KANSELA wa Ujerumani ANGELA MERKEL anatarajia kwenda mahali ilipoanguka Ndege ya Shirika la Ujerumani, GermanWings katika Milima ya Alps nchini Ufaransa. GermanWings ambayo ni tawi la bei nafuu la Shirika la Ndege la Ujerumani, Lufthansa imesema, ndege yake iliyopata ajali ilikuwa ikitoka katika mji wa Barcelona nchini Uhispania, ikielekea Duesseldorf Ujerumani, ikiwa na watu Zaidi ya 100. Rais wa Ufaransa FRANCOIS HOLLANDE amesema anaamini hakuna mtu aliyenusurika katika ajali...
MTANDAO wa Jinsia Tanzania-TGNP umesema kuwa, utaendeleza harakati za kuhakikisha kwamba, Wanawake wanatoa sauti ya pamoja katika kudai Katiba mpya inayozingatia mrengo wa Kijinsia. Akizungumza na EFM Mkurugenzi wa TGNP, LILIAN LIUNDI amesema , Wanawake wanatambua kuwa Katiba inayozingatia mrengo wa Kijinsia ni ile inayotokana na mchakato ulioshirikisha Sauti za Wanawake na Wanaume, na iliyoweka bayana makubaliano na Msingi Mkuu unaoongoza Tanzania. Amesema kuwa kama Katiba itakua imejengewa msingi wa Usawa, Utu na Heshima ya Mwanamke na...
KUENDELEA kuongezeka kwa matukio ya mabadiliko ya hali ya hewa,kumeathiri sekta ya kiuchumi,ikiwemo Kilimo na Ufugaji. Hivi karibuni maeneo ya Kanda ya Ziwa Victoria,hususan Wilaya ya Kahama,kumeshuhudiwa matukio hayo ya kupotea kwa mifugo na uharibifu wa mazao. Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa-TMA,Dokta AGNES KIJAZI,amesema kuwa,ili kukabiliana na matukio hayo kuna haja ya kuwepo kwa mfumo thabiti wa kutoa taarifa mapema....
SPIKA wa Bunge wa ANNE MAKINDA,amewataka Wabunge kuwa makini na kuacha ushabiki wa Vyama, wakati wa kuchangia masuala muhimu ya kutunga Sheria. Amewataka kuwasilisha maombi ya mapendekezo ya kurekebisha sheria kwa kujikita kwenye mambo yenye manufaa kwa Taifa. Spika ANNE, ameeleza hayo Bungeni,ambapo amesema hayupo tayari kupokea mapendekezo ya Marekebisho ya Muswada yaliyokiuka...
Timu ya taifa ya Malawi (The Flames) inatarajiwa kuingia nchini hapo kesho siku ya alhamisi ukiwa ni msafara wa watu 25 watakaotua uwanja wa taifa wa Mwl. Jk Nyerere ambapo siku ya ijumaa wanatarajiwa kutua katika jiji la Mwanza tayari kwa mchezo wao wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Stars siku ya jumapili. Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto amesema msafara huo utakaokuwa na wachezaji 18 na viongozi 7, kocha mkuu wa The Flames Young Chimodzi...
Baada ya kukosa nafasi ya kuandaa kombe la dunia mwaka 2018 kwa kuambulia kura mbili na kubwagwa na urusi katika nafasi hiyo sasa England inafikiria kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kupata nafasi ya kuwa mwenyeji wa wa fainali za kombe la dunia mwaka 2026. Mwenyekiti wa shirikisho la kandanda nchini England Greg Dyke amesema jaribio lao litategemea kama rais wa FiFa Sepp Blatter hataendelea kusalia madarakani lakini pia kuteuliwa kwa mwingereza David Gill katika kamati ya kuu ya uongozi ya Fifa...
WAZIRI wa Mambo ya nchi za Nje wa Yemen RIYADH YASEEN amezitolea wito nchi ya Ghuba ya Uarabu kuingilia Kijeshi katika nchi yake, kuwazuia wapiganaji wa Kihouthi ambao wanaipinga Serikali ya Rais ABDU RABBU MANSOUR HADI, ili wasiendeleei kuyateka maeneo zaidi ya nchi. Katika mahojiano na Gazeti la Kiarabu la Al-Sharq al-awsat, Waziri YASEEN amesema wapiganaji hao wameteka Miji na Viwanja vya ndege, na kumtia kizuizini yoyote wanayemtaka. Amesema wameelezea hofu yao kwa Baraza la Ushirikiano wa nchi za Ghuba,...
NDEGE ya abiria inayomilikiwa na shirika la ndege la Germanwing Airbus A320 Imeanguka katika Milima ya Alps nchini Ufaransa. Ndege hiyo ilikuwa imebeba abiria 142 na Wahudumu 6 ikitoka Barcelona Uhispania kuelekea Duesseldorf. Ndege hiyo inayomilikiwa na shirika la ndege la Ujerumani Lufthansa chini ya nembo Germanwings imeripotiwa kuanguka karibu na mji wa...
JAMII ya Wafugaji katika kijiji cha Mindukeni Kata ya Talawanda Jimbo la Chalinze Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani,wameomba kutengewa maeneo yao ili kuepusha migogoro inayojitokeza baina yao na Wakulima ikiwemo kujeruhiwa na Kuuwawa. Ukosefu mpango wa matumizi bora ya ardhi, umesababisha kundi hilo la wafugaji kutengwa kushiriki kwenye shughuli za Kimaendeleo ndani ya vijiji vyao. Jamii hiyo ya Wafugaji wamefikisha kilio chao,mbele ya Mbunge wa jimbo hilo RIDHIWANI KIKWETE wakati akiwa kwenye ziara yake katika Kata ya...
IMEBAINISHWA kuwa mojawapo ya masuala yanayochangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la Matumizi ya dawa za kulevya nchini, ni uwepo wa shughuli za Kilimo cha Mazao ya aina mbalimbali za Dawa hizo ikiwemo Bangi katika baadhi ya maeneo ya nchi. Hayo yamesemwa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge Mheshimiwa JENISTER MHAGAMA, wakati akiwasilisha kwa mara ya Pili Muswada wa Sheria ya Udhibiti wa Dawa za kulevya wa mwaka 2014, ambapo ameitaja...
WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, FRANK-WALTER STEINMEIER amesema pande zinazohusika katika mzozo wa Ukraine, lazima ziepukane na hatua zozote zinazoweza kupelekea mzozo mpya kusambaa zaidi nchini humo. Aidha, STEINMEIER ametoa wito wa kuendelea kwa mchakato wa mpango wa amani wa Minsk, ambao umesainiwa mwaka uliopita, katika juhudi za kusimamisha mapigano Mashariki mwa Ukraine. STEINMEIER na maafisa wengine waandamizi wanaohusika na mzozo wa Ukraine, wanatarajiwa kukutana mjini Paris, Ufaransa kujadiliana kuhusu hatua za kusitisha mapigano...