Slider

VIPIMO VYA MARADHI YA MOYO KUFANYIKA BURE MUHIMBILI LEO
Local News

LEO ni Siku ya Afya ya Moyo Duniani ambapo kila ifikapo September 29  ya kila mwaka Dunia nzima huadhimisha siku hiyo inayolenga kuijulisha jamii baadhi ya masuala mbalimbali yanayo husu afya ya Moyo. Katika mkutano na waandishi wa habari jana, jijini Dar es salaam daktari bingwa wa magonjwa ya moyo nchini, TULIZO SHEMU SANGA amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi leo katika hospitali ya Taifa ya muhimbili ili kupima afya hiyo bure. Aidha DKT TULIZO ameongeza kuwa kwa mujibu wa utafiti...

Like
358
0
Tuesday, 29 September 2015
WENGER AGOMA KUMJIBU MOURINHO
Slider

Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger  amekataa kujibu chokochoko za Jose Jose Mourinho na kuonyesha zaidi kuwa na malengo na klabu yake. Mourinho alitoa maneno ambayo kimsingi hayakumtaja Wenger moja kwa moja ila kwa tafsiri ya ndani inaonyesha meneja huyu wa Chelsea alilenga kumsema Arsene Wenger. katika maelezo yake Mourinho alitaja kufanana kwa waalimu wa timu zote zinazoshiriki ligi ya Uingereza kuwa na presha ya kutotaka kufanya vibaya hali inayowafanya wawe na kazi ngumu katika kuhakikisha wanafikia malengo huku akiwataja...

Like
233
0
Tuesday, 29 September 2015
UINGEREZA YATANGAZA KUTUMA MAJESHI SOMALIA
Slider

UINGEREZA imetangaza kwamba itawatuma wanajeshi wake Somalia kusaidia wanajeshi wanaolinda amani nchini humo. Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron amesema wanajeshi 70 watatumwa Somalia kujiunga na kikosi cha Umoja wa Mataifa kinachowasaidia wanajeshi wa Muungano wa Afrika wanaokabiliana na wapiganaji wa al-Shabab. Amedokeza pia kuwa wanajeshi takriban 300 watatumwa Sudan...

Like
212
0
Monday, 28 September 2015
WAMILIKI WA VITALU VYA MBOGAMBOGA WAMETAKIWA KUFUATA KANUNI NA TARATIBU ZA KIAFYA
Local News

WAMILIKI wa vitalu vya mbogamboga wametakiwa kufuata kanuni na taratibu za kiafya zilizowekwa na serikali pindi wanapolima kilimo hicho ili kulinda afya za watumiaji.   Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Ubungo NHC, AMANI SIZYA ameiambia efm radio kuwa asilimia kubwa ya wakulima wa mbogamboga wanatumia maji yanayopita kwenye mitaro ya maji taka kumwagilia mboga hizo, na kusababisha kutokuwa salama kiafya kwa...

Like
240
0
Monday, 28 September 2015
DK BILAL AONGOZA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI KUUAGA MWILI WA CELINA KOMBANI
Local News

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Muhammed Gharib Bilal leo amewaongoza mamia ya waombolezaji katika kuuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Celina Kombani aliyefariki Septemba 24 katika hospitali ya Andraprash Apolo Nchini India kutokana na ugonjwa wa Saratani ya Kongosho.   Tukio hilo ambalo limefanyika katika viwanja vya karimjee jijini Dar es salaam limehudhuriwa na viongozi mbali mbali wa chama na serikali kutoka Tanzania bara na visiwani...

Like
253
0
Monday, 28 September 2015
TANZANIA YAAHIDI KUCHUKUA HATUA 5 ZA KUTETEA NA KUENDELEZA HAKI ZA WANAWAKE
Local News

TANZANIA imeahidi kuchukua hatua tano muhimu za kutetea na kuendeleza haki za wanawake kati ya sasa na mwaka 2030, kwa kufuta sheria kandamizi kwa wanawake na kutunga sheria za kuleta usawa wa kijinsia.   Miongoni mwa hatua hizo ni pamoja na kufuta na kufanya mabadiliko ambayo yanaendeleza vitendo vya kiutamaduni vinavyoendeleza ubaguzi kwa wanawake ikiwemo Sheria ya Ndoa, Sheria ya Urithi na kutunga Sheria ya Kukomesha Ukatili dhidi ya wanawake.   Msimamo huo umeelezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano...

Like
219
0
Monday, 28 September 2015
HAMILTON ATWAA TAJI LA JAPAN GP
Slider

Dereva wa magari yaendayo kasi Lewis Hamilton ameshinda michuano ya Suzuki na kutwaa taji la 41 katika mchezo huo. Dereva huyu wa timu Mercedes, alishinda taji hilo na kumfikia mkongwe wa michuano ya Fomula 1 Mbrazili Ayrton Senna. Hamilton alimzidi kwa alama 48 dereva mwenzake wa timu ya Mercedes, Nico Rosberg, katika mbio za michuano hiyo ya Grand prix. Kukiwa kumesalia mbio tano Hamilton, anashikilia alama 48 zaidi ya Rosberg, huku akionekana na uwezo wa kushinda taji lingine la tatu...

Like
285
0
Monday, 28 September 2015
17 WAZAMA BAHARINI SYRIA
Global News

KIASI cha raia 17 wa Syria wamezama katika bahari ya Aegean baada ya kuondoka Uturuki wakielekea Ugiriki. Takriban wahamiaji wengine 20 kutoka Syria wameokolewa na maafisa wa Uturuki baada ya boti yao kuzama na Vyombo vya habari vya Uturuki vimeripoti hapo jana kuwa miongoni mwa waliokufa maji ni watoto watano. Boti hiyo ilikuwa imewabeba wahamiaji 37 na kwa mujibu wa shirika la kimataifa la kushughulikia wahamiaji IOM, zaidi ya wahamiaji laki 350,000 wengi wao kutoka Syria wameingia Ugiriki mwaka huu...

Like
270
0
Monday, 28 September 2015
WITO UMETOLEWA KWA MASHIRIKA, MAKAMPUNI NA TAASISI KUSAIDIA JAMII
Local News

WITO umetolewa kwa Taasisi, mashirika na makampuni kote nchini kujenga utamaduni  wa kutumia sehemu ya faida wanayoipata kuisaidia jamii kupitia sekta ya afya ambayo inakabiliwa na changamoto mbalimbali. Wito huo umetolewa mjini Kisarawe na Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam Profesa Emanueli Mjema wakati akikabidhi msaada wa mashuka 176 yaliyotolewa na chuo hicho kusaidia wodi ya Wazazi ya Hospitali ya wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani. Amesema chuo cha CBE mwaka huu kimetimiza miaka 50 tangu kuanzishwa...

Like
433
0
Monday, 28 September 2015
TANZANIA YAUNGA MKONO MALENGO ENDELEVU YA MAENDELEO
Local News

TANZANIA imeunga mkono Malengo Endelevu ya Maendeleo (Sustainable Development Goals – SDG’s), ikisisitiza kuwa malengo hayo ni silaha ya kutosha ya kufuta umasikini duniani katika sura zake zote ifikapo mwaka 2030. Aidha imesema kuwa endapo dunia itafanikiwa kutekeleza malengo hayo ya SDG’s katika miaka 15 ijayo kama ilivyopangwa ni dhahiri kuwa ifikapo mwaka 2030 dunia itakuwa mahali pazuri zaidi. Msimamo huo wa Tanzania umeelezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipohutubia Baraza Kuu...

Like
254
0
Monday, 28 September 2015
MWILI WA MAREHEMU CELINA KOMBANI WAAGWA LEO
Local News

MWILI wa aliyekuwa Waziri wa nchi ofisi ya Rais menejimenti ya Utumishi wa Umma na mgombea Ubunge wa jimbo la Ulanga mashariki kupitia-CCM– marehemu Celina Kombani  kuagwa leo katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es salaam. Kwa mujibu wa Taarifa zilizotolewa na Ofisi ya Bunge kupitia kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano zinaeleza kuwa baada ya Zoezi hilo kukamilika mwili wa marehemu utasafirishwa kwenda nyumbani kwa marehemu mkoani Morogoro ambapo utapokelewa na viongozi mbalimbali wa mkoa na maafisa kutoka serikalini....

Like
326
0
Monday, 28 September 2015