ZAIDI ya kaya 260 waathirika wa mafuriko wanaoishi kwenye mahema katika eneo la mateteni wilayani kilosa mkoani morogoro wanaishi maisha magumu kwa kutegema viazi vitamu na wengine wanalazimika kulala nje na familia zao kutokana na uchakavu wa mahema. wakizungumza kwa uchungu waathirika hao wamelalamikia kuendelea kuishi maisha magumu kutokana na uchakavu wa mahema ambapo baadhi yao wanalala nje na watoto na kuishi kwa kutegemea viazi vitamu kusukuma maisha. Hata hivyo, wameiomba Serikali kuwaonea huruma kwa watu hao kutokana na maisha...
MATOKEO katika uchaguzi wa rais uliofanyika nchini Burundi wiki hii yatatangazwa kesho, ambapo rais aliye madarakani Pierre Nkurunziza anatarajiwa kushinda kipindi cha tatu huku wapinzani wake wakidai kuwa ni kinyume na katiba. Mkuu wa Tume ya uchaguzi nchini Burundi Pierre-Claver Ndayicariye amesema kiasi cha asilimia 72 hadi 80 ya wapiga kura wa nchi hiyo wanaofikia milioni 3.8 wamepiga kura siku ya Jumanne....
IMEELEZWA kuwa Mji muhimu wa mwisho uliokuwa mikononi mwa kundi la Al Shabaab kusini magharibi mwa Somalia wa Baardheere umechukuliwa tena na vikosi vya Muungano wa Afrika (AU) -miaka 7 baada ya wapiganaji hao wenye itikadi kali kuingia kwa mara ya kwanza katika mji huo . Wakazi wa mji huo wamesema vikosi vya Kenya na Somalia vikiwa na silaha nzito na usaidizi wa mashambulizi ya anga viliuvamia mji huo , ambao wapiganaji wa Al Shabaab waliutoroka usiku. Majeshi kutoka Kenya,...
ALIYEKUWA Mbunge wa Jimbo la Wawi kisiwani Zanzibar kupitia chama cha wananchi-CUF– Mheshimiwa HAMAD RASHID leo amekabidhiwa rasmi kadi ya kuwa mwanachama wa chama cha Alliance for Democratic Change-ADC. Akizungumza wakati wa kumkabidhi kadi hiyo ya uwanachama, Mwenyekiti wa –ADC- Taifa SAID MIRAJI amesema ni muda muafaka sasa kwa watanzania kuwa wamoja ili kuleta maendeleo kwa Taifa. Aidha amevihakikishia vyama vingine vya siasa kuwa chama chao kipo tayari kushirikiana kwa masuala muhimu na yenye maslahi kwa wananchi...
WATU kumi wamefariki dunia papo hapo na wengine 47 kujeruhiwa baada ya basi la kampuni ya simiyu express lililokuwa likitokea bariadi mkoani simiyu kuelekea jijini dar es salaam kupasuka tairi la mbele na kupoteza mwelekeo na kisha kuparamia mti katika kijiji cha Wilunze eneo la Chalinze nyama wilayani Chamwino Mkoani Dodoma. Kwa mujibu wa mashuhuda wamesema kabla ya ajali, basi hilo lenye namba za usajili T 318 ABM Scania lilikuwa kwenye mwendo mkali na wakasikia kishindo cha kupasuka kwa tairi....
Mwanamfalme Ali bin Al Hussein wa Jordan, aliyeshindwa uchaguzini na Sepp Blatter jaribio lake la kutaka kuwa rais wa Fifa mwezi Mei, amesema Blatter hafai kusimamia shughuli ya mageuzi kwenye shirikisho hilo lililoandamwa na kashfa ya ufisadi. Amesema jukumu hilo linafaa kuachiwa mrithi wake. Kupitia taarifa iliyotolewa Jumatano, Mwanamfalme Ali, aliyejiondoa uchaguzini duru ya pili baada ya kupata kura 73 dhidi ya 133 za Blatter duru ya kwanza, alisema ana wasiwasi Blatter, ambaye ameongoza shirikisho hilo linalosimamia soka duniani tangu...
SHIRIKA moja la kutetea haki za binadamu limeishutumu mojawepo ya kampuni kubwa zaidi duniani ya mauzo ya mawese iliyoko nchini Liberia kwa kutumia mlipuko wa ugonjwa wa Ebola kujinufaisha. Shirika hilo la Global Witness limesema kuwa wakati mlipukowa ugonjwa huo ulipoifikia Afrika Magharibi mwaka uliopita kampuni ya Golden Veroleum ilifyeka maelfu ya ekari kwa maandalizi ya kilimo cha zao la mawese wakati ambapo makundi ya misaada kwa jamii yalikuwa yanashughulika na kuokoa maisha ya watu kutokana na ugonjwa huo. Hata...
WABUNGE wa Ugiriki wamepiga kura ya kuunga mkono mashariti mapya yaliyowekwa na wadeni wa taifa hilo lililo katika hatari ya kufilisika. Hatua hiyo inatoa nafasi ya kuanzishwa kwa mashauriano mapya kati ya taifa hilo pamoja na mataifa mbalimbali yanayotoa msaada wa kuokoa uchumi wa nchi hiyo kutoshuka. Hata hivyo Waziri Mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras alishinda kura hiyo ya Bunge baada ya kura ya kuunga mkono kupigwa na vyama vingine vya upinzani juu ya suala...
ALIEKUA Diwani wa Kata ya Kunduchi kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo -CHADEMA- ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chama hicho -BAWACHA-jimbo la Kawe Janeth Rithe ameachana na chama hicho na kujiunga na chama cha ACT WAZALENDO akiambatana na Viongozi wenzake 12 wa jimbo la Kawe. Akiongea na Waandishi wa Habari Mara baada ya kukabidhiwa kadi ya Chama cha ACT WAZALENDO Rithe amesema amechukua uamuzi huo baada ya kusoma sera na kugundua kua hicho ndio chama kinachosimamia...
JOPO la Madaktari kutoka Hospitali mbalimbali za Marekani wameanza kutoa huduma za kiafya katika Hospitali ya Serikali ya Mwananyamala kwa Wagonjwa mbalimbali wenye matatizo ya kansa, kinywa, macho, kisukari pamoja huduma nyingine za kiafya Wataalam hao walioshirikiana na Jumuiya ya Watanzania waishio Marekani na Taasisi ya Wanaawake wa Afrika ya Kupambana na Kansa-AWCA wanatarajia kuhudumia wagonjwa zaidi ya 600 katika maeneo ya Dar es salaam na Zanzibar ambapo Jopo hilo limechangia dawa zenye thamani ya takribani Milioni 200 kwa Watanzania....
JESHI la Marekani limesema kuwa mmoja viongozi wa kundi la kigaidi la al-Qaeda, ameuwaa katika shambulio la angani lililotekelezwa na ndege za kijeshi za Marekani Nchini Syria. Idara ya ulinzi ya Pentagon imesema kuwa Muhsin al-Fadhli, alikuwa kinara wa kundi la Khorasan, lililotumwa na al-Qaeda, kutoka Pakistan hadi nchini Syria. Mmoja wa wajumbe wa bunge la congress amesema kuawawa kwa mtu huyo Al Fahdli mwenye ufahamu na gaidi hatari ambaye amekuwa akijaribu kuiangamiza Marekani na washirika wake ni faraja...