Baada ya jana Ather Mwambeta kuishia kwa kutaja kikosi cha Simba tangu alivyojiunganayo leo anaendelea Ather anataja kikosi cha Yanga kilichoitesa Simba kwakuifunga miaka mitano Ni mchezo gani bora nje na ndani ya Tanzania ambao haujawahi kutokea kwa upande wake kwanini? Tanzania ingekuwa juu kisoka kama tungekuwa na kina Samatha wengi yeye amecheza soka kwa mafanikio je katika familia yake kuna mtu ambae anaweza kufuata nyayo...
Michezo mitatu itachezwa leo hii katika ligi mbalimbali barani ulaya katika ligi kuu ya soka ya nchini Hispania la liga kikosi cha kocha VICTOR FERNANDEZ Deportivo la corona wakiwa nyumbani katika uwanja wa Riazok watawakaribisha Eibar. Katika ligi ya bundesiliga ya huko ujerumani kocha ROBERTO DI MATEO akiwa katika uwanja wanyumbani atawaongoza vijana wake wa Schalke newfia au schalke 04 katika mchezo wao dhidi ya Borussia Monchengladbach. NA France ligi one klabu ya Saint Etienne ikiwa nyumbani itakipiga dhidi ya...
HABARI kutoka Libya zinasema kuwa idadi kadha ya wafanyakazi katika kisima kimoja cha mafuta wameuawa katika shambulio moja Jumanne usiku. Afisa mmoja mwandamizi wa kijeshi amesema kuwa watu kumi na watatu wameuawa katika kisima cha Mabrook. Watano ni raia wa kigeni, watatu wakiwa ni Wafilipino na wawili wanatoka Ghana. Afisa huyo amesema kuwa wote waliouawa walikatwa koromeo, mbali na Mlibya mmoja ambaye alipigwa risasi. Hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo, ingawa taarifa za watu walioshuhudia tukio hilo wanasema watu...
MFALME wa Jordan ameahidi mapambano yasiyo na huruma dhidi ya wapiganaji wa Islamic State kufuatia kuuawa kwa rubani wa nchi hiyo. Baada ya mkutano wa makamanda wa juu wa jeshi na maafisa usalama, Mfalme Abdullah amesema vita hivyo vitaelekezwa dhidi ya kundi hilo na damu ya rubani huyo wa ndege za kivita Muath al-Kasasbeh haitapotea bure. Hapo jana, Jordan iliwanyonga wafungwa wawili wapiganaji wenye msimamo mkali waliokuwa katika orodha ya adhabu ya kifo, kama kulipiza kisasi cha kuuawa kwa rubani...
TAASISI ya Usafirishaji na Uchukuzi Tanzania- CILT inatarajia kufanya mkutano mkuu wa kimataifa utakaohusisha nchi mbalimbali za bara la Afrika kuanzia machi 4 mwaka huu. Mkutano huo utahudhuriwa na wanachama wa CILT, Maafisa wa Sekretarieti ya Taasisi hiyo makao makuu mjini londan, wanachama kutoka nchi zingine nje ya Africa sambamba na viongozi wa Taasisi za uchukuzi wa lojistiki na wadau wengine. Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam Kaimu Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Taasisi ya CILT...
TANZANIA imesema kuwa dhamira yake ya kufungua balozi katika baadhi ya nchi duniani iko pale pale na itatekeleza mpango wake huo kwa kadri hali ya fedha na uchumi inavyoruhusu. Aidha, Tanzania imesema kuwa itaendelea kushirikiana na Iran katika kupambana na kukabiliana na ugaidi duniani kwa sababu nchi mbili hizo, kama ilivyo dunia nzima, zinahitaji dunia tulivu na inayosaka maendeleo ya watu bila usumbufu na vitisho vya ugaidi. Mambo hayo mawili yamejadiliwa katika mazungumzo kati ya Rais wa Jamhuri ya...
MAAFISA wa Marekani wamesema vikosi vya jeshi la Marekani vimefanya shambulio nchini Somalia dhidi ya kiongozi mwandamizi wa kundi la al-Shabaab. Shambulio hilo lililofanywa Januari 31 kwa kutumia ndege isiyo na rubani kusini mwa mji mkuu Mogadishu lilimlenga Yusef Dheeq , mkuu wa operesheni za nje na mipango ya upelelezi na usalama wa kundi hilo. Hata hivyo haijathibitishwa iwapo ameuwawa katika operesheni hiyo. Shambulio hilo ni kampeni ...
SERIKALI ya Jordan imewanyonga Wairaq wawili kwa kulipiza kisasi kwa kuuliwa raia mmoja wa nchi hiyo na kundi la Dola la Kiislamu. Hatua hiyo ya kunyongwa imekuja saa chache baada ya kutolewa video inayoonesha rubani wa jeshi la Jordan akichomwa moto akiwa hai. Ripoti za televisheni ya taifa zinasema rubani huyo aliuwawa kiasi mwezi mmoja uliopita. Mchambuzi wa masuala ya mashariki ya kati Randa Habib amesema mauaji hayo ...
VIONGOZI wa dini nchini wametakiwa kuwaelimisha waumini wao kuachana na matumizi mabaya ya mitandao ya mawasiliano ili kuinusuru jamii na athari mbaya za mitandao hiyo. Akizungumza katika semina ya viongozi wa dini leo jijini Dar es salaam iliyo andaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano nchini -TCRA- Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Profesa JOHN NKOMA amewataka viongozi wa dini kuwaelimisha waumini wao kuepuka matumizi mabaya ya mitandao ya mawasiliano kwani ina mchango mkubwa katika kuharibu maadili ya jamii hususani vijana na watoto....
WABUNGE wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania, wamewataka viongozi wa serikali hususani mawaziri na manaibu wao kufanya tathimini ya kutosha juu ya maswali mbalimbali yanayoulizwa ili kutoa majibu sahihi naya kuridhisha kwa manufaa ya Taifa. Wito huo umetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na mbunge wa kigoma kaskazini mheshimiwa ZITTO KABWE wakati akiomba mwongozo kufuatia majibu yaliyotolewa na Naibu waziri wa Nishati na Madini mheshimiwa CHARLES MWIJAGE kwa baadhi ya maswali ya wabunge yaliyoelekezwa kwa wizara hiyo katika kipindi...
ASSA MWAMBETA ninani alitokea wapi na alianza kucheza soka lini. MWAMBETA akiwa anaishi ilala kota pia aliendelea kucheza mpira katika timu mbali mbali. ASSA anaelezea jinsi alivyo hamia simba ambayo ilikuwa ikijulikana kama Sunderland. Alikitumikia kikosi hicho cha Sunderland kwa misimu mingapi. KATIBU MKUU WA AFRICANSPORTS KHATIBU ENZI: Nini kiliipoteza African sports kwenye ramani ya soka kwa kipindi kirefu na ilikuwa wapi kwa kipindi chote hicho kuna mikakati gani kuhakikisha timu inafanya vizuri ligi...