MKUTANO mkuu wa nchi sita zenye nguvu duniani ikiwemo Iran unatarajiwa kuendelea tena huko Vienna nchini Australia, pamoja na tarehe ya kuhitimishwa kwa mazungumzo hayo kutajwa . Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Urusi,Sergei Lavrov, amesema kwamba awali kulikubwa na sababu ya kuamini kuwa suala hilo litahitimishwa katika siku chache lakini haikuwa hivyo. Naye waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ufaransa,Laurent Fabius amehakikisha kutoondoka mapema katika meza ya mazungumzo hayo ambapo pia ametaja hatua zitakazo chukuliwa...
RAIS wa Marekani Barack Obama amefanya mazungumzo na kiongozi wa chama cha jamii ya wavietnam Ikulu mapema wiki hii,mkutano ambao ni wa kwanza tangu nchi hizo mbili kurejesha uhusiano baada ya miaka ishirini iliyopita. Rais Obama amesema kwamba pamoja na kutofautiana kwa falsafa za kisiasa,nchi kati ya nchi hizo mbili bado unahitajika ushirikiano wa dhati, katika kujiimarisha kiuchumi. Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema kwamba Rais Obama anatafuta kuweka historia ya serikali yake kutoka katika uhusiano tete na Vietnam na...
IMEELEZWA kuwa zaidi ya ajira elf 16 zinatarajiwa kuzalishwa kutokana na kuanzishwa kwa shughuli za ujenzi wa mitambo ya mafuta na gesi nchini Tanzania. Akizungumza na kituo hiki Jijini Dar es salaam Mkufunzi wa umeme kutoka chuo cha –VETA– mkoani Lindi MAJEO MGOE amesema shughuli hizo zitasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza Ajira hususani kwa wahitimu wa chuo hicho. Magoe ameongeza kuwa mafunzo wanayopata wanafunzi kutoka katika chuo hicho yamewasaidia vijana kuongeza sifa za kuajiriwa hali ambayo inawawakwamua...
WIZARA ya Nishati na Madini nchini imewahakikishia wananchi wa jimbo la Nkasi kuwa ipo tayari kusimamia vyema suala la ujenzi wa mradi usambazaji wa umeme katika kipindi kifupi kijacho. Ahadi hiyo imetolewa leo Bungeni na Naibu waziri wa wizara hiyo mheshimiwa CHARLES MWIJAGE wakati akijibu swali la mheshimiwa ALLY KESSY aliyetaka kufahamu mikakati ya serikali juu ya utekelezaji wa suala hilo. Mheshimiwa Mwijage amesema kuwa ili kuhakikisha mradi huo unakamilika mapema serikali imejipanga kuwatumia wataalamu wazawa katika kukamilisha...
Steven Gerrard amesema kuwa aliyewahi kuwa mchezaji mwenzake katika kikosi cha England David Beckham amehusika kwa kiasi kikubwa kwenye uhamisho wake kwenda kuichezea LA Galaxy. Beckham amekaa Los Angeles na kushinda kombe la MLS katika mchezo wa mwisho uliochezwa December 2012. Gerrard, 34, anatarajiwa kucheza mchezo wake wa kwanza akiwa na kikosi hicho katika mchezo wa kirafiki dhidi ya wamexico siku ya jumamosi. “David ni shujaa wangu, ni mtu hodari sana, mchezaji mzuri, ni mtu niliemtegemea kujifunza na kupata ushauri...
Kiungo wa zamani wa England Frank Lampard amesema anajisikia faraja na mwenye bahati kukipiga katika timu moja ya New York City na Andrea Pirlo Mchezaji huyo wa zamani wa klabu za Chelsea na Manchester City,37 aliwekwa wazi na klabu ya New York siku ya jumanne akiwa tayari kukipiga katika mchezo wake wa kwanza na klabu hiyo dhidi ya Toronto tarehe 12 July. Klabu hiyo ya New York pia amemuongeza muitalia Andrea Pirlo, 36, kutoka Juventus kuongeza nguvu kwenye kikosi pamoja...
SERIKALI ya China imeidhinisha hatua kadhaa mwishoni mwa juma kulishinikiza soko ambalo limepoteza takriban asilimia 30 ya thamani yake katika wiki tatu zilizopita kurudi katika hali yake. Wawekezaji wengi wana wasiwasi na kwamba robo ya kampuni zilizoorodheshwa kuomba kusitisha kuuza hisa zao zinasababisha uwezo wa serikali kukopa unazidi kuwa katika hatari. Taarifa zaidi zinaonesha kuwa hali hiyo ni kama hatua ya kuzilinda kampuni hizo dhidi ya hasara zaidi ambapo kwa kipindi cha mwaka uliopita serikali ilifurahia uwekezaji katika soko la...
WANAMGAMBO wa kundi la Al Shabaab wamekiri kuhusika na shambulizi lililotokea eneo la Kaskazini Mashariki mwa Kenya ambapo watu 14 wameuawa usiku wa kuamkia leo. Taarifa za awali zimeonesha kuwa shambulio hilo lilikuwa na nia ya kuwalenga wafanyikazi wengi wa machimbo ya mawe wasiokuwa wenyeji katika maeneo hayo. Hata hivyo imeelezwa kuwa mashambulizi kama hayo yametishia kudumaza shughuli za maendeleo na kiuchumi katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa Kenya ambapo wengi wa wafanyikazi wake ni watu kutoka maeneo ya nje...
SERIKALI imeombwa kuona umuhimu wa kutafuta njia mbadala ya kuhakikisha inapunguza foleni katika Jiji la Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na kuruhusu maeneo ya bandari kavu kutumika kama barabara kuu ya kupitishia maroli ya mizigo. Ombi hilo limetolewa na Mjumbe wa Kamati ya Amani Mkowa wa Dar es Salaam ALPHONCE TEMBA wakati akizungumza na kituo hiki juu ya namna ya kupunguza msongamano wa magari ya mizigo yanayosababisha foleni barabarani. Amesema kuwa maeneo kama Chalinze, Ruvu kigwaza na Mlandizi yanaweza...
MKURUGENZI wa Taasisi ya Takwimu nchini dokta Albina Chuwa amesema kuwa suala la takwimu zinazohusu hali ya mazingira, ikiwemo uharibifu unaotokana na uchafuzi wa maji, hewa chafu na kupotea kwa uoto wa asili bado ni ngeni katika nchi zinazoendelea, hususan za bara la Afrika. Dokta Chuwa ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya siku tano ya takwimu za hali ya mazingira kwa nchi za Jumuiya ya Afrika mashariki jijini Arusha uliohudhuriwa na viongozi wa Takwimu wa nchi hizo. Amesema kuwa mafunzo...
MASHIRIKA ya kutetea maslahi ya wanyama nchini Zimbabwe yameonesha kushangazwa na hatua ya nchi hiyo kuuza Tembo kwa madai kwamba inahitaji fedha kwaajili ya kukabiliana na uwindaji haramu. Waziri wa mazingira nchini humo amesema kuwa tembo hao walisafirishwa kwa ndege hadi China kwenye ndege binafsi ya mizigo huku wahifadhi wa wanyama wanasema wanyama hao wanahitaji uangalifu wa miaka kadhaa kutoka kwa wazazi wake. Tembo hao wataishi katika mbuga ya wanyama karibu na mji uliopo kusini mwa china– Guangzhou wakati taarifa...