video hiyo inaandaliwa chini ya kampuni ya Next level na inatarajiwa kutoka hivi...
POLISI nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wamewafyatulia risasi waandamanaji kwenye mji mkuu Kinshasa walio na hasira katika kile kinachoonekana kama jitihada za kutaka kuongoza uongozi wa rais Joseph Kabila. Watu kadha walitolewa eneo la katikati mwa mji wakiwa na majeraha ya risasi ambapo pia kulitokea makabiliano kwenye chuo kikuu cha mji huo. Milio ya risasi iliripotiwa katika maandamano mengine katika mji ulio mashariki wa Goma....
UTAWALA nchini Malawi umesema kuwa umewaokoa maelfu ya watu ambao walikuwa wamekwama kutokana na mafuriko ambayo yameikumba nchi hiyo. Wanajeshi walitumia mashua na ndege za helikopta kuwahamisha watu kwenda maeneo yaliyoinuka kufuatia kuharibiwa kwa barabara na madaraja. Takriban watu 200 wameripotiwa kufariki dunia huku wengine laki 2 wakilazimika kuhama makazi yao....
WANANCHI wameombwa kusaidiana na Jeshi la Polisi kutoa taarifa haraka pindi wanapoona tukio la uhalifu au kuona umiliki wa silaha kinyume na sheria ili kuweza kulinda amani na ulinzi wa Taifa . Wito huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Wilaya ya Temeke SOPHIA MJEMA kwenye sherehe ya utoaji sifa na zawadi kwa Maafisa, Wakaguzi na Askari wa vyeo mbalimbali. MJEMA amefafanua kuwa ni muhimu wananchi kushirikiana na Polisi ili kuweza kupunguza matukio ya uhalifu na kuongeza...
IDARA ya Ajira Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imetoa rai kwa vijana wote nchini waliopo shuleni kujikita zaidi kwenye taaluma ya masomo ya sayansi kwani sekta ya Sayansi ni moja ya Sekta yenye uhitaji mkubwa wa wataalam hao katika Nyanja mbalimbali za utumishi wa umma. Rai hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Katibu Msaidizi kutoka Idara ya Ajira katika Utumishi wa Umma MALIMI MUYA alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari. Bwana MUYA amefafanua kuwa uhaba wa...
Hili ni daraja linalopatikana nchini Ujerumani Ujenzi wa daraja hili lenye maajabu yake duniani ulianza mnamo mwaka 1930 ambapo halikukamilika kufuatia vita kuu ya pili ya dunia hivyo ujenzi wake ulisimamishwa hadi mnamo mwaka 1997 mradi wa ujenzi uliendelezwa na lilifunguliwa rasmi mwaka 2003. Daraja hili limekuwa likitumika na watu kusafirishia bidhaa kwa njia ya meli za mizigo lakini pia watu hutumia kuvuka upande mmoja kwenda mwingine na zaidi limekuwa kivutio kikubwa cha utalii Daraja hili limepewa jina la Magdeburg...
Polisi Moro imeibana Coastal Union kwao Mkwakwani mjini Tanga. Wageni hao wameikomalia Coastal na kuilazimisha sare ya bila kufungana. Polisi Moro ilipoteza nafasi mbili za kufunga katika kipindi cha kwanza. Lakini Coastal nayo ilishindwa kufunga katika kipindi cha pili baada ya kupata nafasi zaidi ya mbili. Hata hivyo, Polisi ilionyesha soka safi la pasi za uhakika na kumiliki mpira muda mwingi licha ya kuwa ugenin MECHI YA COASTAL UNION DHIDI YA YANGA YAAHIRISHWA Mechi kati ya Coastal Union dhidi Yanga...
KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis anarejea mjini Rome leo baada ya ziara ya wiki moja barani Asia ambako aliwavutia mamilioni ya watu na kuuwasilisha ujumbe wa kuwatetea masikini. Baba Mtakatifu alizitembelea Sri Lanka na Ufilipino katika ziara yake ya pili katika bara hilo, mnamo muda wa miezi mitano. Hapo jana kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki aliongoza sala iliyohudhuriwa na waumini milioni sita katika mji mkuu wa Ufilipino, Manila. Na katika ujumbe wake,Papa Francis kwa mara nyingine amewataka watu...
WAPIGANAJI wa kundi la kigaidi la Boko Haram wamewateka nyara watu zaidi ya 60 baada ya kufanya shambulio kaskazini mwa nchi jirani ya Cameroon. Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, magaidi hao walifanya shambulio hilo hapo jana, yaani siku moja baada ya Chad kuwapeleka wanajeshi wake nchini Cameroon, ili kupambana na magaidi hao. Afisa mmoja wa polisi ameliambia shirika la habari la AFP kwamba, wapiganaji wa Boko Haram walivivamia vijiji viwili vya kaskazini mwa Cameroon hapo jana na walizichoma moto...
MAMLAKA ya Utabiri wa Hali ya Hewa Tanzania-TMA, imetoa tahadhari ya kuwepo kwa vipindi vya mvua kubwa inayozidi milimita 50 ndani ya saa 24 kati ya Januari 18 na 20 mwaka huu. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mamlaka hiyo kwa vyombo vya habari jijini Dar es salaam, maeneo yatakayoathirika na Mvua hiyo ni pamoja na Mikoa ya Ruvuma, Mtwara, Lindi, Morogoro, Pwani, Dar es salaam na Kisiwa cha Unguja. Taarifa hiyo imeeleza kuwa hali hiyo inatokana na kuimarika kwa...