MAHUJAJI kutoka duniani kote wameanza kukusanyika leo hii katika mlima wa Arafat nchini Saudi Arabia kwa kisimamo cha siku nzima ambacho ndio kilele cha ibada ya Hijja inayofanyika kila mwaka. Takriban mahujaji milioni 2 wanakusanyika bega kwa bega kwa siku nzima na Wengi wameonekana wakiwa wamenyanyua mikono yao juu huku wakimuomba msamaha Mwenyezi Mungu kwa makosa yao na ya jamaa zao. Siku kama ya leo miaka 1,400 iliyopita, Mtume Muhammad alitoa khutba yake ya mwisho katika mlima huwo wakati wa...
IMEELEZWA kuwa Tanzania inatarajia kuzindua Dira ya Madini mapema mwezi Januari mwaka 2016, ambayo ni sehemu ya Dira ya Madini Afrika iliyoasisiwa mwaka 2009 na wakuu wa nchi zenye madini Afrika kwa lengo la kuboresha sekta hiyo nchini. Hayo yamesemwa na Mratibu wa Mradi wa Biofueli, Wizara ya Nishati na Madini, Paul Kiwele, katika warsha kuhusu dira mpya ya madini Afrika iliyofanyika mjini Morogoro. Warsha hiyo ya siku tatu iliyoandaliwa na Wizara ya Nishati na Madini imewakutanisha wataalam kutoka taasisi...
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo amekabidhi misaada yenye thamani ya shilingi milioni 9 na laki 7 kwa vituo mbalimbali vya makundi maalum Tanzania bara na Visiwani ikiwa kama zawadi ya kusherekea sikukuu ya Idd Alhaji inayotarajiwa kuwa kesho Septemba 24 mwaka huu. Misaada hiyo iliyojumuisha mchele , mafuta ya kupikia na mbuzi vimegaiwa kwa vituo hivyo ili na wao waweze kusherekea na kufanikisha sikukuu za Idd kama watu wengine kwa kuwa sikukuu hiyo husherekewa kila mwaka na...
Legend wa mchezo wa baseball kutoka nchini Marekani, Yogi Berra ambae alikuwa chachu ya utengenezwaji wa vibonzo vya Yogi Bear amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 90. Jengo la kumbukumbu linalofanya hifadhi ya kumbukumbu za kazi na maisha ya ya legend huyu lilitangaza habari za kifo cha Yogi Berra siku ya jumanne jioni. Berra ambae ameitumikia timu ya New York Yankees kwa takribani miaka 19 amewahi kuwa mchezaji mwenye thamani ya juu kwa mara tatu huku akiweka rekodi ya...
Daktari wa klabu ya Chelsea ya nchini England Eva Carneiro ameamua kuondoka katika klabu hiyo wiki sita baada ya kukwaruzana na meneja wa timu Jose Mourinho. Carneiro aliingiliwa katika majukumu yake baada ya Mourinho kusema kuwa benchi lake la matibabu lilikuwa na watu wasiojua majukumu yao kwa kumtibu hovyo Eden Hazard wakati wa sare ya 2-2 na Swansea tarehe 8 Agosti. Chelsea ilimuomba Carneiro mwenye miaka 42 kurejea kazini lakini alikataa na kwa sasa analishughulikia suala hilo kisheria zaidi. Chama...
KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amewasili nchini Marekani kuanza ziara ambako pia atahudhuria kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, na kuzungumza katika kikao cha Congress ya Marekani, ambacho kinajumuisha Baraza la Wawakilishi na Baraza la Seneti. Papa Francis mwenye umri wa miaka 78 alipokelewa na Rais wa Marekani Barack Obama na mkewe Michelle Obama katika uwanja wa ndege za kijeshi wa Andrews karibu na Washington DC. Awali, katika ziara yake ya siku tatu...
KIONGOZI wa mapinduzi ya kijeshi ya wiki iliyopita nchini Burkina Faso Jenerali Gilbert Diendere hii leo anatarajiwa kukabidhi madaraka kwa rais aliyempindua, Michel Kafando baada ya shinikizo kubwa kutoka kwa viongozi wa kikanda. Makubaliano yamepatikana kati ya jenerali huyo na jeshi la nchi yake usiku wa leo, hii ikiwa ni kwa mujibu wa wawakilishi wa pande hizo mbili. Makubaliano hayo yamejengwa juu ya vipengele vitano, ambavyo vinajumuisha kile kinachowataka wanajeshi wa kikosi cha ulinzi wa rais kilichojaribu kufanya mapinduzi –...
MSAMA promotions wanatarajia kufanya tamasha la amani October mwaka huu lenye lengo la kuhamasisha na kudumisha amani kwa watanzania hususani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi na baada ya uchaguzi. Mratibu wa Msama Promotion HUDSON KAMOGA ameiambia EFM kuwa tamasha hilo litafanyika ndani ya mikoa kumi na kumalizika kabla ya uchaguzi huku akisisitiza kuwa watanzania wanatakiwa kuilinda amani na kuhakikisha nchi haiingii kwenye machafuko kutokana na...
SERIKALI imeshauriwa kuboresha mishahara ya walimu ili waweze kufanya kazi kwa bidii tofauti na ilivyo sasa ambapo wamekuwa wakifanya kazi wakiwa na mawazo yakutojua kesho yao. Rai hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Rais wa chama cha ngumi Tanzania MUTTA RWAKALE wakati wa mahafali ya 12 darasa la saba shule ya msingi UKWAMANI ambapo amesema kuwa kutokana na walimu kuwa na mishahara midogo inaweza kuchangia kufeli kwa wanafunzi kutokana na kutokuwa makini wakati wakufundisha huku wakiwaza namna ya kupata...
RAIS wa Bunge la Seneti nchini Nigeria, Bukola Saraki leo amefika kortini mjini Abuja ambako anakabiliwa na makosa 13 yanayohusu maadili. Makosa hayo ni pamoja na kuwahadaa wananchi kwa kigezo cha kutangaza mali yake pamoja na kukosa kutangaza mkopo, makosa ambayo ameyakanusha. Kesi dhidi yake inaendeshwa na jopo la mahakama kuhusu maadili na inahusu makosa anayodaiwa kuyatenda alipokuwa gavana wa jimbo la Kwara kati ya mwaka 2003 na...
VIONGOZI wa mapinduzi nchini Burkina Faso wamekataa kutii matakwa ya kusalimu amri na kutishia kupigana vita endapo watashambuliwa. Walinzi wa rais walioongoza mapinduzi walikuwa wamepewa hadi saa nne kwa saa za Afrika kuweka chini silaha na wanajeshi ambao walifika katika mji mkuu Ouagadougou. Hayo yamejiri huku marais wa mataifa ya Afrika Magharibi chini ya muungano wa Ecowas wakikusanyika Abuja, Nigeria kwaajili ya kufahamishwa na Rais wa Senegal Macky Sall kuhusu hatua zilizopigwa katika kutatua mzozo...