Rais wa Kamati kuu ya Kimataifa ya Olimpiki, Thomas Bach, amesema kuwa uchafuzi wa bahari ni moja ya kikwazo Rio de Janeiro katika maandalizi ya michuano ya hapo mwakani. Hata hivyo kutokana na hali hiyo waandaji wa mashindano hayo ya riadha wamesema kuwa watafanya kila linalowezekana kwa afya ya wanariadha wakati wa Olympiki. Takribani asilimia 70 ya maji taka yanamwagika Rio de Janeiro katika fukwe za Guanabara,eneo ambalo wapiga mbizi watafanyia mashindano yao. Katika hali inayoonyesha ni hatari kwa afya...
Bendi ya muziki wa afro pop kutokea Kenya hivi karibuni imeingia kwenye Headlines za vyombo vikubwa vya habari ulimwenguni baada ya kutumbuiza katika hafla ya chakula cha usiku katika ikulu ya nchi iliyoandaliwa na rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta akimakrimu rais wa marekani Barack Obama alipotembelea taifa hilo lililobeba histaoria ya maisha ya kiongozi huyu. Katika show hiyo ya Sauti Sol aliyofanyika ikulu Rais Obama pia aliungana na vijana hao kucheza muziki mzuri kutoka kwenye bendi hiyo. ...
RAIS wa Nigeria Muhammadu Buhari ameanza ziara ya siku mbili nchini Cameroon na akiwa huko analenga kuboresha mahusiano na nchi jirani na pia kuimarisha ushirikiano katika kupambana na wanamgambo wa Boko Haram. Buhari alipokelewa na mwenzake wa Cameroon, Paul Biya katika uwanja wa kimataifa wa mji mkuu Yaounde.mbali na mazungumzo yao ya jana, Viongozi hao watakutana na waandishi wa habari leo. Nigeria, Niger, Cameroon na Chad zimeungana katika kuwapiga waasi wa Boko Haram ambao sasa wamekuwa tishio hata...
MAMLAKA ya usafirishaji nchini Ufaransa imesema inachunguza mabaki ya ndege ya yanayodaiwa kupatikana ndani ya Bahari ya Hindi ili kubaini kama ni ya ndege ya Malaysia ya MH370 iliyopotea bila kuwa na taarifa zozote kwa muda mrefu sasa. Taarifa kutoka Marekani zinasema wachunguzi hao ambao wameona picha za mabaki hayo wana uhakika mkubwa kwamba ni ya ndege hiyo ya Malaysia ambapo mabaki hayo ni sehemu ya bawa la ndege. Hata hivyo, Wataalamu wa Ufaransa wanasema ni mapema mno kutoa uhakika...
JESHI la Polisi nchini limeshauriwa kuzisoma kwa kina na kuzielewa vyema Sheria na kanuni za Uchaguzi kabla ya kuzitekeleza ili kuliepushia lawama na kufanya wajibu wao kikamilifu ili kuufanya Uchaguzi unaokuja uwe katika hali ya uhuru, haki na amani. Wito huo umetolewa na Jaji Mstaafu Thomas Mihayo alipokuwa akitoa Mada katika Warsha ya Siku mbili kwa Maafisa wa Jeshi la Polisi iliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini katika Ukumbi wa Hotel ya Grand mjini Zanzibar....
MWANACHAMA mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA, Edward Lowasa asubuhi hii anachukua fomu kuomba kuteuliwa na chama hicho kugombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hii itakuwa ni mara ya tatu kwa kiongozi huyo kuchukua fomu kwa ajili ya kutaka nafasi hiyo ya juu nchini, ambapo mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1995 kisha Juni mwaka huu akiwa ndani ya chama cha Mapinduzi-CCM, kabla jina lake halijakatwa na vikao vya juu vya chama hivho Julai 12 mwaka...
KIONGOZI wa kundi la wanamgambo la Lashkar-e-Jhangvi linalopinga waislamu wa Kishia, ameuwawa nchini Pakistan katika mapambano na polisi mkoani Punjab. Kwa mujibu wa vyombo vya usalama vya Pakistan, wafuasi wa kundi hilo walivamia gari la polisi lililokuwa limembeba kiongozi huyo, Malik Is-haq, na wanachama wengine 13 wa kundi lake. Lengo la wavamizi hao ilikuwa ni kumkomboa Is-haq....
WATU wawili wanaume wanatarajiwa kufikishwa mahakamani nchini Zimbabwe baadaye leo wakishtakiwa kwa makosa ya uwindaji , baada ya simba maarufu nchini humo kuuawa na mtalii mmoja raia wa Marekani . Simba huyo, anayejulikana kwa jina la Cecil, alipigwa risasi nje kidogo ya mbuga ya wanyama ya taifa ya Hwange na Walter Palmer, daktari wa meno na mtu anayependa uwindaji, ambaye pia anaweza kukabiliwa na mashtaka. Maandamano juu ya kuuawa kwa simba huyo yamefanyika nje ya makaazi ya bwana Palmer katika...
WATANZANIA wametakiwa kujiepusha na vitendo vya rushwa kwani vitawafikisha pabaya na kurudisha maendeleo yao nyuma hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini-Takukuru, Dokta Edward Hosea katika mafunzo ya maafisa wa Taasisi hiyo juu ya utakatishaji fedha na kupata taarifa na mlolongo wa uhalifu kwa kutumia sheria za Tanzania. Dokta Hosea amesema mafunzo hayo yatawasaidia maafisa hao kupata na kuelewa vithibitisho vya uhalifu vinavyogusa fedha na mali...
CHAMA cha Mapinduzi –CCM, kimesema kwamba ni chama kikubwa na hakitishwi wala kuzuia mtu yeyote kukihama huku kikizungumzia uwepo wa wanachama ambao waliwahi kukihama na kurejea. Taarifa hizo zimetolewa leo na Katibu wa Siasa na Uenezi wa Mkoa wa Dar es Salaam Juma Simba, ambaye amezungumzia pia kuhusu tetesi kuwa wafuasi wa Lowassa ambao ni wengi ndani ya chama hicho wanasemekana kuwa wapo mbioni kumfuata kada huyo, amesisitiza wao hawazuii mtu yeyote kuhama chama hicho....
Kocha kutoka Mexico, Miguel Herrera amefukuzwa kazi baada ya kumshambulia mwandishi wa habari wa kituo kimoja cha luninga. Hatua hii ya kufukuzwa kazi kwa kocha huyo kunakuja ikiwa ni mbili tu baada ya kuongoza kikosi hicho kwenye kombe la saba la medali ya dhahabu nchini Marekani. Miguel Herrera mwenye umri wa miaka 47 amekuwa akiiongoza timu hiyo ya Mexico kwa miaka16 hadi sasa. katika utetezi wake Herrera amesema kuwa alifanyiwa fujo ndo maana akafikia hatua...