Muigizaji Tracy Morgan amerejea kazini, atakuwa akitangaza moja kati ya show za kwanza katika kipindi cha Saturday Night Live. Kituo cha NBC kimetangaza mastar wa kwanza watakaoongoza kipindi hiki ambao ni Miley Cyrus, Amy Schumer, and Tracy. Kupitia akaunti yake ya Twitter ametweet akionyesha kuwa mwenye furaha na imara kabisa kiafya akiwa tayari kushiriki kwenye SNL Tracy amekuwa kimya kwa muda baada ya kupata ajali ya gari mwaka mmoja...
Muigizaji maarufu duniani Terrence Howard amesema amebadilika saana baada ya kutarakiana na aliyekuwa mpenzi wake Michelle Ghent. Terrence ambae kwa sasa anatamba na series ya Empire amesema alipokuwa pamoja na Michelle kwenye mahusiano amejikuta akiingia kwenye matumizi ya dawa za kulevya ikiwa pamoja na uvutaji wa bangi na cocaine. Terrence amesema kuwa yeye na Michelle wamekuwa wakitumia aina hizo za dawa za kulevya na kutazama sinema za pono. Muigizaji huyu amesema amebadilika baada ya kuachana na mpenzi...
Klabu ya soka ya Athletic Bilbao imetwaa taji la Super Cup Bilbao wametwaa ubingwa huo baada ya miaka 31 katika mchezo uliochezwa katika dimba la Nou Camp.Katika mchezo wa fainali ya kwanza kwenye dimba la San Mames Bilbao walipata ushindi wa mabao 4-0. Mshambuliaji Lionel Messi ndio alianza kuiandikia timu yake bao dakika 44 kabla ya Aritz Aduriz kuisawazishia timu yake katika dakika ya 81 ya mchezo na na kuihakikishia ubingwa huo kwa jumla ya mabao 5-1. Beki wa Barca...
klabu ya soka ya Simba Sc imetangaza rasmi kuachana na mlinda mlango Ivo Mapunda Akizungumza katika kipindi cha Sports Headquarters Mapunda amesema uongozi wa klabu hiyo umefikia maamuzi hayo huku wakimpa sababu kuu ni kuwa hakuonyesha ushirikiano kuingia katika mkataba mpya na klabu hiyo . Baada ya maamuzi ya kuachana na mlinda mlango huyu Simba pia imemtaka Ivo mapunda arejeshe kiasi cha pesa alizolipwa na klabu hiyo ambapo Ivo ametangaza dhamira yake pia kurejesha pesa...
RAIS Abdel Fattah al-Sisi wa Misri, ameidhinisha hatua mpya za kupambana na ugaidi, ambazo zimezua utata zenye nia ya kuimarisha uwezo wa taifa hilo kukabiliana na maasi ya waislamu wenye itikadi kali. Wale watakaopatikana na hatia ya kubuni au kuongoza makundi ya kigaidi, watakabiliwa na adhabu ya kifo au kifungo cha miaka kumi au maisha jela. Makundi ya kutetea haki za kibinadamu yamesema kuwa rais Abdel Fattah al-Sisi, atatumia sheria hizo mpya kuwafungia wapinzani wake na pia kuwazima waasi au...
PANDE zinazozozana nchini Sudan Kusini zinafanya mazungumzo nchini Ethiopia hii leo ikiwa ni siku ya mwisho ya mazungumzo ya amani kabla ya vikwazo vya kimataifa kuwekewa pande zote. Lakini serikali ya Sudan Kusini pamoja na waasi wamesema huenda wakahitaji muda zaidi kutatua maswala kama vile mgawanyo wa madaraka katika serikali ya mpito. Mwakilishi maalum wa Muungano wa Ulaya, Alexander Rondo, ameonya kuwa ucheleweshwaji wa kufikia makubaliano hautavumiliwa. Marais wa Uganda, Kenya na Ethiopia pia wanashiriki mazungumzo...
WAZIRI wa Nishati na madini Mheshimiwa George Simbachawene, amewataka Wanafunzi 22 wanaokwenda nchi ya Jamhuri ya Watu wa China kusomea maswala ya Mafuta na Gesi, chini ya ufadhili wa nchi hiyo, kuzingatia masomo watakayopata huko ili waweze kuwa na chachu ya kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili Tanzania katika sekta ya nishati. Ufadhili huo ni ufadhili wa tatu nchini kufuatia kuanza kwa ufadhili huo mwaka 2013, ambapo awamu ya kwanza walipelekwa wanafunzi nane, mwaka 2014 wanafunzi 10 na mwaka huu wanafunzi...
IMEELEZWA kuwa Taifa linaweza kuwa na mfumo mzuri zaidi endapo litahakikisha kuwa Vijana wanauwezo wa kuajiriwa, kujiajiri au kuwa na ufundi wa kufanya mambo yao wenyewe na sio wawe wanasoma tu na kupata vyeti ambavyo wanashindwa kufanya navyo kitu chochote. Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Katibu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue wakati wa ufunguzi wa warsha ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi iliyoshirikisha wadau mbalimbali wa Elimu na Taasisi binafsi kwa lengo kuunda mkakati wa...
MIILI ya watu imeendelea kuopolewa zaidi katika eneo lilitokea mripuko katika mji wa bandari wa Tianjin, nchini China, na kufanya idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na mkasa huo kufikia 122. Hayo yanafanyika wakati wataalamu wakiharakisha kuondosha kemikali hatari katika eneo hilo na waendesha mashitaka wanajitayarisha kuwachunguza wale wote waliohusika na maafa hayo. Zaidi ya watu 700 walijeruhiwa na wengine 95, wakiwemo wazima moto...
VIONGOZI wa Mataifa 15 ya Jumuia ya Nchi za Kusini mwa Afrika- SADC, wanatarajia kukutana leo nchini Botswana katika Mkutano wao wa Mwaka. Mkutano huo unafanyika wakati eneo hilo linakumbwa na upungufu wa chakula ambapo watu wanaokadiriwa kufikia milioni 27.4 kutoka idadi ya jumla ya wakazi 292, wa eneo hilo wanategemea msaada wa chakula ifikapo mwishoni mwa mwaka huu. Msemaji wa Shirika la Mpango wa chakula wa Dunia-WFO, David Orr, ameliambia shirika la habari la Ufaransa-AFP kuwa Zimbabwe na Malawi...
UMOJA wa Katiba ya wananchi-UKAWA leo unatarajiwa kuweka hadharani mgawanyo wa majimbo ya kugombea katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu. Tayari Umoja huo umeshamsimamisha Mgombea wa Kiti cha Lowasa kuwa ni Edward Lowasa na kabla ya kumsimamisha tayari Viongozi wakuu wa Ukawa walishathibitisha kwamba walifikia makubaliano kwa zaidi ya asilimia 95 kuhusu mgawanyo wa viti vya Ubunge na kwamba mazungumzo zaidi yalikuwa yanaendelea kuhusu majimbo...