Slider

MKUTANO WA MATAIFA IMARA YANAYOINUKIA KIUCHUMI DUNIANI KUANZA LEO URUSI
Global News

MKUTANO wa kilele wa baadhi ya mataifa imara yanayoinukia kiuchumi duniani unaanza rasmi leo nchini Urusi. Nchi zinazoshiriki zinafahamika kama BRICS yaani Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini. Benki ya BRICS ilizinduliwa mapema wiki hii, ambayo itafadhili miradi ya miundo mbinu katika nchi...

Like
144
0
Thursday, 09 July 2015
WATANZANIA WASHAURIWA KUTUMIA ELIMU NA USHAURI JUU YA MATUMIZI BORA YA LISHE
Local News

WATANZANIA wameshauriwa kutumia vyema elimu na ushauri unaotolewa na wataalam mbalimbali juu ya matumizi bora ya lishe ili kupunguza hali ya udumavu kwa watoto wanaozaliwa nchini. Hayo yamesemwa leo bungeni mjini Dodoma na Naibu waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii mheshimiwa Kebwe Steven Kebwe wakati akijibu maswali kutoka kwa baadhi ya wabunge  yaliyoelekezwa katika wizara hiyo kuhusu ushiriki wa serikali katika kupunguza tatizo la udumavu. Mheshimiwa Kebwe amesema kuwa kwa kiasi kikubwa serikali inashiriki katika kuhakikisha kila mwananchi...

Like
247
0
Thursday, 09 July 2015
BODI YA UTALII KUFANYA MAONYESHO DAR
Local News

BODI ya utalii nchini  imesema inatarajia kufanya maonyesho ya utalii Jiji Dar es salaam ambayo  yanategemea kuanza mapema mwezi wa kumi mwaka huu . Akizungumza na Kituo hiki, Kaimu Mkurugenzi mwendeshaji bodi ya utalii Tanzania DEVOTHA MDACHI amesema kuwa maandalizi kwa ajili ya maonyesho ya utalii ya meshaanza na bodi inategemea kupokea mawakala wa utalii zaidi ya 50 na wanahabari wasiopungua 10 kutoka Mataifa mbali mbali. Amebainisha kuwa, maonyesho  hayo ni nafasi kubwa kwa wafanyabiashara  wa Tanzania kutangaza kazi zao...

Like
184
0
Thursday, 09 July 2015
MCHUJO KWA WALIOTANGAZA NIA KUPITIA CCM KUFANYIKA LEO
Local News

KAMATI Kuu ya chama cha Mapinduzi-CCM, leo inatarajiwa kufanya Zoezi la uchujaji wa majina ya watu waliotangaza nia ya kugombea nafasi ya urais ndani ya Chama hicho ambapo inatarajiwa leo itatoa majina ya wagombea watano. CCM inatakiwa kupitisha jina moja la mtu atakayepeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu wa wabunge na rais unaotarajiwa kufanyika tarehe 25 Oktoba mwaka 2015. Hapo kesho, Halmashauri kuu ya chama itakutana ambapo itachuja majina hayo matano hadi kufikia matatu kupitia mtindo wa kupiga...

Like
313
0
Thursday, 09 July 2015
MERCELL JENSEN ATANGAZA KUSTAAFU SOKA
Slider

Mlinzi wa zamani wa Ujerumani Marcell Jansen ametangaza maamuzi ya kustaafu soka akiwa na miaka 29 na kusema hana mpango wa kutafuta klabu nyingine baada ya kumaliza kuitukikia Hamburg SV. Beki huyo wa kushoto ambae pia ameichezea Moenchengladbach na Bayern Munich kabla ya kukipiga kwa miaka saba kwenye klabu ya Hamburg. Amesema amepokea ofa kutoka klabu mbalimbali ila angependelea kuingia kwenye fani nyingine mbali na kucheza mpira. Aliandika kupitia ukurasa wake wa facebook. Jansen aliyecheza kombe la dunia mwaka 2006...

Like
209
0
Thursday, 09 July 2015
MATUMAINI YA RAHEEM STERLING KUBAKI LIVERPOOL YAFIFIA
Slider

Mshambuliaji wa England Raheem Sterling hakuhudhulia mafunzo na mazoezi siku ya jumatano huku ikiripotiwa kuwa mchezaji huyo amekataa kwenda kwenye tour na timu yake ya Liverpool ambapo klabu hiyo inatarajiwa kwenda Asia na Australia wiki ijayo. Sterling, 20, ameipigia simu klabu hiyo na kuwaeleza kuwa hajisikii vizuri kiafya, hii ni kwa mujibu wa vyanzo vya habari nchini Uingereza. Hali hii ya sasa kwa mchezaji huyu na klabu yake inaongeza uvumi juu ya dili mpya iliyowekwa mezani na Manchester City kwakuzingatia...

Like
219
0
Thursday, 09 July 2015
SHIRIKISHO LA SOKA NIGERIA LIMETHIBITISHA KUFANYA MAZUNGUMZO NA SUNDAY OLISEH
Slider

Shirikisho la mpira wa miguu nchini Nigeria limethibitisha kufanya mazungumzo na nohodha wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria (Super Eagles) Sunday Oliseh ili kuweza kumpatia nafasi ya kukinoa kikosi hicho kufuatia kufukuzwa kwa mwalimu wa kikosi hicho Stephen Keshi. Rais wa shirikisho hilo Amaju Pinnick anatajwa kufanya mazungumzo na Sunday Oliseh huko London kwaajili ya kufanya mazungumzo. Taarifa hizo za kupewa nafasi nahodha huyo wa zamani ziliripotiwa pia katika tovuti ya shirikisho la mpira wa miguu...

Like
226
0
Thursday, 09 July 2015
DILMA ROUSSEFF ATOA MSIMAMO WAKUTOTISHIKA
Global News

WAKATI tuhuma zikiongezeka juu ya mustakabali wa serikali yake rais Dilma Rousseff  wa Brazil ameliambia gazeti la Folha de Sao Paulo kwamba hatishiki na kwamba hakuna msingi wa yeye kuachishwa kazi na bunge. Ikiwa ni miezi saba baada ya kuingia katika muhula wake wa pili wa uongozi serikali yake inazidi kutikiswa na kashfa ya rushwa katika kampuni kubwa ya mafuta nchini Petrobras. Tuhuma za hivi karibuni zinadai kwamba kampeni yake ya kuwania urais ilifadhiliwa kwa fedha haramu kutoka kampuni hiyo...

Like
186
0
Wednesday, 08 July 2015
UGIRIKI YAAHIDI KUTIMIZA MASHARTI MAPYA
Global News

SERIKALI ya Ugiriki ipo katika harakati za kuandika mapendekezo mapya yatakayofanikisha mazungumzo ya kutafutia ufumbuzi wa matatizo yake ya kiuchumi. Hali hiyo imekuja kufuatia viongozi wa Ukanda wa Ulaya mjini Brussels kuipa nchi hiyo muda wa siku tano kupeleka mapendekezo yake ya kusaidia kuondokana na tatizo la uchumi. Mbali na nchi hiyo kupewa muda huo wa kupeleka mapendekezo yake  lakini Raisi wa baraza la viongozi wa ukanda wa ulaya Donuld Tusk ameonya kuwa zimesalia siku chache kutatua mgogoro wa Ugiriki...

Like
212
0
Wednesday, 08 July 2015
VIJANA WATAKIWA KUACHA KUTUMIKA NA BAADHI YA WANASIASA KUVURUGA AMANI
Local News

VIJANA nchini wametakiwa kuacha kutumiwa na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa katika kuvuruga Amani ya nchi hususani katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Wakizungumza na kituo hiki waathirika wa dawa za kulevya ambao tayari wameacha matumizi ya dawa hizo wamesema kuwa viongozi wengi wamekuwa wakiwafuata na kuwapa fedha kwa ajili ya kuwalazimisha kuwapigia kura ili wapate nafasi wanazozihitaji. Aidha wamesema kuwa ni vema vijana kujitambua ili kuepukana na vitendo hivyo kwani viongozi hao wanawatumia wakati...

Like
164
0
Wednesday, 08 July 2015
BUNGE LAWASILISHA MUSWADA WA SHERIA YA TUME YA WAALIMU WA MWAKA 2015 LEO
Local News

BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo limewasilisha bungeni muswada wa sheria ya tume ya walimu wa mwaka 2015 wenye lengo la kuboresha huduma za walimu nchini. Akisoma muswada huo kwa mara ya pili bungeni mjini Dodoma Waziri wa Elimu na mafunzo ya Ufundi mheshimiwa Shukuru Kawambwa amesema kuwa lengo kuu la muswada huo ni kutunga sheria ya usimamizi wa masuala muhimu ya walimu ili kuleta manufaa zaidi. Waziri Kawambwa amebainisha kuwa muswada huo utarahisisha pia uwajibikaji kwa walimu...

Like
186
0
Wednesday, 08 July 2015