Slider

CHADEMA: NAFASI YOYOTE YA KUINDOA CCM LAZIMA ITUMIKE
Local News

CHAMA cha  Demokrasia na Maendeleo  CHADEMA kimesema nafasi yoyote ya kukiondoa Chama cha Mapinduzi CCM madarakani ni lazima itumike  kwa kutambua kuwa Chadema ni chama cha watu, na hivyo ni lazima waheshimu mawazo ya kila mtu mwenye lengo linalofanana na chama hicho. Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam katika Mkutano wa baraza kuu la Chama cha Maendeleo na Demokrasia CHADEMA uliofanyika ili kupitia  na kuijadili ilani ya uchaguzi ambayo itapendekezwa katika mkutano mkuu kesho tarehe 4 Agosti 2015. Akizungumza...

Like
182
0
Monday, 03 August 2015
MALAYSIA YATOA WITO KUTOLEWA KWA TAARIFA JUU YA MABAKI YA NDEGE
Global News

MAAFISA nchini Malaysia wametoa wito kwa nchi zilizo karibu na kisiwa cha Reunion katika Bahari ya Hindi kusaidia kutoa habari zozote kuhusu mabaki ambayo huenda yanahusiana na ndege iliyotoweka ya Malaysia. Wito huo umekuja baada ya kipande cha ubawa kupatikana katika kisiwa hicho magharibi mwa Bahari ya Hindi. Kipande kipya cha mabaki kilichopatikana jana Jumapili katika kisiwa hicho kiligunduliwa kuwa ni ngazi ya kawaida ya nyumbani na wala hakihusiani na ndege hiyo ya Malaysia iliyotoweka mwaka mmoja...

Like
183
0
Monday, 03 August 2015
HALI YA WASIWASI YAANZA KUTANDA BURUNDI
Global News

KUMERIPOTIWA kuwepo kwa hali ya wasiwasi nchini Burundi kufuatia mauaji ya Jenerali mmoja ambaye alikuwa mtu wa karibu ya Rais Pierre Nkurunzinza katika masuala ya kiusalama. Jenerali Adolphe Nshimirimana aliuawa jana kwa kupigwa risasi akiwa ndani ya gari katika mji mkuu Bujumbura. Nshimirimana ambaye alikuwa mshauri mwandamizi wa masuala ya usalama wa Rais Pierre Nkurunzinza aliuawa wakati watu waliokuwa ndani ya gari walipomfyatulia risasi yeye na mlinzi wake katika kitongoji cha mji mkuu cha...

Like
208
0
Monday, 03 August 2015
ZAHANATI YA DA.MA AFRICA YAZINDULIWA KIBAHA
Local News

MGANGA Mkuu wa halmashauri ya Mji wa Kibaha, Dokta. Happniness Ndosi amepongeza shirika la masisita Waabuduo Damu ya Kristo kwa kufanikisha ujenzi wa zahanati ya kisasa katika kijiji cha Vikawe wilayani Kibaha mkoani Pwani.   Mganga huyo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa zahanati hiyo, pamoja na kuwapongeza amesema serikali itaendelea kushirikiana na mashirika yote kwa lengo la kuwezesha kila kijiji kiwe na zahanati  kila kata na kila wilaya kuwa na hospitali.   Zahanati hiyo ya DA.MA...

Like
297
0
Monday, 03 August 2015
RAIS KIKWETE KUZINDUA WIKI YA NENDA KWA USALAMA LEO
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dokta Jakaya Mrisho Kikwete leo anazindua maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama Barabarani ambayo kitaifa yanafanyika kwenye viwanja vya Tangamano mkoani Tanga.   Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Said Magalula amesema tayari Rais Kikwete ameshawasili mkoani humo jana na kupokelewa na viongozi mbalimbali kwa ajili ya uzinduzi wa maadhimisho hayo.   Magalula amesema baada ya Rais Kikwete kumaliza uzinduzi wa maadhimisho hayo leo jioni atapata nafasi ya kuwaaga wananchi wa mkoa wa...

Like
274
0
Monday, 03 August 2015
BODI YA LIGI MSITIKISE MASIKIO KAMA MSIMU ULIOPITA,KOMAENI NA MIUNDOMBINU YA VIWANJA KABLA YA LIGI KUANZA
Slider

Na Omary Katanga Michuano ya ligi kuu bara inataraji kuanza kutimua vumbi septemba 12 kwa msimu wa mwaka 2015/2016,na safari hii ikishirikisha jumla ya timu 16 zikiwemo 4 zilizopanda daraja kutoka ligi daraja la kwanza. Timu hizo 4 ni pamoja na African Sports ya Tanga,Majimaji ya Songea,Mwadui FC ya Shinyanga na Toto Africans ya Mwanza, zinazotarajiwa kuonesha ushindani mkubwa kama ilivyokuwa kwa Mbeya City msimu wa mwaka 2013/2014. Ongezeko hilo la timu linaongeza pia idadi ya mechi zitakazochezwa kwa msimu...

Like
277
0
Monday, 03 August 2015
AZAM BINGWA CECAFA KAGAME CUP 2015
Slider

Hongera Azam Fc kwa kutwaa ubingwa  Cecafa kagame Cup kwa mwaka 2015 wakiwa na historia ya kutoruhusu nyavu zake kutikiswa huku ikiwa ni mara ya kwanza kwa wanalambalamba kutwaa taji hili. Azam wametwaa taji hilo hapo jana katika uwanja wa taifa baada ya kuichapa timu ya Gor Mahia ya Kenya kwa mabao 2-0 kwenye mchezo wa fainali Ushindi huo wa wanalambalamba ni matunda ya magoli yaliyofungwa na washambuliaji wake John Bocco na Kipre Tchetche aliyepiga mpira wa adhabu nakuzama moja...

Like
290
0
Monday, 03 August 2015
MAHAKAMA KUU KANDA YA DARESALAAM IMETUPILIA MBALI KESI ILIYOFUNGULIWA NA IPTL, PAP DHIDI YA KAFULILA
Local News

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali kesi namba 301 iliyofunguliwa na Kampuni ya kufua Umeme ya IPTL, PAP pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya PAP Bw Harbinder Singh Sethi dhidi ya Mbunge wa Kigoma Kusini Mhe David Kafulila kwa madai kuwa Kafulila alichafua jina kampuni hizo na muhusika huyo kwamba walichota zaidi ya 300bn kwenye akaunt ya Tegeta escrow kinyume cha sheria na taratibu.   Katika shauri hilo, Kampuni ya IPTL,PAP na Herbinder Singh Sethi walitaka Mahakama...

Like
248
0
Friday, 31 July 2015
UGANDA: MBABAZI KUWANIA URAIS NJE YA CHAMA TAWALA CHA NRM
Global News

WAZIRI  mkuu wa zamani wa Uganda John Patrick Amama Mbabazi ametangaza kuwa hatawania urais kwa chama tawala NRM katika uchaguzi mkuu mwakani. Mbabazi ametangaza hilo leo mchana akiwa nyumbani kwake Kololo katika siku ya mwisho ya kurejesha fomu za uwaniaji wadhfa katika chama hicho tawala. Tangazo hilo la Mbabazi limetokea baada ya rais Yoweri Museveni kutangaza kuwa atarejesha fomu zake za kuwania uwenyekiti wa chama tawala NRM leo....

Like
226
0
Friday, 31 July 2015
WAYAHUDI WENYE MSIMAMO MKALI WAYACHOMA MOTO MAKAZI YA WAPALESTINA
Global News

WATU wanaoshukiwa kuwa ni Wayahudi wenye msimamo mkali wameyachoma moto makazi ya Wapalestina huko Ukingo wa Magharaibi hii leo na kumuua mtoto wa miezi 18 na kuwajeruhi wengine wanne. Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameyaita mashambulizi hayo kuwa ni tukio la kigaidi na kusema kuwa ameshitushwa na kitendo hicho cha kinyama ambacho kina dhamira zote za kigaidi. Msemaji wa Serikali ya Israel Mark Regev amesema wanahakikisha wanawakamata na kuwashitaki waliohusika katika tukio hilo huku wazazi wa mtoto huyo aliyeuawa...

Like
223
0
Friday, 31 July 2015
MANYARA: WADAU WA UKIMWI WAJIPANGA BAADA YA WAFADHILI KUTOTENGA FEDHA
Local News

WADAU wa ukimwi wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, wameazimia kujipanga kikamilifu kuhakikisha wanafanya jitihada za kupatikana kwa fedha za kuendesha bajeti ya ukimwi baada ya wafadhili kutotenga fedha.   Wakizungumza  leo kwenye mkutano wa wadau wa ukimwi wa wilaya hiyo uliofanyika katika mji mdogo wa Mererani, wamesema hadi sasa wafadhili waliokuwa wanawategemea hawajatenga fedha za kushughulika na ukimwi.   Mwenyekiti wa wadau hao Sihimu Hamis amesema sekta binafsi na serikali kwa kwa ujumla wanapaswa kujipanga ili...

Like
341
0
Friday, 31 July 2015