Kiungo wa zamani wa timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars, Orsbone Monday amepotea baaada ya kuchukuliwa na watu wasio julikana huku wakijitambulisha kwao kuwa ni maafisa wa polisi. Mchezaji wa timu ya Tusker FC ya Kenya ameripotiwa kupotea huku taarifa zaidi zikieleza kuwa ametekwa nyara na watu wasiojulikana. Mama mzazi wa Orsbone ameripotiwa akiesema kwamba mtoto wake alifuatwa nyumbani kwake na watu 10 wasiojulikana ambao walijitambulisha kuwa ni polisi kutoka kituo cha Kenyatta ambao hawakuruhusu namba za magari waliyoenda...
Mshambuliaji wa klabu ya Manchester City, Edin Dzeko amejiunga na klabu ya Roma ya Italia kwa mkopo wa muda mrefu huku uhamisho wake ukitazamwa kama uhamisho wa kudumu, ilitangaza klabu ya Manchester City ya England. Mshambuliaji huyo mwenye asili ya Bosnia alijiunga na Man City akitokea Wolfsburg mwaka 2011akiwa na rekodi ya kushinda magoli 72 katika michezo yake 189. Katika msimu uliopita mchezaji huyu hakuhusishwa sana na michezo ya klabu ya Man City hali iliyopelekea apate ushindi wa magoli sita...
WAZIRI MKUU wa Serikali ya Libya inayotambulika kimataifa, Abdullah al-Thani amejiuzulu katika hatua ya kushangaza jana, saa chache baada ya mazungumzo ya amani kati ya makundi hasimu ya nchi hiyo kuanza. Wakati wa kipindi cha mazungumzo katika televisheni kilichokuwa kikirushwa moja kwa moja, waziri mkuu Al-Thani alipambana na maswali makali ya watu wenye hasira ambao wameilaumu serikali yake kwa kushindwa kutoa huduma muhimu kama umeme na usalama ...
WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry amesema iwapo Marekani itajitoa kutoka katika makubaliano ya nyuklia na Iran na kutaka washirika wake watekeleze hatua za vikwazo vya Marekani, kutakuwa na kitisho cha kupotea imani na uongozi wa Marekani pamoja na kupoteza mwelekeo wa sarafu yake ya dola. Akitetea makubaliano ya Julai 14 yaliyoafikiwa mjini Vienna kati ya Iran na mataifa makubwa yenye nguvu duniani, Kerry ametoa utetezi mpya katika ...
KATIKA kuadhimisha siku ya Vijana Duniani, Serikali imewataka Vijana nchini kujitokeza, kujitolea pamoja na kubadilisha fikra zao na kuwa na fikra chanya ili kuhakikisha kuwa badala ya kuachwa nyuma katika maendeleo, wanakuwa mstari mbele katika kuleta maendeleo na mabadiliko nchini. Akizungumza katika hafla hiyo jijini Dar es salaam leo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel amesema, Serikali kupitia Wizara hiyo itashirikiana na Vijana kwa karibu kuhakikisha kuwa Vijana wanawekewa...
WIZARA ya afya na ustawi wa jamii imesema kuwa mpaka sasa hakuna uthibitisho wowote juu ya kifo cha mgonjwa mwenye umri wa miaka 39 kutoka katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu mkoani Kigoma ambacho kimetokana na ugonjwa wa Ebola. Taarifa ya ufafanuzi iliyotolewa na kitengo cha awasiliano kutoka wizarani hapo imeelezwa kuwa sampuli ya mgonjwa huyo imechukuliwa na kupelekwa kwenye maabara ya taifa ya jamii wizara ya afya kwa uchunguzi zaidi ili kubaini chanzo cha ugonjwa...
MAAFISA wa Uholanzi wanaochunguza kuangushwa kwa ndege ya Malaysia yenye nambari ya safari MH17, wametangaza kwamba wamepata kitu ambacho kinaweza kuwa kipande cha roketi aina ya BUK inayotengenezwa na Urusi, katika eneo ilikoanguka ndege hiyo Mashariki mwa Ukraine. Tangazo hilo lililotolewa jana ni la kwanza kutoka kwa maafisa hao, linalohusisha ushahidi wa matumizi ya roketi katika kuangushwa ndege hiyo. MH17 iliangushwa tarehe 17 Julai mwaka jana katika eneo la Mashariki mwa Ukraine eneo linalokumbwa na mzozo, na kuuwa watu wote...
RAIS wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameapa kutolegeza kamba katika operesheni ya kijeshi inayoendelea dhidi ya wanamgambo wa Chama cha Wafanyakazi wa Kikurdi, PKK. Erdogan ameyasema hayo katika hotuba yake kwenye sherehe ya kijeshi, wakati serikali yake ikianzisha mashambulizi mapya dhidi ya waasi wa kikurdi ndani ya mipaka ya Uturuki. Wiki hii ndege za jeshi la Uturuki zimefanya mashambulizi kuvilenga vituo 17 vya wakurdi katika mkoa wa Hakkari, katika juhudi mpya dhidi ya chama cha PKK ambacho kimepigwa...
KUTOKANA na umuhimu na wingi wa Matumizi ya Mafuta kwenye Magari na Mitambo ya serikali katika utekelezaji wa majukumu yake pamoja na gharama kubwa wakala wa huduma ya ununuzi serikalini GPSA umeamua kusimamia mfumo wa udhibiti wa mafuta katika visima na magari ya serikali. Akizungumza na kituo hiki Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa huduma hiyo NAFTAL SINGWEJO amesema kuwa lengo kubwa la mfumo huo ni kuhakikisha kunakuwa na usimamizi bora wa matumizi ya mafuta ambao...
WAKAZI wa kata ya Kiburugwa wilaya ya temeke jijini Dar es salaam wameiomba serikali kuwapatia huduma za kijamii ili kuboresha na kupunguza ghalama za maisha. Akizungumza na kituo hiki mmoja kati ya wakazi wa mtaa wa barabara ya mwinyi wilayani hapo bwana SELEMANI KASAPILA ameainisha baadhi ya huduma wanazo zikosa kuwa ni papoja na kutokuwepo kwa barabara na kituo cha polisi. Aidha mwenyekiti wa mtaa huo Bwana JUMA ALI NGONYANI amekiri kuwa shughuli nyingi za maendeleo katika kata...
Mchezaji aliyeingia kutokea benchi Pedro Rodriguez aliifingua timu yake bao la ushindi katika dakika za nyongeza ambapo Barcelona walishinda kombe la Eefa Super Cup mchezo uliopigwa kwenye mji wa Tbilisi. Washindi wa kombe la Europa Sevilla waliwashangaza Bacelona ambao ni washindi wa klabu bingwa barani ulaya baada ya Ever Banega kufunga goli la kwanza kwa mkwaju safi wa adhabu ndogo. Lionel Messi alifunga mara mbili na kuifanya Barca kuongoza kwa goli 2-1 kabla ya Rafinha na Luis Suarez kufumania nyavu...