Star wa muziki wa Dancehall Popcaan amepata nafasi ya kushiriki kwenye wimbo wa I Know There’s Gonna Be (Good Times) katika project inayoaandaliwa na producer wa Uingereza Jamie xx, wimbo huo pia utamhusisha rapa Young Thug. kutokea Marekani. Hii si mara ya kwanza kwa msanii huyu kushiriki kwenye collabo za kimataifa kwani aliwahi pia kushirikiana na msanii wa Uingereza Melissa Steele kwenye ngoma ya single Kisses for Breakfast.Iliyofanya vizuri kwenye UK Top 10 chart. Mbali na hiyo pia sauti yake...
WAZIRI wa Mambo ya nje wa Ufaransa amesema itakuwa ni busara kuuchelewesha uchaguzi wa kumchaguwa rais mpya wa Shirikisho la Soka la Kimataifa FIFA uliopangwa kufanyika hapo kesho kutokana na uchunguzi mpya kuhusu rushwa dhidi ya shirikisho hilo. Akizungumza siku moja baada ya mchezo wa soka kutumbukizwa kwenye machafuko kufuatia kukamtwa kwa maafisa wa FIFA kutokana na madai ya rushwa yaliyotolewa na Marekani Laurent Fabius amesema muda unahitajika ili kuweza kufahamika nini hasa kitakachoendelea....
MSANII wa Muziki wa Bongo flaver nchini, Juma Kassim Ally, maarufu Juma Nature leo ameto misaada ya vitu mbalimbali katika Hospitali ya Serikali ya Mbagala Rangi tatu iliyopo eneo la Zakhiem, mbagala jijini Dar es salaam. Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo , Juma nature amesema lengo, ni kumshukuru Mungu kwa kutimiza miaka kumi na sita tangu aanze kazi hiyo ya Muziki. Amesema kuwa ameichagua Hospitali hiyo kwakuwa mbali nakuwa ni hospitali iliyopo eneo analoishi lakini pia yeye amekuwa...
IMEELEZWA kuwa viwango vya Mimba za Utotoni Vimepungua na Upatikanaji wa Huduma za Afya ya Uzazi kwa Vijana imeongezeka kufatia mpango wa Uelimishaji unaofanywa na Shirika la Afya na Utafiti Afrika- AMREF Hayo yamebainishwa na Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Dokta Flavian Gowele alipokuwa Mgeni rasmi katika Uwasilishaji wa Ripoti ya Utafiti uliofanywa na shirika hilo kwa kipindi cha miaka minne katika Wilaya za Ilala, Kinondoni na Iringa ambapo Takwimu zinaonyesha kuwa viwango vya Mimba za Utotoni zimeshuka kutoka asilimia...
WATANZANIA wameombwa kutunza miradi mbalimbali ya mandeleo inayoletwa na Serikali kwa kushirikiana na wadau na wananchi wenyewe. Rai hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Juma Chumu alipokuwa akizindua miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya ya Ilala yenye gharama ya shilingi bilioni 14. Aidha amewataka watanzania kuepuka kutumiwa na wanasiasa ili kusababisha uvunjifu wa amani katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka...
IDADI ya watu wanaosumbuliwa na njaa ulimwenguni imepungua na kufikia chini ya watu milioni 800-kwa mara ya kwanza tangu Umoja wa mataifa ulipoanza kutoa takwimu hizo. Hii ni kwa mujibu wa shirika la Umoja wa mataifa la Chakula na Kilimo-FAO ambalo limesema katika ripoti yake ya mwaka iliyochapishwa jana. Shirika hilo lenye makao yake mjini Rome Italy limesema kuna watu milioni 795 ulimwenguni wanaosumbuliwa na njaa-idadi hiyo ikiwa na upungufu wa watu milioni 216 ikilinganishwa na jinsi hali namna ilivyokuwa...
WAZIRI MKUU wa zamani wa Uingereza Tony Blair amejiuzulu nafasi ya ujumbe wa umoja wa kimataifa katika kamati inayoshughulikia usuluhishi wa mgogoro wa Mashariki ya kati, unaohusisha nchi ya Israel na Palestina nafasi ambayo ameitumikia kwa kipindi cha miaka nane. Vyanzo vya habari vilivyokaribu na Blair vinasema ataendelea kuwepo akijihusisha na baadhi ya shughuli katika eneo hilo. Afisa mmoja wa Palestina amemlaumu Blair kwa kufanya kazi ili kuwaridhisha waisrael na Marekani. Umoja huo unaundwa na UN, EU nchi ya Marekani...
IMEELEZWA kuwa kutokana na kitendo cha rais wa burundi pierre Nkurunziza kung’ang’ania madarakani na kusababisha machafuko ndani ya nchi hiyo, hali hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa ongezeko la wakimbizi kutoka burundi Nchini Tanzania kwa kuwa ndiyo nchi jirani iliyopakana na nchi hiyo. Wakizungumza na EFM katika kambi ya muda ya wakimbizi hao iliyopo mjini kigoma katika uwanja wa Lake Tanganyika,wakimbizi hao wameeleza kuwa chama tawala kinachoongozwa na rais Nkurunziza kimekuwa kikitishia hali ya usalama wa...
MSANII wa Muziki wa Bongo flaver nchini, Juma Kassim Ally, maarufu Juma Nature leo anatarajiwa kutoa misaada ya vitu mbalimbali katika Hospitali ya Serikali ya Zakhiem, mbagala jijini Dar es salaam. Akizungumza na EFM Juma nature amesema lengo la kutoa msaada huo, ni sehemu yake ya kumshukuru Mungu wakati anatimiza miaka kumi na sita tangu aanze kazi hiyo ya Muziki. Kilele cha maadhimisho hayo ya miaka kumi na sita ya Juma Nature katika Muziki kitakwenda sambamba na hitimisho la maadhimisho...
Keko rapa kutokea Uganada ametangaza mpango wake wa kujiondoa kwenye kampuni katika kampuni inayomsimamia ya Sony Music Entertainment Africa and ROCKSTAR4000. Rapa huyu amekuwa msanii wa kwanza kutokea nchini Uganda kupata deal ya kufanya albam mbalimbali pamoja na usimamizi wa moja kwa moja chini ya kampuni hiyo ya sony. Kupitia mtandao wa twitter rapa huyu ameelezea maumivu yake kwakusema kwamba hakuweza kuapata nafasi ya kufanya mziki mzuri toka ajiunge na kampuni hiyo mwaka 2012. Maamuzi yake yakutaka kujitoa yanakuja kutokana...
MAAFISA sita wa ngazi ya juu wa shirikisho la kabumbu ulimwenguni FIFA,wamekamatwa na maafisa wa vyombo vya sheria vya Uswisi hii leo mjini Zurich, siku mbili kabla ya mkutano mkuu wa shirikisho hilo. Maafisa hao wanakabiliwa na kitisho cha kuhamishiwa Marekani ambako watakabiliwa na madai ya kuhusika na visa vya udanganyifu, ukandamizaji, na kubadilisha fedha kinyume cha sheria. Kwa mujibu wa idara ya sheria ya serikali kuu ya Uswisi,maafisa hao wa FIFA wanakabiliwa na tuhuma za kupokea rushwa ya mamilioni...