OFISA Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili,Ufilisi na Udhamini-RITA,PHILIP SALIBOKO,amesimamishwa kazi. Hatua hiyo inatokana na kesi inayomkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu, inayohusu kupokea mgawo wa fedha kutoka Akaunti ya Tegeta ESCROW. Kwa mujibu wa taarifa iliyopatikana na kuthibitishwa na SALIBOKO mwenyewe,kusimamishwa...
MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF,LADISLAUS MWAMANGA,ameitaka jamii kuelewa kuwa, chombo hicho ni cha Serikali na hakina mwingiliano wa Dini,wala itikadi yoyote ya Kisiasa. Amesema lengo la TASAF ni kuonyesha uwajibikaji na kuwezesha Wananchi wote kuwa na maisha bora. MWAMANGA ameeleza hayo alipokuwa akizindua kikao kilichojumuisha Waandishi wa Habari,Waratibu,Wahasibu na Maofisa wanaofuatilia shughuli za mfuko...
HATIMAYE Serikali imeumaliza rasmi mgogoro wa ardhi uliodumu kwa kipindi kirefu baina ya Wizara ya Maliasili na Utalii na Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo,unaohusisha eneo la hifadhi ya Taifa ya Saadani. Aidha,Serikali imeiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo,kukaa na Shirika la Hifadhi ya Taifa-TANAPA sanjari na wadau,kurejea mipaka ya zamani ya eneo hilo,ili kuepusha mgongano usio na tija. Mgogoro huo umeibuka mwaka 2005,baada ya Serikali kuipandisha hadhi Mbuga ya wanyamapori ya Saadani kuwa Hifadhi ya Taifa na kumpa...
RAIS JAKAYA KIKWETE,amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Dokta RAJABU RUTENGWE,kutokana na vifo vya watu 18 na wengine 11 kujeruhiwa katika ajali ya basi na lori,iliyotokea mwishoni mwa wiki iliyopita. Ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Msimba,barabara kuu ya Morogoro-Iringa,kilometa chache kutoka Ruaha Mbuyuni na kusababisha watu 18 kuteketea kwa moto. Dokta KIKWETE amesema amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya vifo vya watu 18 kutokana na ajali ya barabarani iliyosababisha miili yao kuungua...
Maria Sharapova mchezaji nambari mbili duniani katika mchezo wa tennis hatocheza mchezo wa nusu fainali mwishoni mwa wiki hii dhidi ya mjerumani kwenye mashindano ya Fed Cup yanayofanyika huko Sochi nchini Urusi. Maamuzi hayo yakumuondoa Sharapova yamekuja kufuatia kusumbuliwa na jeraha la mguu Akizungumza na waandishi wa habari, Sharapova ameonesha masikitiko yake kutokana na namna alivyokuwa na hamasa ya kufanya vizuri katika mashindano hayo. “ mimi na timu yangu tulibadilisha ratiba ya mazoezi ili kuweza kuiwakilisha nchi yangu...
Wababe wa jiji la Madrid nchini Hispania jana wameshindwa kutambina katika mchezo wa kwanza wa Kombe la Mabingwa barani Ulaya,UEFA, hatua ya robo fainali baada ya kutoka sare ya bila kufungana 0-0. Katika mchezo huo uliochezwa katika dimba la Vicente Calderon Athletico Madrid walikuwa wenyeji wa Real Madrid ambapo timu hizo zitarudiana katika uwanja wa Bernabeu tarehe 22 Aprili. Nyota ya mshambuliaji wa real Madrid Gareth Bale ilishindwa kung’aa jana baada ya kukosa nafasi ya wazi mnamo dakika ya tatu...
SERIKALI imeuingiza kwenye urithi wa taifa,Ukumbi wa Nkurumah wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam,UDSM. Tukio hilo la kihistoria limefanyika katika ukumbi huo,ambapo Waziri wa Maliasili na Utalii,LAZARO NYALANDU,ametia saini makubaliano ya kuingiza ukumbi huo kwenye urithi wa Taifa. Akizungumza katika hafla hiyo,Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam,Profesa RWEKEZA MUKANDALA,anesema tukio hilo ni muhimu kwa...
MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Simiyu,Dokta TITUS KAMANI,amewataka wananchi wote wenye sifa za kupiga kura,kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la Wapigakura. Ameeleza kuwa,wakati utakapofika wajitokeza kupata haki ya kuchagua Kiongozi wanayemtaka katika Uchaguzi Mkuu ujao wa OCTOBA mwaka huu. Dokta KAMANI ambaye Pia ni Mbunge wa Busega na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi,amewaomba wananchi ambao watajiandikisha kwenye daftari hilo kuvitunza vizuri vitambulisho...
MAWAZIRI wa Mashauri ya Kigeni wa Ujerumani , Ufaransa , Urusi na Ukrain wameelezea wasiwasi uliopo kufuatia kutokea kwa mapigano Mashariki mwa Ukrein na kikiukwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyoafikiwa mwezi Februari. Baada ya mazungumzo yaliyofanyika mjini Berlin, Waziri wa Mashauri ya kigeni wa Ujerumani FRANK-WALTER STEINMEIER amewaambia Waandishi wa Habari kuwa kati ya silaha ambazo zitaondoa ni pamoja na Vifaru. Pande hizo mbili zimeonekana kuheshimu makubaliano hayo hadi kulipotokea mapigano ya hivi majuzi kwenye uwanja wa...
WAZAZI na Walezi mkoani Mwanza,wametakiwa kuwalea watoto katika maadili ya Kiroho,ili kuepuka Wimbi la Ujangili na Uvunjifu wa Amani nchini. Mkurugenzi wa Vijana,Jimbo la Nyanza Kusini,Mchungaji JOSEPH MSESE,amesema hayo wakati wa Sherehe ya Uzinduzi wa huduma za Matendo kwa Vijana wa Kanisa la Waadventista Wasabato, katika Kanisa la Kakebe,Igoma jijini humo. MSESE amebainisha kuwa ili mtoto akue katika maadili mazuri na kuachana na matendo machafu ni vyema akalelewa kimwili,kiroho kijamii na...