Waandamanaji wanapanga kutumia panya 200 katika maandamano katika mji wa Nyeri mkoa wa kati nchini Kenya kulingana na gazeti la the Star nchini humo. Gazeti hilo limemnukuu mshirikishi wa maandamano hayo John Wamagata akisema ”tutaleta panya 200 na kuwatembeza katikati ya mji”. Gazeti hilo linaongezea kwamba maandamano hayo yanayopangwa kufanyika wiki ijayo yanapinga mapendekezo ya bunge la kaunti hiyo kutumia shilingi milioni 75 kujenga klabu ya kuimarisha afya. Klabu hiyo itakuwa na eneo la kunyosha misuli,eneo la kuoga kwa...
Rais wa Marekani, Barack Obama, ameshtumu vikali matamshi ya mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Republican, Donald Trump, kwamba waislamu wasiruhusiwe kuingia Marekani. Obama amesema hiyo ‘si marekani wanayohitaji.’ ”Kuwabagua Waislamu wa Marekani kutasababisha nchi hiyo kukosa usalama,na kuongeza tofauti iliopo kati ya nchi za magharibi na zile za kislamu”, Obama alisema Siku ya Jumatatu bwana Trump, aliongezea kuhusu mpango wa kupiga marufuku nchi zote ambazo zina historia ya kutekeleza mashambulizi dhidi ya...
Kamati ya dharura ya shirika la afya duniani imetoa tathmini kuwa kuna uwezekano mdogo kidogo cha maambukizi ya virusi ZIKA kuenea katika mataifa mengine ,hivyo mashindano ya Olympic hayana haja ya kuhamishwa nchini Brazil.Ingawa tayari kulikuwa na wito wa michuano hiyo ya Rio kuahirishwa au kuhamisha mashindano hayo. Shirika la afya ulimwenguni WHO, kwa mara nyingine limetoa angalizo la awali kukataza watu kutosafiri au kufanya biashara katika maeneo ambayo kwa sasa yana virusi vyua ZIKA. Hata hivyo shirika hilo limewataka...
Mchezaji wa zamani wa Timu ya taifa ya Brazil Carlos Dunga ametimuliwa kwenye nafasi ya Kocha wa Brazil kufuatia Nchi hiyo kutupwa nje ya Michuano ya Copa America na Peru. Shirikisho la Soka la Brazil, CBF, limetoa taarifa ya kumtimua Dunga ambaye pia alitarajiwa kuiongoza Nchi hiyo kwenye Michezo ya Olimpiki ambayo itachezwa nchini Brazil mwezi Agosti. Pamoja na Dunga, pia Wasaidizi wake wote wa Benchi la Ufundi wameondolewa, na CBF imesema itateua Watu wengine kuingoza Timu hiyo. Brazil ilifungwa...
Klabu ya Everton imethibitisha usajili wa kocha Ronald Koeman kuwa mkufunzi wake mpya kwa kandarasi ya miaka mitatu. Everton wamelipa dola milioni 5 kama fidia kwa mkufunzi huyo wa miaka 53 ambaye anaihama klabu ya Southampton baada ya kuisimamia kwa miaka miwili. Everton imekuwa bila mkufunzi tangu ilipomtimua Roberto Martinez kabla ya mwisho wa msimu uliopita. Koeman amesema kuwa Everton ni klabu yenye historia kubwa na ari ya kutaka kushinda huku mwenyekiti wa klabu hiyo akimwita raia huyo wa Uholanzi...
Wabunge sita nchini Kenya wanatarajiwa kuwasilishwa mahakamani kufuatia madai ya kutoa matamshi ya chuki. Siku ya Jumapili mbunge mmoja anayegemea upande wa serikali alidaiwa kutaka kuuawa kwa aliyekuwa waziri mkuu na kiongozi wa upinzani nchini humo Raila Odinga. Wabunge hao ni Moses Kuria, Kimani Ngunjiri na Ferdinand Waititu kutoka kwa upande wa serikali na Junet Mohammed Aisha Jumwa,Johnson Muthama na Timothy Bosire upande wa upinzani. Bw Kuria anadaiwa kuitisha kuuawa kwa Raila kupitia lugha ya kikikuyu.Hathivyo amekana kutoa matamshi...
Ripoti kutoka Orlando Marekani zasema Omar Mateen, mtu aliyewafyatulia risasi na kuwaua watu 49 katika klabu moja ya watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja, alikuwa akitembelea klabu hiyo iitwayo Pulse mara kwa mara. Wahudumu na meneja wa klabu hiyo amenukuliwa na magazeti ya Marekani akisema kuwa, ameshawahi kumuona Mateen, hata akinywa pombe katika eneo hilo. Naye mkewe wa zamani Sitora Yusufiy, amemwelezea Mateen kama mtu aliyekuwa na tabia za ugomvi wa mara kwa mara na kutaka kupigana na watu na...
Rais Dkt. John Pombe Magufuli amewaapisha mawaziri wapya wa mambo ya ndani na yule wa kilimo siku mbili tu baada ya kutangaza mabadiliko madogo katika baraza lake la mawaziri. Jumamosi iliyopita rais Magufuli alitangaza uteuzi wa mbunge wa Buchosha Dkt. Charles John Tizeba kuwa waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi. Kufuatia uteuzi huo, aliyekuwa Waziri wa Kilimo, bwana Mwigulu Lameck Nchemba aliteuliwa kuwa Waziri wa mambo ya ndani ya nchi. PICHA: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John...
Shirikisho la kandanda barani ulaya , UEFA, limeonya kuzichukulia hatua na hata kuzifukuza timu za Uingereza na Urussi. Hatua hiyo ni kufuatia mashabiki wa timu kuwa chanzo cha ghasia zinatokea kama ilivyotokea wakati wa mechi yao ya huko Marseille. suala la ulevi linatajwa kuwa ni moja ya vyanzo vya vurugu hizo ambapo baadhi ya mashabiki wana kwenda katika viwanja vya michezo hiyo huku wakiwa...
Waziri wa maswala ya ndani wa ufaransa , Bernard Cazeneuve, ametoa ushauri kwa wakuu wa miji mbalimbali wenyeji wa kinyanganyiro cha soka barani ulaya Euro2016, kupiga marufuku matumizi ya pombe katika maeneo tete siku ya na hata kabla ya siku ya mechi kufanyika. Hii ni kutokana na matukio ya wafuasi wa timu kadhaa kushambuliana katika visa vilivyochochewa na ulevi huko mjini Marseille katika kipindi cha siku 3 zilizopita. Shirikisho la kandanda barani ulaya , UEFA, limeonya kuzichukulia hatua ya hata...
Eritrea imeishtumu Ethiopia kwa kutekeleza shambulio katika mpaka wake ambao una ulinzi mkali. Wakazi katika eneo la Tsorona wanasema wamesikia milio ya risasi na kuona wanajeshi wakielekea katika mpaka. Hata hivyo Waziri wa habari wa Ethiopia amesema hafahamu lolote kuhusu vita hivyo. Zaidi ya watu laki moja walifariki katika mapigano yaliyodumu mika miwili na nusu katika ya mataifa yote mawili. Kamati ya Umoja wa Mataifa ilisema kuwa eneo linalozozania linapaswa kuwa la Eritrea, lakini Ethiopa haijawahi kukubali uamuzi huo. Mwandishi...