 12 October 2015
MZOZO WA SYRIA: MAWAZIRI WA MAMBO YA NJE ULAYA KUKUTANA LEO
Global News

MAWAZIRI wa Mambo ya nje wa nchi za Umoja wa Ulaya wanakutana leo Luxembourg kujadili njia za kuutafutia ufumbuzi mzozo nchini Syria. Mkutano huo unafanyika huku kukiwa na wasiwasi kuhusu hatua ya Urusi kujiingiza kijeshi katika mzozo huo na mustakabali wa rais wa Syria Bashar al Assad ukiwa haujulikani. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, mzozo wa Syria umesababisha watu wapatao 250,000 kuuawa tangu mwaka...

Like
207
0
Monday, 12 October 2015