Wasikilizaji wa 93.7 EFM kisarawe jana walijipatia mafuta ya bure, baada ya bwana E kutoka EFM kupita eneo hilo na kugawa mafuta. Kila mwananchi wa eneo hilo aliye na chombo cha moto kama bajaji, pikipiki alifurahia huduma hiyo ya bure na yenye manufaa. Mchakato ulikuwa rahisi tu. Wasikilizaji walitakiwa kufika kituo cha mafuta alichopo bwana E, wakiwa na stika ya EFM, wanasikiliza EFM na bwana E kuwazawadia mafuta ya bureee. Huu ni mwanzo tu kwa wasikilizaji wa kisarawe. “Siku ya...
WAZIRI mkuu wa Croatia amesema nchi yake haiwezi kuwazuia wahamiaji wanaotaka kuelekea upande wa magharibi mwa Ulaya. Zoran Milanovic amesema Croatia itajaribu kuwaandikisha wakimbizi wengine zaidi kadiri itakavyowezekana. Mamlaka nchini humo zinasema jumla ya wahamiaji Elfu 11 wameingia nchini humo baada ya Hungary kufunga mpaka wake uliosababisha kufungwa kwa njia ya kuelekea nchi za...
SERIKALI ya Chile imetangaza hali ya dharura katika mji uliokumbwa na tetemeko la ardhi linaloaminika kuwa lenye nguvu zaidi. Watu 11 wamepoteza maisha na wengine milioni moja wameacha makazi yao baada ya kutokea kwa tetemeko hilo lenye ukubwa wa kipimo cha ritcha 8.3 kuleta athari siku ya Jumatano usiku. Tetemeko hilo ambalo ndilo kubwa zaidi duniani na la sita kutokea nchini humo kwa kipindi cha mwaka huu lilidumu dakika...
WANANCHI wa wilaya ya Mkuranga, mkoa wa Pwani wanatarajia kunufaika na mradi mkubwa wa usambazaji wa maji kufuatia kukamilika kwa zoezi la uchimbaji wa kisima cha maji chenye urefu wa mita 541 ambacho kina uwezo wa kuzalisha lita milioni 1.8 kwa siku. Akitoa taarifa za kukamilika kwa kazi ya uchimbaji wa kisima hicho mwakilishi wa kampuni ya kuchimba visima ya ZENTAS kutoka Uturuki nchini Tanzania dokta Mohammed Akbar amesema wanaendelea na majaribio ya kuyatoa maji kutoka ardhini jambo ambalo...
Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa imesema kuwa imesikitishwa na taarifa zisizo za kweli zilizotolewa katika vyombo vya habari kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, katika kipindi cha miaka 10 ya uongozi wake ametumia Shilingi trilioni 4 kwa ajili ya safari za kikazi nje ya nchi, ambazo ni wastani wa bajeti nzima ya wizara kwa miaka mitano 5. Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Mambo ya Nje na...
Mapato ya kilabu ya Manchester United yalianguka kwa pauni milioni 38 msimu uliopita baada ya kushindwa kufuzu katika mechi za vilabu bngwa Ulaya. Jumla ya mapato ya timu hiyo ni pauni milioni 395.2 chini kutoka pauni milioni 433.2 lakini fedha za ufadhili ziliongezeka na kuvunja rekodi kwa asilimia 14 na kufikia pauni milioni 154.9 . Hatua hiyo ilisababisha mapato ya watu wanaoingia uwanjani kushuka kwa asilimia 16 na kufikia pauni milioni 90.6 huku mapato ya utangazaji yakishukana kufikia pauni milioni...
RIPOTI mpya ya shirika la afya duniani WHO, na shirika la kuwahudumia watoto UNICEF imesema zaidi ya maisha ya watu milioni 6 yameokolewa kutokana na ugonjwa wa malaria katika muda wa miaka 15 iliyopita. Uingiliaji kati katika afya ya jamii barani Asia na eneo la mataifa ya kaukasus umekuwa na mafanikio makubwa katika kuudhibiti ugonjwa huo. Asilimia 80 ya vifo vitakavyotokana na Malaria mwaka huu inatarajiwa kuwa katika mataifa ya Afrika kusini ya...
KIKOSI cha walinzi wa rais kimeipindua Serikali ya mpito ya Burkina faso na kimetangaza katika runinga ya taifa kwamba kimevunja kile ilichokitaja kuwa serikali ya mpito isiyoambilika. Mwanachama wa kikosi hicho jenerali Gilbert Diendere ametajwa kuwa kiongozi mpya wa mpito. Mipaka yote imefungwa huku amri ya kutotoka nje ikiwekwa na Mkuu wa bunge amelitaka jeshi kuingilia kati ili kuzuia hatua hiyo aliyoitaja kuwa ya kundi dogo la...
KUTOKANA na tatizo la ajira hususani kwa vijana ambalo hivi sasa ni zaidi ya asilimia 13, wadau mbalimbali wa maendeleo kwa kushirikiana na watafiti nchini wanatarajia kuandaa mpango maalum utakaowasaidia vijana kuendana na soko la ajira ili waweze kupata ajira kwa urahisi. Wadau hao pamoja na baadhi ya vijana wanaotafuta ajira na wale waliojiajiri katika sekta mbalimbali wamekutana leo jijini Dar es salaam kwa lengo la la kujadili na kuangalia namna tafiti mbalimbali zinzavyoweza kusaidia kupunguza tatizo la ukosefu wa...
MTANDAO wa watetezi wa haki za binadamu nchini (THRDC) umetoa ripoti kuhusu utekelezaji wa mapendekezo 107 ya haki za binadamu yaliyofanyika na kuridhiwa na makundi mbalimbali. Hayo yamebainishwa katika mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam na mkurugenzi wa mtandao huo unaojumuisha asasi 80 zinazojiusisha na utetezi wa haki za binadamu, ONESMO OLENGURUMA ambapo amesema mchakato huu utakuwa endelevu ili kuhakikisha haki za binadamu zinapewa kipaumbele...
TETEMEKO kubwa la ardhi limeipiga Chile na kusababisha tishio la kutokea kwa tsunami, katika eneo lake la pwani na maeneo mengine ya bahari ya Pacific. Tetemeko hilo lenye ukubwa wa 8.3 katika vipimo vya ritcha, lilipiga maeneo ya pwani na kuenea kwa kilomita 250 kaskazini magharibi wa mji mkuu Santiago. Nchi hiyo imewahamisha wakazi milioni moja katika eneo la pwani, ambako tayari Rais wa Chile amethbitisha watu watano wamepoteza maisha baada ya tetemeko hilo...