WAMILIKI wa vyombo vya habari nchini-MOAT na waandishi wahabri wamelaani muswada mpya wa sheria ya vyombo vya habari uliotaka kuwasilishwa katika kikao cha bunge kilichopita kwa hati ya dharula kwa kuwa baadhi ya vipengele kwenye muswaada huo unapunguza uhuru wa vyombo vya habari. Hata hivyo muswaada huo wenye kasoro nyingi unaonesha kuwa kuna hila chafu za kutaka kupitisha sheria hiyo bila kuhusisha wadau wa tasnia hiyo ili kudhibiti vyombo binafsi na wananchi wasiweze kutoa na kupata taarifa jambo ambalo ni...
Mastar wengi na watu maarufu barani Afrika hivi karibuni wamekuwa wakizionyesha silaha zao kwenye mitandao ya kijamii ambazo wengi wao haifahamiki kama wanamili kisheria au la. Lakini pia inawezekana wanafanya hivyo kama njia ya kujihami kufuatia kuongezeka kwa matukio ya uharifu wa kutumia silaha. Star wa muziki kutokea Kenya kaka sungura mwishoni mwa wiki iliyopita alivamiwa na watu aliodai kuwa ni majambazi waliokuwa na silaha na kumuibia laptop yake aina HP Envy 17 pamoja na simu yake mpya aliyonunua wiki...
URUSI imeanza mazoezi makali ya kivita yanayojumuisha kikosi cha anga cha wanajeshi 150 pamoja na kikosi cha mashambulio ya mbali ya makombora. Wizara ya mambo ya ndani ya Urusi inasema kuwa wanajeshi elfu kumi na mbili wanatarajiwa kuhusishwa na mazoezi hayo makali ya siku nne yanayolenga kutaka kujua uimara wa jeshi hilo na utayari wake. Hata hivyo tukio hili la mazoezi ya majeshi hayo yanalenga nchi za magharibi kufuatia machafuko yanayoendelea Ukraine ambapo Urusi imekuwa ikinyooshewa kidole kutokana na machafuko...
JUMLA ya watu kumi na nane wamepoteza maisha kutokana na mafuriko makubwa yaliyotokea maeneo ya Magharibi mwa Marekani na Kaskazini mwa Mexco. Taarifa zaidi zinasema kuwa wengi wa waliothibitishwa kufariki dunia kutokana na mafuriko hayo ni kutoka mpakani mwa Mexco katika mji wa Acuna ambapo watu 3 wamefariki na wengine 12 hawajulikani walipo. Hata hivyo Gavana wa jimbo la Texas GREG ABBOTT amesema kuwa mafuriko hayo yameleta madhara makubwa katika jimbo lake hususani uharibifu wa makazi ya...
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo –Chadema-dokta WILBROAD SLAA amewataka wasimamizi wa daftari la kudumu la wapiga kura kutoa kipaumbele kwa makundi maalum katika jamii ili waweze kujiandikisha bila kupata madhara. Dokta SLAA ameyasema hayo wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Hamugembe wilayani Bukoba ambapo amesema kuwa kitendo cha kuwatengenezea mazingira bora wahusika wa makundi hayo kutarahisishia kutumia nafasi hiyo kutimiza malengo yao ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu. Mbali na...
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dokta JAKAYA KIKWETE amemteua ANTHONY MAVUNDE kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kurugenzi ya mawasiliano Ikulu jijini Dar es salaam imesema kuwa Rais amefanya uhamisho wa wakuu wa Wilaya kumi kwa nia ya kuongeza ufanisi katika uongozi wa Wilaya mbali mbali nchini. Katika mabadiliko hayo amemhamisha Luteni EDWARD OLE LENGA kutoka Wilaya ya Mkalama Mkoani Singida kuwa mkuu wa wilaya mpya ya Kyerwa...
RIPOTI za mahakama nchini Burkina Faso zinasema kuwa mwili ambao unahisiwa kuwa wa raisi wa zamani aliyeuawa Thomas Sankara utafukuliwa hii leo katika jaribio la kutaka kubainisha ikiwa ni wake. Familia na marafiki wa rais Sankara wamekuwa na shauku iwapo mabaki hayo ni yake. Sankara ambaye aliuawa wakati wa mapinduzi mwaka 1987, alichukuwa uongozi baada ya mapinduzi ya mwaka wa 1983 na baadaye alipinduliwa na Blaise Compaore ambaye aliitawala Burkina Faso hadi mwaka uliopita alipolazimishwa kuondoka na maandamano makubwa katika...
BASI moja limechomwa moto mjini Bujumbura Burundi na waandamanaji waliorejea mabarabarani kupinga uamuzi wa rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu. Kitongoji cha Kanyosha kimekuwa kitovu cha maandamano hayo dhidi ya awamu ya tatu ya rais Nkurunziza. Maandamano haya yanarejea baada ya kuuawa kwa kiongozi wa chama cha upinzani Zedi Feruzi nje ya nyumba yake katika mji mkuu Bujumbura....
WAKURUGENZI wa Halmashauri za wilaya nchini wameombwa kuwagharamia watu wenye ulemavu wa ngozi ili kwenda kushiriki maadhimisho ya siku ya albino kote duniani ambayo kitaifa yatafanyika juni 13 mkoani Arusha ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo juu ya siku ya watu wenye ulemavu wa ngozi, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi Kasim Kibwe amesema kuwa maadhimisho hayo yanakusudia kuongeza ufahamu juu ya...
TUME ya Taifa ya uchaguzi leo imetangaza rasmi ratiba ya uchaguzi mkuu kwa mujibu wa mamlaka iliyopewa kikatiba. Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na kusainiwa na mwenyeki wa tume hiyo jaji mstaafu DAMIAN LUBUVA imesema kuwa uteuzi wa wagombea katika vyama kwa ngazi ya urais, ubunge na udiwani utafanyika Agosti 21 mwaka...
Tamasha kubwa la kuadhimisha miaka kumi na sita ya msanii JUMA NATURE maarufu kama kiroboto pamoja na hitimisho la sherehe za mwaka mmoja za 93.7 EFM linalofahamika kama KOMAA CONCERT kwa mara ya kwanza litafanyika rasmi jumamosi hii ya tarehe 30 mwezi mei katika ukumbi wa Dar Alive –Mbagala, kuanzia saa kumi na mbili jioni. Tamasha hili limeandaliwa na Juma nature akishirikiana na EFM kwa lengo la kuwaburudisha Mashabiki wa juma nature na wasikiliazaji wa 93.7 EFM ikiwa ni...