Slider

MAPIGANO YAZUKA TENA JUBA, SUDAN KUSINI
Global News

Mapigano yamezuka tena nchini Sudan Kusini saa chache baada ya Umoja wa Mataifa kuhimiza pande hasimu kusitisha vita. Mwanahabari aliyeko mjini Juba ameambia BBC kwamba milio ya risasi na milipuko mikubwa imeanza kusikika kote mjini humo. Amesema silaha nzito zinatumika kwenye vita hivyo. Mapigano yamekuwa yakiendelea kwa siku kadha kati ya wanajeshi watiifu kwa Rais Salva Kiir na wanajeshi watiifu kwa Makamu wa Rais Dkt Riek Machar. Vituo vya Umoja wa Mataifa pamoja na maeneo ya raia pia yameshambuliwa, jambo...

Like
223
0
Monday, 11 July 2016
EURO 2016: URENO YATWAA UBINGWA
Slider

Ureno wameshinda michuano ya kandanda ya Ulaya, Euro 2016, kwa kuwafunga wenyeji Ufaransa 1-0 katika dakika za ziada kwenye mchezo wa fainali mjini Paris. Goli la ushindi lilifungwa na Eder katika dakika ya 110, na kusababisha huzuni kubwa kwa mashabiki wa Ufaransa waliofurika kwenye uwanja wa Stade de France. Ilikuwa furaha kubwa kwa mashabiki wa Ureno. Hii ni mara ya kwanza Ureno kushinda michuano mikubwa. Ureno walicheza kwa kujituma na ushirikiano bila ya mchezaji wao nyota Cristiano Ronaldo aliyetoka kutokana...

Like
415
0
Monday, 11 July 2016
WATU 12 WAFARIKI KUTOKANA NA FOLENI YA MAGARI
Global News

Watu 12 wamefariki nchini Indonesia kutokana na foleni ya magari iliyosababisha mamilioni ya watu kukwama barabarani siku kadha. Wengi walifariki kutokana na kukosa maji mwilini na uchovu. Watu wengi waliokuwa wakisafiri kwa sherehe za kuadhimisha mwisho wa mwezi mtukufu wa Ramadhan walikusanyika katika makutano ya barabara kisiwa cha Java. Na hapo ndipo msongamano mkubwa wa magari ulipotokea. Maafisa wa uchukuzi nchini Indonesia wanasema vifo hivyo vimetokea katika kipindi cha siku tatu. Vyombo vya habari nchini Indonesia vinasema wengi wa...

Like
294
0
Friday, 08 July 2016
MAREKANI NA KOREA KUSINI WAJILINDA DHIDI YA KOREA KASKAZINI
Global News

Marekani na Korea Kusini zimekubaliana kuweka mfumo wenye utata wa ulinzi dhidi ya makombora, kama njia ya kukakabiliana na vitisho vinayoendelea kutoka kwa Korea kaskazini. Mfumo huo wa ulinzi unaowekwa katika maeneo yenye milima mirefu kudhibiti mashambulizi ya makombora utawekwa kujibu vitisho tisho kutoka Pyongyang, ilieleza taarifa. Haijabainika wazi ni wapi mtambo huo utawekwa na hatimae ni nani ataudhibiti. Uchina, ambayo imekuwa ikipinga mara kwa mara mpango huo, imepinga mfumo huo tena kupitia wajumbe wa korea Kusini na Marekani....

Like
333
0
Friday, 08 July 2016
POLISI WATANO WAUAWA DALLAS, MAREKANI
Global News

Maafisa watano wa polisi mjini Dallas, Marekani wamepigwa risasi na kuuawa wakati wa maandamano ya kupinga mauaji ya watu weusi. Maafisa wengine sita wanauguza majeraha. Maafisa wa polisi katika mji ulio katika jimbo la Texas, wanasema mauaji hayo yametekelezwa na washambuliaji wawili wa kulenga shabaha. Mkuu wa polisi wa Dallas David Brown amesema amesema maafisa wa polisi bado wanakabiliana na mshukiwa mmoja ambaye anadaiwa kujibanza katika jumba linalotumiwa kuegesha magari. “Mshukiwa huyo ambaye tunawasiliana naye amewaambia maafisa wetu...

Like
241
0
Friday, 08 July 2016
SETELITE YA JUNO YAKARIBIA SAYARI YA JUPITA
Global News

Ile Setelite ya Juno iliiyosafiri kwa miaka mitano kwenda katika sayari ya Jupita sasa inakaribia kufika kwenye sayari hiyo.Wanasayansi wanakadiria setelite hiyo itafika muda mfupi ujao majira ya saa 12:15 asubuhi hii kwa saa za afrika mashariki. Setilite hiyo kama itafanikiwa kufika ilipokusudiwa kwenye sayari hiyo inatarajiwa kudumu kwa mwaka mmoja na nusu kuchunguza sayari jinsi...

Like
305
0
Tuesday, 05 July 2016
ICELAND WAPOKEWA KISHUJAA
Slider

Maelfu ya raia wa Iceland wamekusanyika katikati ya mji mkuu wa Reykjavik kukaribisha msafara wa timu yao ya taifa kwa mafanikio iliyopata kwenye michuano ya Kombe la mataifa Bingwa barani ulaya mwaka huu 2016. Wachezaji walipita katikati ya mji wakiwa ndani ya basi kubwa la wazi wakisindikizwa na ngoma hadi katika mlima wa Arnarholl ambapo mashabiki waliwasalimia kwa shangwe na makofi . Iceland ambayo imeshiriki kwa mara ya kwanza mashindano makubwa ya Kombe la mataifa barani Ulaya ilifikia ukingoni mwa...

Like
412
0
Tuesday, 05 July 2016
MCHEZAJI MWENYE ASILI YA DRC ATUA CHELSEA
Slider

Klabu ya Chelsea ya Uingereza imemsajili mshambuliaji wa Ubelgiji mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.Michy Batshuayi amehamia Chelsea kutoka klabu ya Marseille ya Ufaransa na kutia saini mkataba wa miaka mitano. Mamake ni Viviane Leya Iseka na babake Pino Batshuayi. Michy alikuwa na fursa ya kuchezea timu ya taifa ya DR Congo kutokana na asili ya wazazi wake lakini mwaka jana aliamua kuwa mchezaji wa Ubelgiji. Aliwachezea mechi ya kwanza dhidi ya Cyprus Machi 2015 na kufunga bao....

Like
282
0
Monday, 04 July 2016
NETANYAHU: ISRAEL INATAKA UHUSIANO NA AFRIKA
Global News

Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu ametua nchini Uganda katika ziara ya kwanza kabisa kwa kiongozi wa taifa hilo la kiyahudi kuzuru Afrika tangu mwaka wa 1987. Ziara hiyo ya siku 5 imeanzia Uganda, na kisha waziri Netanyahu anatarajiwa kuzuru Kenya, Rwanda na kisha Ethiopia. Ilikuwa kihoja kwa wageni waalikwa kuingia kwenye uwanja huo wa ndege kwani usalama uliimarishwa huku maafisa wa usalama wa Israeli wakishika doria na mbwa na walenga shabaha, mbali na upekuzi wa kawaida wa maafisa wa...

Like
211
0
Monday, 04 July 2016
APPLE KUNUNUA TIDAL YA JAY Z
Entertanment

Kampuni ya Apple inadaiwa kutaka kuchukua umiliki wa huduma ya kusikiliza muziki ya moja kwa moja ya mwanamuziki Jay Z Tidal. Kampuni hiyo imeripotiwa kwamba inaangazia wazo la kuinunua huduma hiyo kutokana na ushirikiano wake na wanamuzika bingwa kama vile Kanye West na Madonna. Duru zimearifu jarida la Wall Street kwamba mazungumzo yameanza na huenda yakasababisha kupatikana kwa makubaliano. Msemaji wa Tidal amekana kwamba imefanya mazungumzo na Apple. Jay Z alizindua huduma hiyo mnamo mwezi Machi mwaka uliopita kama mpinzani...

Like
243
0
Friday, 01 July 2016
MAHUJAJI WAISLAMU KUVALISHWA BANGILI ZA KIELEKTRONIKI
Global News

Saudia inatarajiwa kuwapatia bangili za kielektroniki mahujaji wanaoelekea Mecca kwa Hajj ya mwaka huu ambalo ni kongomano kubwa la Waislamu kutoka kote duniani. Hatua hiyo inafuatia mkanyagano uliotokea mwaka uliopita ambapo zaidi ya mahujaji 750 wanaaminikia kuuawa huku wengine 900 wakijeruhiwa. Bangili hizo zitakuwa na habari za kibinafsi za kila hujaji pamoja na zile za matibabu kusaidia mamlaka ya Saudia kuwatambua na kuwalinda mahujaji hao. Takriban kamera 1000 pia zimewekwa. Bangili hiyo ya utambulisho itukuwa na habari muhimu kama vile...

Like
242
0
Friday, 01 July 2016