BARAZA la usalama la Umoja wa Mataifa limeamua kuwawekea vikwazo majenerali sita wa kijeshi nchini Sudan Kusini wanaotuhumiwa kuchochea vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimedumu kwa miezi kumi na nane sasa. Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Samantha Power amesema uamuzi wa baraza hilo la usalama unadhihirisha kuwa wale wanaohusika na ukiukaji wa haki za binadamu na kuhujumu juhudi za kupatikana amani watakabiliwa na sheria. Majenerali hao sita waliowekewa vikwazo wamepigwa marufuku kusafiri na mali zao...
WAZIRI MKUU wa Ethiopia Heilemariam Disalegn Boshe leo anatembelea Kiwanda cha kutengeneza Dawa za Kuulia Wadudu-TAMCO- kilichopo Kibaha Mkoani Pwani akiongozana na Mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Ziara hiyo ya siku mbili ni sehemu ya Mapambano ya Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Nchi ya Ethiopia dhidi ya Mazalia ya Mbu ili kudhibiti kuenea kwa Ugonjwa wa Malaria ambapo Waziri Mkuu Boshe ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Viongozi wa Afrika katika Mapambano dhidi ya Malaria. Mheshimiwa Boshe amewasili jana...
Nyota wa Argentina Javier Mascherano amewaomba wadau na wapenzi wa mpira wa miguu kuwa na utulivu kuelekea fainali kati yao na wapinzani wao Chile. Timu hizi mbili zitakutana siku ya jumamosi huko Santiago huku mwenyeji wa michuano hiyo Chile wakiwa na shauku ya kumaliza karibu karne ya kushindwa kutwaa taji kwenye michuano mikubwa huku wakishuhudiwa na mashabiki wa nyumbani. Wakati huohuo pia Argentina wanateswa na hamu ya kushinda taji la kwanza katika kipindi cha miaka 22, wakitazama zaidi ubora wa...
Kundi A Cecafa Kagame Cup: Yanga ( Tanzania), Gor Mahia ( Kenya), Khartoum ( Sudan), Telecom ( Djibout), KMKM ( Zanzibar ). Kundi B Cecafa Kagame Cup: Azam (Tanzania), Malakia ( South Sudan), KCC ( Uganda), Adama City ( Ethiopia) Kundi C Cecafa Kagame Cup : APR( Rwanda) , Al Shandy ( Sudan), LLB ( Burundi), Elman (...
MAKUNDI ya wapiganaji yamefanya mashambulizi dhidi ya maafisa wa usalama nchini Misri katika Rasi ya Sinai. Jeshi limesema makabiliano yanaendelea huku wanajeshi kadhaa na wapiganaji wakiuawa.Taarifa ya jeshi imesema vizuizi vitano vya polisi vililengwa sawa na kituo kimoja cha polisi. Hili ndilo shambulio kubwa zaidi kufanywa na wapiganaji wa kiisilamu walioko eneo la Sinai, miaka miwili baada ya kuondolewa madarakani kwa Rais aliyeegemea mrengo wa kidini Mohamed Morsi....
INDONESIA imasema kuwa idadi ya watu waliofariki huko Medan katika ajali ya ndege ya kijeshi imepanda na kufikia watu 141. Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi la wana anga nchini humo hakuna yeyote aliyenusurika kifo miongoni mwa watu 122 waliokuwa ndani ya ndege hiyo ya mizigo. Jeshi limesema kuwa limeanzisha uchunguzi kubaini haswa ni akinani waliokuwa ndani ya ndege hiyo ya kijeshi baada ya uvumi kuenea kuwa ndege hiyo ilikuwa imewabeba abiria waliokuwa wamelipa nauli. ...
IMEELEZWA kuwa, Magonjwa yasiyoambukiza kama vile kansa, kisukari na shinikizo la damu, yameonesha kushika kasi katika nchi zinazoendelea hususani nchi ambazo zinauchumi mdogo zaidi ikiwemoTanzania. Hayo yamesemwa leo na Kaimu Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya Dokta CHARLES MASSAMBU alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya ufunguzi wa semina iliyoandaliwa na Wizara hiyo ambayo imehusisha Sekta mbalimbali yenye lengo la kujadili namna ya kuthibiti na kuzuia magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza nchini....
SERIKALI imewasilisha mswada wa sheria ya kuwalinda watoa taarifa za uhalifu na mashahidi wa mwaka 2015 unaolenga kuweka utaratibu wa kisheria wa kulinda watoa taarifa za uharifu na mashahidi. Akiusoma kwa mara ya pili leo Bungeni mjini Dodoma, Waziri wa Katiba na Sheria, Dokta Asha Rose Migiro, amesema lengo hilo litatekelezwa kwa kuimarisha mifumo iliyopo ya upatikanaji wa taarifa za...
Zaid ya watu 140 wanahofiwa kufariki dunia kufuatia ajali ya ndege ya Kijeshi kuanguka katika makazi ya watu muda mfupi baada ya kupaa. Kaskazini mwa Indonesia . polisi na timu ya Taifa ya uokozi wanaendelea kuwatafuta waathirika wengine kwenye eneo hilo la tukio katika mji wa...
IRAN na nchi zenye nguvu zaidi duniani zimeongeza muda wa kufikia makubaliano kamili kuhusu mpango wa kinyuklia wa Iran hadi tarehe saba mwezi huu baada ya kushindwa kufikia makubaliano hayo hapo jana. Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov amesema baada ya miaka miwili ya mazungumzo kati ya nchi zinazohusika, anaamini makubaliano yako karibu yatafikiwa. Rais wa Marekani Barack Obama hata hivyo amesisitiza nchi yake haitasita kujiondoa kutoka mazungumzo hayo ya kinyuklia iwapo masharti yanayotakiwa kutimizwa hayatakuwa ya...
KATIBU MKUU wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema ulimwengu unapaswa kuona aibu kuwa miaka mitatu baada ya nchi zenye nguvu zaidi duniani kuidhinisha azimio mjini Geneva la kuleta amani Syria, lakini bado watu wa nchi hiyo wanataabika kwa kiwango kikubwa na mzozo huo na huenda Taifa hilo likasambaratika. Ki Moon amesema zaidi ya watu 220,000 wameuawa Syria katika vita ambavyo vimedumu kwa miaka mitano na zaidi ya nusu ya idadi ya raia wa nchi hiyo wamelazimika kuyatoroka makaazi...