Slider

RIO2016: WACHEZAJI KOREA KUSINI NA KASKAZINI WAJIPIGA SELFIE
Slider

Wanamichezo wa mazoezi ya viungo kutoka Korea Kusini na Kaskazini, ambao wanashiriki Michezo ya Olimpiki Rio 2016, wameuonesha ulimwengu ishara ya umoja, kwa kupiga selfie pamoja. Lee Eun-ju wa Korea Kusini na Hong Un-jong wa Kaskazini walipiga picha wakiwa wametabasamu wakati wa mazoezi kabla ya kuanza kwa michezo hiyo. Picha za wanawake hao wawili zimesifiwa sana kwa kuashiria moyo wa Olimpiki wa kuwaleta watu pamoja. Korea Kaskazini na Kusini huwa na uhasama mkubwa. Uhusiano baina ya nchi hizo mbili umedorora...

Like
206
0
Tuesday, 09 August 2016
SABABU YA SAMAKI KUPUNGUA ZIWA TANGANYIKA
Slider

Utafiti mpya umebaini kupungua kwa idadi ya samaki katika Ziwa Tanganyika, mojawapo ya maziwa muhimu zaidi kwa uvuvi duniani, kumetokana na ongezeko la joto duniani katika karne moja iliyopita. Ziwa Tanganyika ndilo la kale zaidi Afrika na samaki wake huwa muhimu sana kwa lishe katika mataifa yanayopakana na ziwa hilo.Lakini idadi ya samaki imepungua sana, huku wavuvi wakiendelea kuongezeka. Ongezeko hili la wavuvi lilidhaniwa kuwa chanzo kikubwa cha kupungua kwa idadi ya samaki.Lakini utafiti mpya unaonesha chanzo hasa ni ongezeko...

Like
418
0
Tuesday, 09 August 2016
DC KINONDONI: “JIAJIRI USISUBIRI KUAJIRIWA”
Slider

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Salum Hapi ametambulisha mradi mpya unaoenda kwa jina la ‘JIAJIRI USISUBIRI KUAJIRIWA’ mapema leo katika kipindi cha #JotoLaAsubuhi. Hapi amesema lengo la mradi huo ni kuwapatia  vijana mitaji inayotokana na vyanzo vya mapato ya Halmashauri ya wilaya ya Kinondoni ni sawa na asilimia 10 ya mapato yote yanayopatikana kwa mwaka mzima ambayo hutengwa kwa ajili ya Vijana na Wanawake. Amebainisha kuwa fedha nyingine wanategemea kuzipata toka kwa Rais Dk. John Pombe Magufuli ikiwa ni...

Like
528
0
Wednesday, 03 August 2016
PICHA: BWANA E AMWAGA WESE BUREEE TEMEKE, YOMBO BUZA
Slider

Wale wadau wa E-fm wenye sticker za namba ya bahati 93.7 wamebahatika kuwekewa wese full tank kutoka kwa Bwana E katika kituo cha mafuta cha Lake Oil Yombo Buza, zoei hili ni endelevu unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha unasikiliza Efm kujua eneo ambalo bwana E anapiga misele na kutunza Sticker...

Like
1648
0
Thursday, 28 July 2016
BARCELONA YARIPOTIWA KUFIKIA MAKUBALIANO NA JAVIER MASCHERANO
Slider

Klabu ya Fc Barcelona imerepotiwa kufikia makubaliano na mlinzi wake ‪Javier Mascherano‬ juu ya kuongeza mkataba wa kuendelea kusalia klabuni hapo kwa miaka mitatu zaidi kutoka kwenye mkataba wake wa awali. Taarifa hizi huenda zikazima ndoto ya mambingwa wa Serie A ‪ Juventus‬ ambayo ilikuwa ikimnyatia baada ya kumsajili ‪Dani Alves‬ kutoka klabu ya...

Like
272
0
Wednesday, 27 July 2016
GONZALO AKABIDHIWA JEZI NO 9
Slider

Nyota mpya wa klabu ya Juventus ya Italia Gonzalo Higuain amekabidhiwa jezi no 9 kwenye kikosi cha mabingwa hao wa ligi kuu ya Italia Serie A. Higuain mwenye umri wa miaka 28 amejiunga na Juventus kwa dau LA Euro million 94.7 akitokea Napoli pia ya Italia. Katika msimu uliopita nyota huyo amefunga magoli 36 akiweka rekodi hiyo kwenye ligi...

Like
260
0
Wednesday, 27 July 2016
ARSENAL YAPATA PIGO
Slider

Klabu ya Arsenal imepata pigo baada ya nyota wake Per Mertesacker kuripotiwa kuwa atakaa nje ya uwanja kwa muda wa miezi 5 akisumbuliwa na maumivu ya jeraha la goti. Beki huyo sasa ameondolewa kwenye msafara wa kikosi kitakachokuwa ziarani nchini Marekani kujiandaa na msimu mpya wa ‪#‎epl‬ utakaoanza mwezi ujao. Kwa mantiki hiyo inapotiwa kuwa nyota huyo atakaa nje ya dimba hadi mwaka...

Like
242
0
Tuesday, 26 July 2016
SAKHO MGUU NDANI,MGUU NJE NDANI YA LIVERPOOL
Slider

Maisha ya mlinzi wa kati wa Liverpool Mamadou Sakho yanaonekana kuanza kuwa magumu baada ya kocha wa klabu hiyo Jurgen Klopp kuamuru nyota huyo arudi nchini England kutoka Calfonia Marekani ambapo timu hiyo imeweka kambi kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu ya nchini England inayoanza kutimua vumbi mwezi ujao. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya uingereza kocha Jurgen Klopp hajafurahishwa na mwenendo wa kitabia wa nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 kwenye kambi yao huko Marekani nakuagiza...

Like
264
0
Tuesday, 26 July 2016
NEC YATAKA TUME HURU
Local News

Dar es Salaam. Baada ya kukamilisha Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka jana kwa mafanikio, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa mapendekezo saba kwa Serikali ili iyashughulikie kwa lengo la kuboresha uchaguzi ujao. Mapema mwezi huu, Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu, Damian Lubuva akiwa sambamba na wajumbe wengine wa taasisi hiyo na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), walikabidhi ripoti ya uchaguzi huo kwa Rais John Magufuli. Licha ya kueleza mafanikio yaliyopatikana katika kipindi chote cha mchakato huo, kuanzia...

Like
240
0
Tuesday, 26 July 2016
SUMTRA KUISHTAKI UDART KWA KUTOZA NAULI ZAIDI
Local News

Dar es Salaam. Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra), imesema wakati wowote kuanzia sasa itaufikisha mahakamani uongozi wa Mabasi ya Kwenda Haraka (Udart) kwa tuhuma za kuwatoza abiria nauli zaidi kinyume na matangazo yao. Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra, Gilliard Ngewe alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa, mashtaka dhidi ya uongozi huo yameshaandaliwa na kilichobaki ni kuyafikisha mahakamani. Ngewe alisema Udart inatoza nauli ya Sh650 badala ya 400 kwa ruti ya kutoka Mbezi hadi Kimara...

Like
384
0
Tuesday, 26 July 2016
LALIGA: HUU NDIO MKWANJA ULIOVUNWA NA BARCELONA KATIKA MSIMU WA 2015/16
Slider

Machampion wa kandanda nchini Hispania klabu ya Fc Barcelona imetangaza kuvuna kitita cha Euro million 679 katika msimu uliopita 2015/16 wa ligi kuu ya huko ‪#‎Laliga‬. Katika makusanyo hayo yaliyovunja rekodi klabu hiyo imetangaza kupata faida ya Euro milioni 29 baada ya makato ya kodi. Katika hatua nyingine klabu hiyo imetangaza mipango yake ya upanuzi wa dimba la Camp Nue kwa siku za usoni kupitia faida...

Like
384
0
Tuesday, 26 July 2016