SERIKALI imeoneshwa kusikitishwa na vitendo vya kikatili vinavyofanywa na baadhi ya watu kwa watu wenye ulemavu wa ngozi -ALBINO-vinavyojitokeza mara kwa mara katika maeneo mbalimbali nchini. Hayo yamesemwa leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu waziri wa mambo ya ndani mheshimiwa PEREIRA SILIMA ambapo amesema kuwa mbali na jitihada nyingi zinazo chukuliwa na serikali amewaasa wananchi kushirikiana vyema ili kukomesha tatizo hilo nchini....
Kuelekea kwenye mashindano ya shika ndinga wilaya ya kinondoni wafahamu baadhi ya wanafamilia wa 93.7 efm akiwemo viongozi unaweza kushiriki kwenye mashindano haya kwakusikiliza vipindi vyote vya redio hii na kujibu maswali yatakayoulizwa ...
miongoni mwa yaliyojiri kwenye Sports Headquarters leo...
MAZUNGUMZO kuhusu mpango tata wa Iran wa Nyuklia yameendelea nchini Uswisi, kwa kuwasili Mawaziri wa Mambo ya Nje kutoka Mataifa Sita yenye nguvu duniani. Kiongozi wa mazungumzo wa Iran ABBAS ARAQCHI amesema makubaliano yanawezekana lakini mazungumzo yako katika hatua ngumu na bado kuna mambo ya kutatua. Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza PHILIP HAMMOND pia amesema anaamini makubaliano yatafikiwa lakini yatatakiwa kuhakikisha Iran haipati uwezo wa kutengeneza bomu la nyuklia....
KUFATIA Mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam baadhi ya Wananchi wamewataka watu waishio maeneo ya mabondeni, kuhama maeneo hayo ili kunusuru Maisha, Mali pamoja na kuepusha gharama kwa Serikali pindi maafa yanapotokea. Wakizungumza na EFM kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema Jiji la Dar es salaam, bado lina maeneo mengi yaliyosalama, hivyo wanapaswa kuepuka utamaduni wa kwamba maisha bora yanapatikana katikati ya Mji bila kujali Usalama wa maeneo hayo. Wananchi hao wamesema imekuwa ni Desturi ya Watanzania kulaumu Serikali...
MHADHIRI na Mtafiti wa Masuala ya Kiislamu kutoka Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar -SUZA Dokta ISSA HAJI ZIDI amesema, Dini ya Kiislamu haipingani na Uzazi wa Mpango kwani ulikuwepo tokea wakati wa Mtume MUAHAMAD, hivyo amewashauri Waislamu kuzitumia kwa ajili ya kulinda afya zao. Akizungumza kwenye mjadala kuhusu Uzazi wa mpango katika Uislamu ulioandaliwa na Kitengo Shirikishi cha Afya ya Uzazi na Mtoto, Dokta ZIDI amesema, lengo la Uzazi wa Mpango ni kulinda Afya ya Mama na Mtoto aliyezaliwa...
RAIS JAKAYA KIKWETE amewataka Watanzania kuipigia kura ya ndiyo Katiba Inayopendekezwa, kwa kuwa ni bora kuliko inayotumika sasa. Pia amewaonya Viongozi wa Dini wanaohamasisha wafuasi wao kuipigia Kura ya Hapana Katiba, kwa kufanya hivyo wanaingilia Uhuru binafsi wa mtu kuamua mambo yake. Rais KIKWETE ameeleza hayo katika Mkutano wa Viongozi wa Dini wanaounda Kamati ya Amani kwa Mkoa wa Dar es salaam ambapo mikoa mbalimbali...
Mkali wa muziki wa pop duniani Akon amewasili nchini Kenya siku ya ijumaa tayari kuhudhuria kwenye kilele cha tamasha la kutafuta vipaji vya muziki la Airtel Trace Music. Msafara wa Akon unaundwa na timu ya watu mashughuli duniani akiwemo Devyne Stephens pamoja na mkongwe aliegundua wakali kama Jay Z, P Diddy, Alicia Keys, Usher, Mariah Carey, Akon n.k Tanzania inawakilishwa na Mayunga ambae alishinda kwenye mashindano ya hapa nyumbani nakupata nafasi ya kusonga...
Dereva wa mbio za magari wa timu ya Ferrari Sebastian Vettel raia wa Ujeruamani ameibuka na ushindi kwenye mashindano ya Malaysian Grand Prix baada ya kumbwaga Lewis Hamilton wa timu ya Mercedes. Ushindi huo wa Vettel kwenye michuano hiyo ni wa kwanza katika mashindano hayo akiwa na timu ya Ferrari Ushindi wa mjerumani huyo umemfanya kuwa ndiye dereva mwenye mafanikio makubwa katika eneo la Sepang akiwa na mataji manne Katika pambano hilo lililokuwa na ushindani mkali Hamilton alifanikiwa kushika nafasi...
Katika mchezo wa kirafiki uliochezwa jana kwenye uwanja wa Ccm Kirumba Mwanza kati ya timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na timu ya taifa ya Malawi (The Flames) na kumalizika kwa sare ya kufungana 1-1 wadau wamekuwa na maoni tofauti kufuatia matokeo hayo. Malawi ndio walikuwa wa kwanza kuliona lango Stars katika dakika ya tatu ya mchezo kupitia mchezaji wake Esau Kanyenda goli lililodumu hadi kipindi cha pili cha mchezo. Matumaini ya watanzania waliokuwa wakifatilia mchezo huo yaliletwa na...
Mbali na director mkali wa filamu pamoja na muziki Marekani Brett Ratner kuukana ukweli kuhusu yeye kuwa na mahusiano na Mariah Carey na kuziita taarifa hizo ni utoto kwa sasa ameshindwa kuficha kikohozi chake kufuatia kuonekana kwa picha tofauti zikiwaonyesha wawili hao wakiwa pamoja katika muonekano wa wakimapenzi. Mariah Carey na Brett Ratner wanatofauti ya mwaka mmoja wakati Ratner akisherehekea siku yake ya kuzaliwa siku ya ijumaa huku ya Mariah Carey ikifuata siku ya jumamosi. Moja kati ya picha hizo inawaonyesha wawili hawa...