WAHAMIAJI wengi zaidi wanaendelea kuwasili nchini Bulgaria licha ya kuongeza ulinzi katika mipaka yake, kuweka kamera na vifaa vitakavyotambua nyendo za watu na kurefusha uzio wa usalama wenye urefu wa kilometa 160 ambao umejengwa kwenye mpaka wake na Uturuki. Data rasmi zinaonyesha kuwa kiasi cha watu elfu 25,000 wamejiandikisha kama wakimbizi nchini Bulgaria katika miaka miwili iliyopita, hiyo ikiwa ni idadi na ile iliyoandikishwa katika muda wa miongo miwili iliyopita....
UTAFITI umeeleza kuwa Watu wanaofanya kazi kwa saa nyingi wako hatarini kupata kiharusi,utafiti huo ulifanywa kwa zaidi ya watu laki tano. Takwimu zilizochapishwa kwenye jarida la kitabibu, Lancet, linaonyesha upo uwezekano wa ongezeko la hatari ya ugonjwa huo kwa watu wanaofanya kazi zaidi ya muda wa kawaida. Wataalam wanasema watu wanaofanya kazi kwa saa nyingi zaidi wawe na utaratibu wa kupima kiwango cha msukumo wa damu na kwamba kufanya kazi kwa muda mrefu zaidi kuliko kawaida na kukaa kwa...
UONGOZI wa Kituo cha kulelea watoto wadogo wakiwemo yatima na waliotelekezwa na wazazi, Msimbazi centre wameiomba serikali, jamii na Taasisi mbalimbali kutambua uwepo wa watoto hao. Akizungumza na EFM jijini Dar es Salaam mlezi wa kituo hicho sista Anna Francis amesema miongoni mwa watoto waliopo hapo ni wale waliotupwa na mama zao pindi wanapojifungua kwa visingizio mbali mbali. Aidha sista Anna amesema kuwa mbali na kutopata misaada kutoka sehemu mbalimbali kwa sasa kituo hicho kina watoto arobaini na...
SERIKALI imeombwa kulipatia Hati Miliki soko la Ndizi na Matunda lililopo mabibo urafiki jijini dar es salaam kutokana na soko hilo kukosa ufadhili wa mikopo katika benki kwa sababu ya kukosa hati hiyo. Akizungumza na Efm Mwenyenye kiti wa Soko hilo Bwana KIBWANA ALFAN PAZI amesema kuwa endapo watapata hati miliki ya soko hilo itawasaidia kupata wafadhili kutoka sehemu mbalimbali watakao wawezesha katika biashara yao. PAZI amebainisha kuwa vijana wengi wameweza kujiajili wenyewe kupitia nafasi wanazo zipata katika...
KATIKA hali isiyo ya kawaida mtoto mwenye umri wa miaka 12, Neema Maginga katika Manispaa ya Musoma Mkoani Mara amefariki dunia na wakati wa maandalizi ya mazishi yake marehemu akabadirika kutoka umbo lake la kawaida na kuwa mzee mwenye umri unaokadiliwa kuwa miaka( 60). Akizungumzaa na EFM katika eneo la tukio mama mzazi wa marehemu amesema ni katika hali isiyofahamika wakati wa maandalizi ya kwenda kupumzisha mwili wa marehem ndipo ilipotokea sitofahamu katika mwili wake na kubadilika katika maumbo tofauti...
Ligi kuu Tanzania bara kuanza kutimua vumbi tarehe 12 mwezi wa 9. Mechi za ufunguzi zitakuwa kama ifuatavyo Jumamosi. Ndanda vs mgambo – Nangwanda Cjaona African sports vs simba – mkwakwani Tanga. Maji maji vs jkt ruvu – Songea Azam vs Tanzania prisons – Azam Comlex Stand utd vs mtibwa – Kambarage Kagera Toto afrika vs Mwadui – Kirumba Mwanza Jpili. Yanga vs coast unioni –...
BUNGE la Ujerumani limeanza kujadili kuhusu maamuzi ya mwisho ya kulipwa kwa deni la Ugiriki wakati ambapo kansela Angela Merkel anakabiliana na changamoto ya upande wa upinzani na wale wa chama chake kujadili juu ya deni la dola bilioni tisini na nne. Mambo ambayo yalipewa kipaumbele na wabunge wa upinzani ni kuhusiana na deni la ugiriki kulipwa na Ujerumani huku kukiwa na wasiwasi juu ya maamuzi ya shirika la fedha duniani IFM, kutoshiriki katika kulilipa deni hilo. Waziri wa fedha...
RIPOTI kutoka nchini Nigeria zinasema kuwa karibu watu 60 huenda waliuawa wakati wa shambulizi katika kijiji kimoja kaskazini mashariki mwa nchi hiyo lililoendeshwa na watu wanaoshukiwa kuwa wanachama wa na Boko Haram. Shambulizi hilo lilitokea katika jimbo la Yobe lilifanyika Alhamisi iliyopita na habari hizo zimepatikana kutoka kwa wale walionusurika. Walioshuhudia wamesema kuwa wanamgambo wa Boko Haram waliwasili katika kijiji hicho wakitumia pikipiki ambapo walianza kuwafyatulia watu...
CHUO cha Kilimo cha Sokoine SUA kinatarajia kugeuza kitivo cha Kilimo cha chuo hicho kuwa Chuo cha Kilimo rasmi kitakachokuwa kinatoa mafunzo ya Kilimo cha kawaida na Kilimo cha Biashara ili kuboresha mfumo wa utawala na utendaji uwe wa kifanisi zaidi. Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam leo Mgeni Rasmi Naibu Makamu Mkuu wa SUA Utawala na Fedha Profesa Yonika Ngaga amesema lengo hasa ni kuboresha taaluma kwa kurekebisha mfumo mzima wa uendeshaji, usimamizi na utendaji wa...
JAMII imeombwa kutowadharau na kutowanyanyapaa Wagonjwa wa Siko Seli na badala yake kuwasaidia kutibu hali zao kwa kuwa asilimia 13 ya Watu wote Nchini wana vinasaba vya ugonjwa huo ambapo Tanzania imetajwa kuwa nchi ya 5 duniani kuwa na Wagonjwa wengi zaidi. Wito huo umetolewa leo katika Uzinduzi wa Mpango wa Miaka 3 wa kupima Watoto wachanga Siko Seli utakaoenda Sanjari na Bonanza la Michezo kuadhimisha Mwezi wa kuongeza uelewa juu ya ugonjwa huo uliondaliwa na Taasisi binafsi ya...
MAREKANI imeanza mazungumzo na mataifa mengine wanachama kwenye Umoja wa Mataifa, juu ya uwezekano wa kuiwekea vikwazo Sudan Kusini, endapo serikali itashindwa kusaini makubaliano ya amani na waasi, ndani ya wiki mbili zijazo. Mshauri wa usalama wa Rais Barack Obama, Susan Rice, amesema Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini kwa mara nyingine ameivuruga nafasi ya upatikanaji wa amani. Juzi Jumatatu, rais huyo wa Sudan Kusini aliishangaza Marekani na mataifa mengine yanayosimamia mazungumzo ya amani ya nchi yake, kwa kukataa kusaini...