IMEELEZWA kuwa Tanzania inapokea idadi ya wagonjwa wapya takribani elfu 44,000 kila mwaka lakini wengi wao kwasababu mbalimbali hawafiki Hospitalini, na ni asilimia 10 tu ya wagonjwa ndio wanaofika katika Taasisi ya Saratani Ocean road. Hata hivyo kati ya hao takribani asilimia 80 hufika wakiwa katika hatua za juu za ugonjwa, hali ambayo hupunguza uwezekano wa kutoa matibabu ya kuponyesha ugonjwa wao. Akizungumza na Wanahabari jijini Dar es salaam Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Dokta...
MELI nne za kijeshi za Urusi zimeshambulia maeneo ya kundi la Dola la Kiislamu nchini Syria kwa makombora, hii ikiwa ni moja kati ya kampeni zake za kijeshi kulishambulia kundi hilo. Rais Vladimir Putin ameelezwa na waziri wake wa ulinzi Sergei Shoigu kwamba pamoja na ndege za kijeshi, meli nne za kijeshi kutoka eneo la bahari ya Caspian zimeshiriki katika hujuma hiyo na kuongeza kwamba meli hizo za kijeshi zimefanya mashambulizi 26 ya makombora dhidi ya ...
MAHAKAMA nchini Brazil imebaini kuwa Rais wa nchi hiyo Dilma Rousseff amekiuka sheria za usimamizi wa akaunti ya bajeti ya mwaka jana. Serikali ya nchi hiyo ilishitakiwa kwa tuhuma za kuazima fedha kinyume cha sheria benki kuu kwa lengo la kuziba upungufu wa bajeti serikalini. Hata hivyo Kambi ya upinzani nchini Brazil imesema kuwa hatua hiyo ya mahakama inawasafishia njia ya kuanza kuchukua hatua za kisheria kumuondoa madarakani Rais...
WAKAZI wa jiji la Dar es salaam wamewaomba wamiliki wa vyombo vya usafiri kuangalia upya viwango vya bei ya nauli mara baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji EWURA kushusha bei ya mafuta . Wakizungumza na E fm baadhi ya wakazi hao wamewaomba wamiliki kuwapunguzia bei za nauli kwani bei za mafuta zimeshuka kutoka bei za awali ambapo zilikuwa shilingi 2300 kwa lita moja ya petroli tofauti na ilivyo sasa ambapo bei ya petrol kwa lita moja...
KATIBU mkuu kiongozi balozi ombeni sefue leo anatarajia kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa wadau wa takwimu ulioandaliwa na ofisi ya taifa ya takwimu (nbs) kwa ajili ya kukubaliana jinsi ya kushirikiana katika kuhakikisha takwimu za viashiria vya mpango wa maendeleo endelevu zinapatikana kwa wakati. akizungumza na wandishi wa habari jijini dar es salaam jana afisa habari wa ofisi hiyo, veronica kazimoto amesema mkutano huo utakuwa na lengo la kuelimishana juu ya kukamilika kwa utekelezaji wa malengo ya milenia (mdgs)...
Kamati ya maadili katika shirikisho la soka duniani FIFA imependekeza Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA asimamishwe kazi kwa siku tisaini. Wanachama wa kamati hiyo walikutana wiki hii baada ya Jaji mkuu nchini Uswizi kufungua mashtaka ya uhalifu dhidi ya Blatter mwezi uliopita. Blatter anatuhumiwa kwa kutia saini kandarasi zisizo na manufaa yoyote kwa FIFA mbali na kufanya ‘malipo’ kwa rais wa shirikisho la UEFA Michel Platini. Blatter ambaye ni raia wa Uswizi amekuwa rais wa FIFA tangu mwaka...
Chini ya mwalimu mzawa Charles Boniface Mkwasa, kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kimeendelea kuonyesha mabadiliko ya hali ya juu kufuatia mchezo wao dhidi ya timu ya taifa ya Malawi. Stars imefanikiwa kuitandika Malawi 2-0 katika uwanja wa taifa jijini Daresalaam katika mchezo wa kuwania kucheza Kombe la Dunia . Magoli ya stars yalitiwa nyavuni na Mbwana Samatta pamoja na Thomas Ulimwengu katika kipindi cha kwanza magoli yaliyodumu hadi mwisho wa...
Hizi ni picha za mjengo mpya wa Jay Z na Beyoncé Mjengo huo unapatikana Holmby Hills, kwenye jimbo la California nchini Marekani Wawili hao wametoa kitita cha dola milioni 45 za kimarekani ambayo ni sawa na $150k za malipo ya kukodi mjengo huo kwa mwezi. Kwenye mkataba uliosainiwa na wawili hawa utawafanya waishi kwenye mjengo huo kwa mwaka...
WAZIRI mkuu nchini Yemeni Khaled Bahah amenusurika kifo baada ya hoteli aliokuwa akiishi pamoja na baraza lake la mawaziri kushambuliwa mjini Aden. Milipuko kadhaa imeikumba hoteli ya Qasr siku ya jumanne asubuhi pamoja na makao makuu ya vikosi vya milki za kiarabu vinavyoiunga mkono serikali. Msemaji wa serikali nchini Yemen, Rajeh Badi amekiambia chombo cha habari cha AFP kwamba roketi zilirushwa katika maeneo matatu kutoka nje ya mji huo ikiwemo eneo walilokuwepo. Hoteli ya Qasr ilioshambuliwa nyumba...
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) limewakutanisha wadau mbalimbali katika kongamano la kujadili na kuhamasisha Amani katika kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Kongamano hilo lililofanyika wilayani Simanjiro mkoani Manyara limewakutanisha viongozi wa dini, mila na wawakili wa muungano wa Redio za Jamii nchini ambao kwa pamoja walisisitiza umuhimu wa Amani. Ofisa Miradi wa Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin...
MAMLAKA ya Manunuzi ya Umma Tanzania-PPRA-imezifungia kushiriki zabuni kampuni 7 pamoja na wakurugenzi wake kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kampuni hizo kufanya vitendo vya udanganyifu katika manunuzi. Akizungumza Jijini Dar es Salaam leo Mwenyekiti wa Bodi wa PPRA Martin Lumbanga amesema kuwa miongoni mwa kampuni hizo kampuni 6 zimefungiwa kwa kipindi cha miaka miwili kwa kukiuka masharti ya mkataba na kampuni moja imefungiwa kwa kosa la kuwasilisha dhamana za zabuni za kughushi. Miongoni mwa kampuni zilizofungiwa kushiriki kununua...