Slider

NEC YAWATAKA VIONGOZI WA SIASA KUEPUKA TAARIFA ZISIZO SAHIHI KUHUSU TUME HIYO
Local News

TUME ya Taifa ya Uchaguzi-NEC, imewataka viongozi wa vyama vya siasa kuepuka kutoa taarifa na shutuma sisizo sahihi kuhusu Tume hiyo na badala yake wajikite katika kufikisha taarifa zilizo sahihi na zilizokusudiwa kwa Wafuasi wao na kuwahamasisha wananchi kujitokeza kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa tarehe 25 Oktoba 2015.   Akizungumza leo katika  Mkutano wa Tume na viongozi  wa vyama vya siasa jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Damian Lubuva, amesema Tume imeaandaa vituo vya kupigia kura elfu...

Like
202
0
Monday, 12 October 2015
TANZANIA NA NAMIBIA KUSIMAMIA USALAMA AFRIKA
Local News

RAIS wa jamhuri ya muungano wa Tanzania dokta Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Rais wa Namibia Dokta Hage Gottfried Geingob, wameahidi kuwa watasimamia kwa juhudi nchi za bara la Africa ili kuhakikisha zinakuwa na usalama wa kisiasa na  kiuchumi hata watakapo maliza muda wao wa uongozi ili wananchi wake waweze kuishi kwa amani. Akizungumza Ikulu Jijini Dar es Salaam  wakati akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari Dokta Kikwete amesema kuwa  endapo viongozi  wakubwa wa Africa wakiweza kuwakomboa wananchi wao...

Like
197
0
Monday, 12 October 2015
CHINA OPEN: DJOKOVIC AMBWAGA RAFAEL NADAL
Slider

Mcheza tenesi namba moja kwa ubora kwa upande wa wanaume Novak Djokovic ametwaa taji la michuano ya wazi ya China. Djokovic alimshinda Rafael Nadal anayeshikilia nafasi ya nane kwa ubora wa mchezo huo duniani kwa Seti 6-2 6-2 na kushinda taji lake la sita kwa mwaka huu. Na kwa upande wa wanawake Muhispani Garbine Muguruza alipata ushindi wa seti 7-5 6-4 dhidi ya Timea Bacsinszky na kutwaa taji la pili. Kwa ushindi huo Muguruza anapanda mapka nafasi ya nne kwa...

Like
224
0
Monday, 12 October 2015
UTURUKI YAOMBOLEZA VIFO VYA WATU 95
Global News

MAELFU ya Watu wamekusanyika mjini Ankara nchini Uturuki kuomboleza vifo vya takriban watu 95 waliouawa kwa milipuko miwili ya mabomu. Watu wanaounga mkono Chama cha Kikurdi ambao walikuwepo kwenye mkutano katika eneo ambalo mabomu yalilipuka wanaamini kuwa idadi ya kweli ya waliopoteza maisha ni Watu 128. Vyanzo vya ulinzi vinasema kuwa vinalishuku kundi la wanamgambo wa IS kuhusika kwenye shambulio hilo huku Serikali ikikanusha vikali madai kuwa imehusika katika mashambulizi...

Like
254
0
Monday, 12 October 2015
PUTIN ATETEA MASHAMBULIO YA URUSI SYRIA
Global News

RAIS wa Urusi Vladimir Putin ametetea uamuzi wa nchi yake wa kuchukua hatua za kijeshi nchini Syria, kwa kusema kuwa lengo lake ni kusaidia utawala halali wa Rais wa Syria Bashar al-Assad. Awali rais Putin aliiambia runinga ya taifa ya Urusi kwamba Moscow pia inataka kuunda mazingira yatakayowezesha kuwepo kwa maafikiano ya kisiasa nchini humo. Hata hivyo amekanusha madai kwamba mashambulio ya ngani ya Urusi yanalenga makundi ya upinzani badala ya yale ya wapiganaji wa Islamic...

Like
231
0
Monday, 12 October 2015
UNESCO YAENDESHA WARSHA KWA WAKUU WA HIFADHI NA VITUO VYA UTALII
Local News

Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) kwa kushirikiana na Idara ya mambo ya kale imeendesha warsha ya siku moja kwa wakuu wa hifadhi na vivutio vya utalii nchini kwa lengo la kushirikishana masuala muhimu yanayohusu utalii.   Warsha hiyo iliyohudhuriwa na Wakuu wa hifadhi mbalimbali nchini imehusisha uwasilishaji wa mafanikio na changamoto wanazokutana nazo wakuu wa hifadhi hizo huku matatizo makubwa yakiwa ni Ukosefu wa fedha kwaajili ya Kujiendesha.   Akizungumza katika warsha hiyo Mkuu wa Hifadhi ya...

Like
301
0
Monday, 12 October 2015
SERIKALI IJAYO KUENDELEZA USHIRIKIANO NA UDUGU NA NAMIBIA
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema ushirikiano na udugu baina ya Tanzania na Namibia utaendelea kuwepo hata kwa Serikali ya Awamu ya Tano itakayokuwepo madarakani. Rais Kikwete aliyasema hayo jana Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akimkaribisha Rais wa Namibia Dokta Hage Geingob kwenye mkutano wa pamoja na waandishi wa habari. Kwa upande wake Rais wa Namibia amesema kuwa amefurahishwa na hali ya Amani iliyopo nchini hususani kwa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu...

Like
235
0
Monday, 12 October 2015
MUZIKI MNENE KIGAMBONI 2015
Local News

MUZIKI mnene bar kwa bar wiki iliyopita ulivuka kivuko na kuhamia kigamboni.Wakazi wa eneo hilo ambao ni wasikilizaji wa 93.7 EFM walipata burudani ya aina yake kutoka kwa timu nzima ya EFM redio. Burudani ilianza na kabumbu katika uwanja wa shule ya msingi Ufukoni kati ya EFM na magogoni veteran.Timu ya magogoni veterani ilitetea ushindi nyumbani kwa kuifunga EFM magoli manne huku EFM ikiambulia mawili 2. Kwa kuwa kigamboni kumezungukwa na fukwe kibao, muziki mnene uliendelea katika fukwe ya Navy...

Like
568
0
Monday, 12 October 2015
VIDEO: VANESSA – NEVER EVER
Entertanment

Vanessa ameshinda tuzo ya Best Female East Africa kwenye Tuzo za AFRIMMA Unaweza kuitazama video ya wimbo mpya wake mpya...

Like
575
0
Monday, 12 October 2015
PICHA: E-FM VS MAGOGONI VETERANI MUZIKI MNENE BAR KWA BAR 2015
Slider

Mchezo wa mpira wa miguu kati ya E-fm Vs Magogoni Veterani umemalizika katika uwanja wa Ufukoni huku matokeo ya mchezo huo yakiwaweka vifua mbele maveterani wa Magogoni wakiwa na ushindi wa magoli 4 – 2. Efm ndio walikuwa wa kwanza kuliona lango la Magogoni Veterani mpaka kipindi cha mapumziko Efm walikuwa mbele kwa magoli mawili kwa moja. Hali ilibadilika katika kipindi cha pili ambapo maveterani wa Magogoni waliongeza mashambulizi katika lango la Efm na kuweza kupata magoli matatu ya haraka....

Like
434
0
Saturday, 10 October 2015
WIZARA YA ULINZI URUSI YAKANUSHA KUANGUSHA MAKOMBORA IRAN
Global News

WIZARA ya ulinzi ya Urusi imekanusha madai yaliyotolewa na afisa mmoja wa Marekani kuwa makombora manne ya Urusi yaliyofyatuliwa katika Bahari ya Caspian kuelekea Syria yalianguka nchini Iran. Msemaji wa wizara hiyo Jenerali Igor Konashenkov amesema makombora yote yaliyofyatuliwa yalipiga katika maeneo yaliyolengwa. Afisa wa Marekani, ambaye jina lake halikujulikana, amesema makombora hayo yalianguka nchini Iran siku ya Jumatano lakini hakutoa maelezo yoyote kuhusu mahali yalikoanguka au ikiwa yalisababisha uharibifu wowote....

Like
306
0
Friday, 09 October 2015