MTOTO wa kiume mwenye umri wa miezi saba amekatwa sehemu zake za siri na bibi yake wa kambo. Inaelezwa kuwa Mtoto huyo amefanyiwa ukatili huo nyumbani kwao Nyamaguku wilayani rorya wakati mama yake akiwa ameenda kutafuta kuni na tayari amepelekwa katika Hospital ya Bugando Mkoani Mwanza kwa ajili ya matibabu. Mama wa mtoto huyo Rehema Marwa amesema wakati tukio hilo linatokea hakuwepo nyumbani, aliporejea ndipo alipopata taarifa kuwa mtoto wake amekatwa sehemu za...
Meneja wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho ametoa utetezi kufuatia maamuzi yake ya kmtoa nahodha John Terry na nafasi yake kuchukuliwa na Kurt Zouma katika kipindi cha mapumziko kwenye mchezo kati yao na klabu ya Manchester City. Chelsea ilipokea kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Manchester City siku ya jumapili kwenye mchezo wa ligi kuu nchini England. Katika utetezi wake bosi wa Chelsea amethibitisha kuwa Terry hakupata majeraha bali alimtoa kwa sababu za kimchezo. “ilikuwa wazi kwenye mipango yangu kumuingiza...
Nyota namba tatu kwa ubora wa mchezo wa tenesi muingereza Andy Murray ametwaa ubingwa wa michuano ya Rogers Murray ametwaa ubingwa huu baada ya kumshinda mpinzani wake Novack Djokovic kwa seti 6-4 4-6 6-3 katika mchezo uliochukua muda wa saa tatu. Kwa ushindi huu Murray anavunja mwiko wa kupoteza mapambano manane dhidi ya Novack ambae anashilikia nafasi ya kwanza kwa ubora. Murray amemzawadia ushindi huo kocha wake Amelie Mauresmo,aliyepata...
SERIKALI ya Kenya inatarajiwa kuharibu boti moja iliyopatikana imebeba takriban kilo 7 za mihadarati aina ya Heroini. Boti hiyo inayoitwa ‘Baby Iris’ ilikamatwa na polisi kwa tuhuma za ulanguzi wa mihadarati katika bahari ya Kenya huko Mombasa na itaharibiwa kulingana na sheria za Kenya. Ripoti ya polisi inasema kuwa ‘Baby Iris’ inamilikiwa na bwenyenye mmoja raia wa Uingereza na kwamba Jeshi la wanamaji la Kenya ndilo lililokabidhiwa jukumu hilo la...
WAFUASI wa rais Yoweri Museveni wamewashambulia wafuasi wa Amama Mbabazi nyumbani kwake katika kitongoji kimoja cha mji mkuu wa Kampala. Vijana hao waliokuwa wamevalia shati zenye maandiko ya kumuunga mkono rais Museveni walishambulia boma la kiongozi huyo ambaye ameahidi kuwania kiti cha urais dhidi ya rais Museveni katika uchaguzi mkuu ujao. Vijana hao walimtuhumu waziri huyo mkuu wa zamani kwa kuwapa ahadi hewa kuwa angewapa...
KUFUATIA Serikali kupitisha sheria ya kodi ya ongezeko la thamani ya Mwaka 2014 iliyoanza kutumika rasmi Julai Mosi Mwaka huu, Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA imeandaa semina na wadau mbalimbali wa Michezo kujadili utekelezaji wa kodi hiyo katika sekta ya michezo kwa kuwa Sekta hiyo inamchango mkubwa wa mapato ya Serikali endapo itatumika vizuri. Semina hiyo ya siku moja imewashirikisha TFF na Wadau mbalimbali wa Michezo kwa lengo la kutoa mafunzo maalum juu ya sheria mpya ya kodi ya ongezeko la...
JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ limekanusha taarifa zinazo sambaa kwenye Mitandao na vyombo vya habari kuhusu Jeshi hilo kuwataka Maafisa na Askari kuwasilisha kadi zao za kupiga kura na kuchukua namba za kadi hizo. Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Habari na Mahusiano kwa Umma wa JWTZ KANALI NGEMELA LUBINGA amesema kuwa habari hizo ambazo zilisemwa na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ubungo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA JOHN MNYIKA na kusambaa katika vyombo...
MIEZI miwili baada ya kukamatwa na kuzuiliwa nchini Uingereza mkuu wa ujasusi wa Rwanda Luteni Jenerali Karenzi Karake hatimaye amerejea nchini Rwanda jana. Kiongozi huyo alikamatwa Uingereza mwezi Juni mwaka huu baada ya kukamilisha ziara ya kikazi nchini humo kwa tuhuma za uhalifu wa kivita. Jenerali Karenzi ni mmoja wa maafisa 40 wa jeshi la Rwanda ambao majina yao yapo kwenye waranti uliotolewa na jaji wa Uhispania kutaka wakamatwe kutokana na tuhuma za uhalifu wa kivita wakati wa mauaji ya ...
RAIS wa zamani wa Cuba Fidel Castro ametimiza umri wa miaka 89 kwa kuandika barua ya wazi kwa taifa lake. Barua hiyo ilichapishwa katika gazeti la serikali la Granma ambapo hajazungumzia lolote kuhusu ufunguzi wa ubalozi mpya wa Marekani jijini Havana utakavyofanya kazi na waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry. Badala yake ameituhumu Marekani kwa kuisababishia hasara ya mamilioni ya dola baada ya miaka mingi ya vikwazo vya biashara baina ya nchi hizo...
WANANCHI Visiwani Zanzibar wametakiwa kufuata utaratibu wa kukata miti, ili kuepukana na uharibifu wa mazingira. Mkuu wa wilaya ya Magharibi ‘B’ Unguja Ayoub Muhammed amesema wilaya ya Magharibi imekuwa na kasi ya kukatwa miti kiholela hali ambayo inachangia uharibifu wa mazingira. Amefahamisha kuwa baadhi ya wananchi wamekuwa na visingizio vya kuwa wajasiriamali na kwamba wanalazimika kukata miti jambo ambalo ni kinyume na...
CHAMA cha wananchi- CUF Mkoa wa Morogoro kimesema kikipata ridhaa ya wananchi kupitia ukawa kitahakikisha kinasimamia migogoro ya wakulima na wafugaji kwa kuweka bayana mipaka ya vijiji vya wakulima na wafugaji ili kuondoa malalamiko ya muingilano wa shughuli za kilimo na ufugaji. Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara muda mfupi baada ya kuchukua fomu ya kugombea ubunge jimbo la kilosa kupitia ukawa mwenyekiti wa chama cha wananchi cuf wilaya ya morogoro mjini Abedi Mlapakolo ameeleza idadi kubwa ya wakulima na wafugaji...