WAOKOAJI Kaskazini mwa Ufilipino wameendelea na kazi ya kuchimbua ardhini kwa lengo la kutafuta mamia ya wachimba madini waliofukiwa baada ya kukumbwa na kimbunga. Hali hiyo imekuja kufuatia zaidi ya watu kumi na tano kuripotiwa kufariki dunia na wengine kadhaa hawajulikani walipo kutokana na kimbunga hicho kikubwa. Hata hivyo mmomonyoko wa udongo ulisababishwa na kimbunga ambacho kilifukia migodi mitatu kaskazini mwa kisiwa cha Luzon ambapo kwa sasa kimepungua kasi na kinaelekea Japan katika kisiwa cha...
JUKWAA la Tiba asili Tanzania limewaasa wananchi kuithamini na kuendeleza Amani iliyopo kwa kuepuka kujihusisha na vishawishi vitakavyosababisha kuvunjika kwa Amani. Wito huo umetolewa Jijini Dar es salaam na mwenyekiti wa Jukwaa hilo Bonaventure Mwalongo wakati akizungumza na kituo hiki juu ya umuhimu kwa watanzania kushiriki katika kuilinda na kuitetea Amani. Mwalongo amebainisha kuwa ni muda muafaka sasa kwa kila mtu bila kujali itikadi ya chama, dini au kabila kushirikiana kwa pamoja katika kila suala muhimu na lenye...
IMEELEZWA kuwa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, yanatarajia kusaidia kuboresha matundu ya vyoo katika shule 10 zilizopo manispaa ya Moshi na wilaya ya Moshi vijijini. Hayo yamesemwa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo –MASHIRIKA YA UN KUSAIDIA UJENZI WA MASHIMO YA VYOO KWENYE SHULE 10 MOSHIUNDP– nchini Alvaro Rodriguez katika hafla ya kuweka msingi kwa ajili ya ujenzi wa matundu 18 ya vyoo katika shule ya msingi Kiboriloni wilayani...
Bondia mwenye tambo zaidi duniani Floyd Mayweather amefanikiwa kununua gari la ndoto zake. Gari hilo ambalo limekua likitajwa na bondia huyo toka mwezi June kwa sasa lipo kwenye mikono yake baada ya kukamilisha malipo yote na kuwa mmiliki halali wa gari hilo la kipekee na la thamani zaidi duniani Gari hiyo aina ya Koenigsegg CCXR Trevita linalokwenda 0-60 kwa sekunde 2.9 na kutembea umbali wa miles 250 kwa saa Mwenyewe Floyd amelipa jina la Hyper car huku gharama za manunuzi...
Meneja wa klabu ya Everton, Roberto Martinez ameelezea mpango wake wa kufanya usajili mpya kwa wachezaji watatu kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili. Miongoni mwa wachezaji anaowatazama meneja huyo ni mlinzi wa klabu ya River Plate, Ramiro Funes Mori, 24 Lakini pia Everton wamekuwa na mazungumzo na klabu ya Dynamo Kiev juu ya kumchukua mshambuliaji Shakhtar Donetsk’s Bernard. Lakini pia Everton imeonyesha kuvutiwa na mshambuliaji wa Uruguay Leandro...
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amesema matokeo ya timu yake dhidi ya West Brom yatawanyima raha wabaya wao. Ameyasema hayo baada ya kupata ushindi wa kwanza tokea msimu mpya wa ligi ya England ianze. Katika mchezo huo uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita, Chelsea iliibuka kidedea kwa jumla ya bao 3-2 dhidi ya West Brom na kushuhudia nahodha wake John Terry akilimwa kadi nyekundu katika dakika ya 54 ya mchezo baada ya kumchezea vibaya mshambuliaji wa West Brom Salomon Rondon. Ushindi...
Manchester City imefanikiwa kurejea kileleni kwenye Premier League kufuatia ushindi wao dhidi ya klabu ya Everton. Ushindi huo wa ugenini ulifanikishwa na Aleksandar Kolarov pamoja na Samir Nasri na kuufanya mchezo kumalizika kwa matokeo ya 2-0. City walikuwa awali wameshinda mechi moja pekee kati ya sita walizochezea Goodison Park – ushindi huo wa pekee ukiwa kwenye safari yao ya kushinda taji 2014. Kutwaa tena taji hilo ndilo lengo lao msimu huu baada yao kutumia pesa nyingi tena kujengwa upwa kikosi,...
Leo kipindi pendwa cha michezo Tanzania cha E SPORTS kimefikisha mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake Katika kusherehekea siku hii muhimu kikosi cha watangazaji wa michezo ndani ya Efm waliungana na wadau wa Stars supporters kusherehekea siku muhimu katika historia ya mapinduzi ya michezo nchini Timu hii machachari kabisa inaundwa na Maulid Kitenge, Omary Katanga, Ibrahim Masoud, Sud Mkumba, Mussa Kawambwa, Oscar Oscar, Francis Mhando, Yusuph Mkule pamoja na Dokta...
KIONGOZI wa Korea kaskazini Kim Jong-Un ameamuru majeshi yaliyoko mstari wa mbele kuwa tayari kwa vita leo, wakati hali ya wasi wasi ya kijeshi na Korea kusini ikiongezeka. Hali hiyo inafuatia mashambulizi ya makombora toka kila upande katika eneo lenye silaha nzito la mpakani. Shirika rasmi la habari la Korea kaskazini KCNA limesema hatua hiyo imekuja wakati wa mkutano wa dharura uliofanyika jana usiku wa kamisheni kuu yenye madaraka makubwa ya kijeshi...
WAZIRI MKUU wa Ugiriki Alexis Tsipras amejiuzulu na kuitisha uchaguzi ufanyike mapema. Hatua hiyo inaonekana kuwa juhudi za kuzima uasi ndani ya chama chake cha Syriza na kuimarisha uungwaji wake mkono wa mpango wa tatu wa uokozi wa uchumi wa nchi hiyo inayokabiliwa na madeni, ikiwa ni hatua ya kwanza ambayo imeidhinishwa na mawaziri wa fedha wa mataifa ya kanda ya euro wiki hii....
WAGOMBEA mbalimbali wa nafasi za urais leo wamerejesha fomu zao katika Tume ya Uchaguzi- NEC, tayari kwa uzinduzi wa Kampeni kuelekea uchaguzi Mkuu oktoba 25 mwaka huu. Akizungumza mara baada ya kurejesha fomu yake, mgombea kupitia chama cha mapinduzi- CCM Dokta John Magufuli amesema ametimiza matakwa yote ya kisheria na sasa kilichobaki ni uzinduzi wa kampeni. Kwa upande wake mgombea wa nafasi ya urais kupitia vyama vinavyounda umoja wa katiba UKAWA Edward Lowasa, amewataka viongozi na wanachama kumuunga...