WITO umetolewa kwa jamii kutowanyanyapaa Watu wenye albinism na badala yake kuwalinda na kuwathamini kama watu wa kawaida kabla ya baada ya uchaguzi kwa kuwa maisha yao yamekuwa hatarini mara kwa mara kutokana na fikra potofu na imani za kishirikina zinazosambazwa na baadhi ya watu. Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam katika hafla ya kukabidhi msaada wa carton 35 za mafuta ya kutunza ngozi na miwani 100 za jua zenye thamani ya shilingi milioni 2 kwa ajili kuwasaidia waweze...
WATANZANIA wametakiwa kuchangamkia nafasi mbalimbali zilizopo katika Sekta nzima ya TEHAMA kwa kujitokeza na kuthubutu kujifunza kushiriki kwa ufanisi katika kushindana au kusaidiana na kampuni zinazokuja kutoka nje kwa kuwa kwa kufanya hivyo kutasaidia kuboresha na kuendeleza Sekta hiyo kwa kuwa bado ingali changa. Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam katika kilele cha mkutano wa CAPACITY Africa ulioshirikisha nchi zaidi ya 65 na kampuni mbali kutoka Ulaya America na Asia kujadili na kujengeana uwezo kuhusu masuala mbalimbali ya TEHAMA...
POLISI wamewakamata watu watatu waliongia na bomu katika sehemu mpya ya maduka mjini Nairobi. Watu waliondolewa kwenye sehemu hiyo ya Garden City,ili kuwawezesha polisi kulitegua bomu hilo. Mkuu wa polisi katika mji wa Nairobi alimewaambia waandishi wa habari kwamba bomu hilo la kutengenezwa liligunduliwa na walinzi kwenye kituo cha usalama cha sehemu hiyo ya maduka. Mkuu huyo amearifu kuwa watuhumiwa hao watatu wanachunguzwa ili kubaini , iwapo wana uhusiano na magaidi, na hasa kundi la al-Shabab la nchini...
MAELFU ya waandamanaji waliokuwa wakipeperusha bendera za Uturuki wamevamia makao makuu ya chama kikuu cha Kikurdi cha HDP. Jengo hilo lililoko katika mji mkuu wa Ankara baada ya kuvamiwa lilichomwa moto. Waziri mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu amelaani vikali mashambulizi na uvamizi huo katika ofisi za kisiasa na hata kwa nyumba za habari na ametoa wito wa kusitisha...
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA, kimeahidi kutetea haki za wavuvi waliouawa na viboko wakiwa wanavua samaki kwenye ziwa Babati, bila kulipwa fidia endapo kitapewa ridhaa na wananchi ya kuingia madarakani. Ahadi hiyo imetolewa na Mgombea udiwani wa Kata ya Bagara Wilayani Babati Mkoani Manyara, Nicodemus Tlaghas ambaye amesema ni kwa muda mrefu wananchi wa eneo hilo walikosa mwakilishi wa kuwasemea na kuwatetea pindi wanapopata matatizo. Mgombea Urais anayeungwa mkono na vyama vya Ukawa Edward Lowasa leo atakuwa Zanzibar wakati...
MGOMBEA mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu ameanza ziara yake mkoani Ruvuma akiinadi ilani ya chama hicho huku akiahidi neema kwa wakulima wa kahawa na mahindi wa mkoa huo. Suluhu ambaye amehutubia mikutano mitatu katika majimbo mawili ya mkoa wa Ruvuma, Jimbo la Nyasa na Mbiga Vijijini, akizungumza katika mikutano yake amesema serikali itakayoundwa na CCM endapo itashinda itahakikisha inashusha umeme katika vijiji vyote vya mkoa huo kwa awamu ili kuchochea maendeleo ya...
Serena williams amemshinda dada yake Venus william katika mashindano ya US Open na kuzidi kusonga mbele katika ushindi mara mbili wa kalenda ya kwanza ya Grand Slam. Serena ambaye ni nambari moja duniani amshinda dada yake kwa seti tatu ya 6-2 1-6 6-3 zilizompa upenyo wa kuweza kuingia kwenye mashindano ya nusu fainali huko New York,Marekani. Katika hatua ya nusu fainali,serena atachuana na mwanadada wa nchini Italia Roberta Vinci siku ya alhamisi wiki...
Wayne Rooney ameivunja rekodi ya upachikaji mabao ya muda wote katika timu ya taifa ya England, iliyokuwa ikishikiliwa na Sir Bobby Charlton katika mchezo dhidi ya Switzerland,uliopigwa uwanjani Wembley wa kufuzu kwa michuano ya ulaya mwaka 2016. Nahodha huyo wa England aliifikia rekodi ya Charlton ya magoli 49,wakati alipofunga dhidi ya San Marino siku ya Jumamosi. Alikua pia katika mchezo dhidi ya Switzerland siku ya Jumanne ambapo alifikisha goli la 50 na kufuta historia hiyo iliyodumu kwa miaka...
JESHI la Nigeria limepiga marufuku matumizi ya farasi na punda katika jimbo la Kaskazini Mashariki la Borno, kama sehemu ya juhudi za vita dhidi ya Boko Haram. Imebainika kuwa Kundi hilo limekuwa likitumia farasi kutekeleza mashambulizi dhidi ya wanavijiji huku jeshi la Nigeria likionekana kupata mafanikio katika vita vyake dhidi ya Boko Haram. Taarifa zinasema kuwa tayari kumepigwa marufuku kwa matumizi ya pikipiki ambazo zilikuwa zikitumiwa na wanamgambo wa Kiislamu wa Boko Haram kuwasafirisha wapiganaji wake katika...
KIONGOZI wa kanisa katoliki Duniani Papa Francis anatarajia kurahisisha taratibu zinazoruhusu wafuasi wa kanisa hilo waliooana kutoa talaka na kuolewa tena huku wakibakia kuwa wafuasi katika kanisa hilo. Papa aliunda tume ya wanasheria wa kanisa mwaka jana kupiga msasa mbinu ya kurekebisha taratibu hizo zinazoruhusu wanandoa kuachana na kupunguza gharama. Bila sheria hiyo wanandoa wa kikatoliki wanaotalikiana na kuolewa upya hutazamwa kama wazinifu na hawaruhusiwi kushiriki kwenye huduma zinazotolewa na...
ASKOFU Mkuu wa kanisa la Ufufuo na uzima Josephat Gwajima amekanusha taarifa zilizotolewa dhidi yake na aliyekuwa katibu mkuu wa chama cha Demokrasia na maendeleo-CHADEMA-dokta Wilbroad SLaa kuwa yeye alimpa taarifa kwamba maaskofu 30 wa kanisa katoliki walipewa fedha na mgombea urais kupitia vyama vinavyounda umoja wa Katiba ya wananchi ukawa mheshimiwa Edward Lowasa ili wamuunge mkono katika harakati zake. Askofu Gwajima ameyasema hayo leo Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya taarifa hizo ambapo...